Uchaguzi 2020 Kwanini Wagombea wanalazimisha kuchaguliwa?

Uchaguzi 2020 Kwanini Wagombea wanalazimisha kuchaguliwa?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Katika kufuatilia kampeni hasa za urais, ni wazi kuwa zoezi zima la kuomba kura lisiporatibiwa vyema zaidi, kwa ujumla wake, linakuwa halina tofauti na mtu anayelazimisha ndoa.

Ndoa ni jambo la kheri lakini sasa ikilazimishwa pasipokuwa na maridhiano, kha! Hiyo inakuwa si ndoa tena, bali inageuka kuwa ni uchuro!

Rais wetu ni mtumishi wetu. Shida na raha zetu zinapaswa kuwa zake.

Tunazo shida nyingi. Ni muhimu akazitambua na tukawa na makubaliano. Katika jitihada za kuwafahamisha watia nia wetu, tumekwenda mbali na kuziorodhesha shida zetu, tukionyesha dhahiri tunataka rais wa namna gani:

Kwenu watia nia, hasa wale wa Urais

Kimsingi tunataka rais huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Wagombea wanapaswa wajipime tokea katika tunayotaka wakatia nia au wakachomoa kama wako nje ya tuyatakayo. Wagombea hawawezi kuja na ya kwao kuja kuyalazimishia kwetu. Sisi ndiyo tunaoweka listi ya mahitaji na katu haiwezi kuwa wao.

Kwa nini kutulazimisha na madege, viwanja vya madege, viwanja vya mipira nk ambavyo si vipaumbele vyetu na wala hatujaomba kokote na hasa kwa sasa?

Sisi tumemtaka nani akanunue madege? Kupitia jukwaa lipi? Eboo! Mbona hivi?

Wagombea, jipimeni wenyewe tafadhalini msitulazimishe wala kitufokea!

Mnatukwaza kwa kweli kwa kutokuona aibu hii nyie wenyewe. Msingoje kuambiwa jamani, ndoa hailazimishwi labda kama ni ya mkeka.

Mgombea atusikilize tunataka nini na tumhoji. Ajabu ni kuwa kuna baadhi yao hata midahalo hawaitaki!

Hivi mna agenda za kutumikia kweli nyie au janja janja za kutuhadaa tuwape rungu matokeo yake mje kututawala kwa mabavu tu?

Jamani, mdada kulazimisha ndoa ni uchuro kama ilivyo kwa mkaka pia."

Ndoa ni maridhiano. Tukutane kwenye midahalo tubarizi tuulizane na kujiridhisha kuwa tumeridhiana. Bila hivi ndoa hiyo isiyokuwa na maridhiano itakuwa vipi?

Hutaki mdahalo, nenda tu katulizane na ng'ombe wako wala tusijuane.

Wagombea tutendeeni haki wengine tunawaonea hata aibu kuwaambia maana sasa mmepitiliza. Kwa hakika mmekuwa zaidi ya mdada anayelazimisha ndoa.

Kha! Uchuro huu jamani!
 
nwingine anatutishia amani eti tusipomchagua tutajuta kwa kuwa hakuna kama yeye

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app

Maajabu ya Firauni kazini.

Hata wale wa propaganda wao naona pumzi imekata au labda wako semina kwa maana hali kwao ni mbaya mno. Kimbunga cha Lissu kitakuwa kimewaacha hoi. Watakuwa hawaelewani na ni full kuweweseka!

Au labda malimbikizo ya zile buku zao yamewavunja nguvu.

Si the lager, evodiya, ngedere na crew nzima ya buku 7 yote imeingia mitini.

Pesa kitu gani?

Nini kama nguvu ya umma?
 
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Katika kufuatilia kampeni hasa za urais, ni wazi kuwa zoezi zima la kuomba kura lisiporatibiwa vyema zaidi, kwa ujumla wake, linakuwa halina tofauti na mtu anayelazimisha ndoa...


Mleta mada tafadhali sana, kwa upendo kabisa agiza kiasi chochote cha kinywaji unachokipenda kwa bili yangu.

Wewe ni kichwa!

Critical thinker.

Kudos!!!!
 
Watanzania Mpeni Lissu urais ni mtu mwenye sera bora kabisa, ni mtu mwenye akili kubwa sana, ni mtu atakayeyutengrnezea mifumo thabiti ya kisheria katika Taasisis zetu.

Achaneni one man shows Dikteta uchwara.
 
jiwe alishajua nchi hii mali yake

Yeye na washirika wake kina chamia, machaliwa, bashiri, mpole mpole, wapara magamba, mbulembo, vibajaji, mchukuma na wote wa namna hiyo wamekuwa wakiota ndoto za mchana.

Mgombea anayejibu hoja za matarajio yetu ndiye aliyechaguo letu. Bi dada asitulazimishe ndoa. Uzuri hii ni ya ridhaa na si ya mkeka!
 
Watanzania Mpeni Lissu urais ni mtu mwenye sera bora kabisa, ni mtu mwenye akili kubwa sana, ni mtu atakayeyutengrnezea mifumo thabiti ya kisheria katika Taasisis zetu.

Achaneni one man shows Dikteta uchwara.

Naunga mkono hoja.
 
nwingine anatutishia amani eti tusipomchagua tutajuta kwa kuwa hakuna kama yeye.

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app

Ujasiri wa namna hii bi dada anayeomba kuolewa anaupata wapi?

Si atuache tule hasara kwa kutokumchagua yeye?

Wafaidika ni sisi tukikuchagua kwa nini unahangaika hivyo? Kweli ni kwa kutuonea huruma huku hutaki kutokea kwenye mdahalo tikakuhoji?

Mgombea wa hivi ni wa kuogopa kuliko ukoma!

Kwa hakika huyu mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo.
 
Kuna mtu anatufokea eti tusichague kwa majaribio, ebo!

Kasema pia kuwa wasipewe nchi wasioaminika. Sijui wanapimwa vipi wasioaminika au ni vipi yeye anaaminika.

Maajabu ya Firauni.
 
Huyu mmoja yeye anasema 2025 atamuachia mwingine wa CCM! Yeye tayari ni mshindi na hahitaji kura zetu! Tume ya uchaguzi itafuata maelekezo ya mteule.
 
Back
Top Bottom