Kwanini wafanyabiashara wadogo 20s-30s waliotoboa wakifilisika ni ngumu kujirudi lakini wanaoanza kushika pesa kwenye 40s ni nadra kudondoka?

Umetema madini yenye kiwango cha A+
 
Tusimulie tujifunze ndugu ,hela Hana adabu kabisa
Ni historia ndefu kdg, lkn kwa ufupi tu, nilivyomaliza chuo nikiwa na age ya late 20s kuna mkondo wa hela niliupata, nikanunua assets kadhaa, i.e viwanja, nikafungua biashara kadhaa na gari safi ya kutembelea..hapo sasa starehe zikaanza rasmi, clubs na mimi, pombe na mimi, nawinda slay queens kila kona...baada ya miaka minne mbele.....Doooooh!!! nilishafulia hata sieleweki, kila kitu nimeuza, hata pesa ya kula ni mtiti..hakuna rangi sikuacha kuona! nilifikia hadi kufikia kubeba zege na Masters yangu ili nipate msosi niwe hai tu, nimefanya kazi za kitumwa sana maana ilibidi nikimbie mkoa kbs, nilipata majuto makali sana! but kwa sasa nimesimama, biashara inatengeneza faida kubwa, nimekuwa na comeback ya nguvu sana...KINACHONIBEBA KWA SASA, 1. Ukomavu wa kimaisha i.e Sina mambo mengi mfano starehe, marafiki wachache ambao ni sahihi 2. Hofu ya kurudi kwenye msoto, inafanya niwe makini zaidi 3. Ninapambana sana kusaka maarifa mapya hasa ktk nyanja za biashara...nk Naamini siwezi kuanguka tena!
 
Good experience
 
Wewe jamaa unayajua sana maisha,,hii comment ni dawa kubwa sana ambayo watu wengi hawaijui
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…