Wachezaji wa kibongo uwezo wa kujisimamia, kujielimisha,nidhamu binafsi ni ndogo.
Naamini mpaka sasa wengi wameshindwa kujifunza kwa Mbwana Samatta.
Nakumbuka kuna wakati Samatta akiwa TP Mazembe, kila akirudi nyumbani wachezaji alikuwa anashangaa wenzie wanamuulizia radio(portable radio),wala sio namna ya kutoka hapo walipo na kufikia njia za kuwafikisha timu kubwa nje ya nchi.
Nishauri wachezaji kupitia chama chao waombe mafunzo ya kuwafanya wawe 'professional players':
Wakipata fedha waweke wataalamu wa kuwasimamia mambo yao(mfano wakala,msemaji na meneja).
Wakiyafanya hayo,natarajia wachezaji wengi watabadilika,
Labda,sasa watajitambua kama wanamuziki wa Bongo flavour(wana watu wanasimamia mambo yao).
KAMA MCHEZAJI,NI STAA NA YUPO TIMU KUBWA,basi angalau
1.mwisho wa msimu awe na CD yenye matukio yenye kuonyesha uwezo wake.
2.awe na mwanasheria wake,kwa ajili ya kuchambua haki na swahili zake.
3.atafute shule ya kujiendeleza,aidha lugha(kifaransa,kispanish,au kiingereza),au taaluma nyingineyo.
4.awe na wakala atakaye kuwa anafuatilia maendeleo yake.
5.kuepuka kuonyesha vitendo vya ukosefu nidhamu awapo uwanjani.
Wakati mwingine vilabu vimekuwa chanzo cha kushindwa kulea ubora na maisha ya wachezaji kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi uendeshaji vilabu.