Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Katika kufuatilia kampeni hasa za urais, ni wazi kuwa zoezi zima la kuomba kura lisiporatibiwa vyema zaidi, kwa ujumla wake, linakuwa halina tofauti na mtu anayelazimisha ndoa.
Ndoa ni jambo la kheri lakini sasa ikilazimishwa pasipokuwa na maridhiano, kha! Hiyo inakuwa si ndoa tena, bali inageuka kuwa ni uchuro!
Rais wetu ni mtumishi wetu. Shida na raha zetu zinapaswa kuwa zake.
Tunazo shida nyingi. Ni muhimu akazitambua na tukawa na makubaliano. Katika jitihada za kuwafahamisha watia nia wetu, tumekwenda mbali na kuziorodhesha shida zetu, tukionyesha dhahiri tunataka rais wa namna gani:
Kwenu watia nia, hasa wale wa Urais
Kimsingi tunataka rais huyu:
Wagombea wanapaswa wajipime tokea katika tunayotaka wakatia nia au wakachomoa kama wako nje ya tuyatakayo. Wagombea hawawezi kuja na ya kwao kuja kuyalazimishia kwetu. Sisi ndiyo tunaoweka listi ya mahitaji na katu haiwezi kuwa wao.
Kwa nini kutulazimisha na madege, viwanja vya madege, viwanja vya mipira nk ambavyo si vipaumbele vyetu na wala hatujaomba kokote na hasa kwa sasa?
Sisi tumemtaka nani akanunue madege? Kupitia jukwaa lipi? Eboo! Mbona hivi?
Wagombea, jipimeni wenyewe tafadhalini msitulazimishe wala kitufokea!
Mnatukwaza kwa kweli kwa kutokuona aibu hii nyie wenyewe. Msingoje kuambiwa jamani, ndoa hailazimishwi labda kama ni ya mkeka.
Mgombea atusikilize tunataka nini na tumhoji. Ajabu ni kuwa kuna baadhi yao hata midahalo hawaitaki!
Hivi mna agenda za kutumikia kweli nyie au janja janja za kutuhadaa tuwape rungu matokeo yake mje kututawala kwa mabavu tu?
Jamani, mdada kulazimisha ndoa ni uchuro kama ilivyo kwa mkaka pia."
Ndoa ni maridhiano. Tukutane kwenye midahalo tubarizi tuulizane na kujiridhisha kuwa tumeridhiana. Bila hivi ndoa hiyo isiyokuwa na maridhiano itakuwa vipi?
Hutaki mdahalo, nenda tu katulizane na ng'ombe wako wala tusijuane.
Wagombea tutendeeni haki wengine tunawaonea hata aibu kuwaambia maana sasa mmepitiliza. Kwa hakika mmekuwa zaidi ya mdada anayelazimisha ndoa.
Kha! Uchuro huu jamani!