Cytochrome p450
JF-Expert Member
- Mar 19, 2019
- 5,638
- 15,044
Sababu kubwa inayopelekea ungezeko la akili kwa watu wa kanda ya ziwa ni kutokana na ulaji mwingi wa SAMAKI.
Tuanzie hapa..
KWANINI SAMAKI?
Uchunguzi wa kisayansi uliofanyika unatujuza kuwa, Samaki wana asili ya mafuta (unsaturated fats) kwenye miili yao inayoundwa na kemikali ziitwazo Omega-3.
Kwa kawaida,mwili wa binadamu hauna uwezo wa kutungeneza hizi lakini ni muhimu. Kwahiyo tunahitaji kuzipata kutokea kwenye ulaji wa Samaki.
Sasa unapokula samaki kwa wingi, ni dhahiri kwamba unaongeza kiasi kikubwa cha Omega-3 kwenye mwili.
Tuje sasa kwenye Ubongo wa binadamu.
Ubongo wa binadamu umeundwa na nyaya/mishipa ya fahamu mingi iitawayo Neurone/ Nerve cell. Hizi ndio hutumika katika kusafirisha taarifa zote ndani ya mwili wa binadamu zilizoamuliwa na ubongo.
Katika muundo wa Neurone, kuna mafuta yanayoizunguka na kuilinda hizo mishipa ya fahamu (Myelin Sheeth) lengo ni kusaidia kulinda zisiharibiwe, kuepusha taarifa zisivuje kutoka nje (kupotea kwa taarifa zilizotafsiriwa na ubongo) na hivyo kuongeza speed ya taarifa zilizobebwa na ubongo kwenda sehemu husika.
Kwahiyo tunapoongeza Omega-3 kwenye mwili, inaenda kusaidia kuimarisha ukuaji wa kuta za Myelin Sheeth na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kazi zao.
Pia, Omega-3 inachochea ongezeko la mtiririko wa damu kwenda kwenye ubongo jambo linalosaidia ubongo kupata Glucose (sukari) ambayo ni muhimu kama chakula chake na hivyo ubongo huweza kupata afya zaidi.
Kwa hali ya kawaida mtu anapokula vizuri akashiba na akaridhika, tunategemea mtu anawiri, Right?
Sasa ni hivyo hivyo kwa ubongo, inapelekea kuongezeka kwa mwingiliano mzuri wa mishipa ya fahamu (Nerve Cell Networking) ambapo huongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufikiri na kuvuta picha (Imagination).
Kwa takwimu zilizofanywa na wazungu nchini Tanzania katika miaka 10 iliyopita zinaonyesha kuwa, asilimia kubwa ya wamama wajawazito wanaoishi kwenye ukanda wa Ziwa Victoria ndio wanaongoza kwa ulaji mwingi wa Samaki wa maji baridi hivyo kupelekea watoto wao kufaidika zaidi na virutubisho hivyo na ndio hupelekea kuzaliwa wa watoto wenye upeo mkubwa wa akili.
BADO HUJACHELEWA, ANZA KULA SAMAKI LEO!