Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Nilizoea kuwaona wachina Dar es Salaam tu lakini nimeshangaa kuwakuta wachina hadi huko Kigoma vijijini, mwanzo nilidhani labda ni wakandarasi kwenye miradi ya barabara, lakini hapana, unawakuta wapo barabarani wanazurura, nilishangaa mpaka wanauza vyombo, yaani wanakodi gari na kuanza kukopesha vyombo kwenye taasisi za kiserikali.
Nimejikuta nashangaa tu, maana hata Kariakoo siku hizi na wao wanamiliki maduka, Juzi mmesikia Kuna boat kutoka Kigoma kwenda Congo inaitwa mama Benita ilizama, wachina walikuwa kama 6 hivi, Hawa jamaa ni wanasaka opportunity sehemu yoyote ile, nadhani upambanaji wao ndio unawafanya hata nchini kwao kutajirika.
Tumeng'ang'ania kukaa mijini tukiwa na maisha ya ufukara lakini hawa jamaa nadhani wameingia Kwa Kasi kutufundisha kitu.