Kwanini Wahindu wanawachukia sana Waislam ambao ni ndugu zao na kuwapenda Wakristo na Wabudha?

Kwanini Wahindu wanawachukia sana Waislam ambao ni ndugu zao na kuwapenda Wakristo na Wabudha?

Umaskini ukikutana na itikadi za msimamo mkali ni kama kiberiti kilichowashwa karibu na petrol.
Kama tatizo lingekuwa Waislamu kwani Dubai wengi wao ni wa dini gani na msuguano kama huo umeuona?

Qatar napo kuna Wahindi wengi msuguano kama huo umeuona?

Kuwait kuna Wahindi wengi msuguano wa namna hiyo umeusikia?

Kote huko Wahindi wana nyumba zao za ibada.

Kuna kipindi ilikuwa ni mwezi wa Ramadhani futari iliandaliwa kabla ya kuswali magharibi ili baada ya swala watu wale. Kwa ghafla kundi la nyani likavamia na kula futari. Kumaliza swala nyani wanakula futari.

Viongozi wakasema tusiwafukuze! Wakaenda temple ya karibu kuwaambia kuna suala limetokea kwenye nyumba yetu ya ibada tunaomba mtusaidie kuli tatua. Walipofika wakakuta nyani wanakula futari, walifurahi sana! Wakalipia gharama ya chakula chote kwa ujumla. Sikujua ina maanisha nini! Kuuliza nikaambiwa ile temple nyani ni mungu wao! Tungeliwakimbiza laiti wangelituona ingelikuwa mtafaruku mkubwa! Wahindu wana miungu mingi! Kuwa makini na kila kiumbe ukiwa kwenye jamii yao hususani India.

Kwa Waislam kuna dhehebu linaloitwa Salafi. Salafi nao wamegawanyika; kuna wa moto kiasi na wa moto kabisa. Hawa chao ni sahihi cha kwako si sahihi, ukimfuata upo sahihi usipomfuata umepotea. Hawa ndoa zao wanafungishana wao tu! Wengine wanafika mbali kabisa asie Muislam kwao wanamuona amekuja bahati mbaya duniani. Fahamu pia; mpaka Waislamu dheheb la Sunni kwa upande wa Salafi wanawaona Sunni wamepotea hivyo utapewa majina mabaya kweli.

Sasa Muhidu mwenye dini nyingi na miungu mingi wawe ndani ya jamii moja na Salafi unategemea nini? Chuki itakuwepo baina yao na uhasama mkubwa!
 
Shida ni Mafundisho ya Dini ya Uislamu, Waislamu wanafundishwa kwamba Mtume Muhammad (SAW) ndiyo wa mwisho kwa maana hiyo hakuna mwingine hivyo basi binadamu wote ni lazima wamkubali na kumfwata, shida inaanzia hapo, tatizo la India ni kwamba Uislamu hauutambui Uhindu na Waislamu wanaamini kwamba watu wote mwishowe ni lazima wawe Waislamu.

Hata Ukristu ulikuwa hivyo zamani lkn tofauti ni kwamba Ukristu unabadilika na muda wakati Uislamu uko vile vile, hivyo siyo India tu hata hapa Tanzania ni swala la muda tu kabla hakijanuka, kwa sababu ya kuamini hivyo nilivyoandika hapo juu, kwa maana nyingine kwa Muislamu kama wewe siyo Muislamu kwa upande wake ni kwamba ubinadamu wako una mapungufu au kasoro hata kama hatokwambia usoni lkn deep inside anaamini hivyo, …
Amna kitu kama icho Uislamu hauna chuki na dini nyingine yoyote ikiwa na wao wanaishi na nyinyi kwa upendo tuje kwenye kipindi cha uhai wa mtume s.a.w aliishi kwenye mji mmoja na watu wa dini nyingine wasiokuwa waislamu na wala akuwadhuru ..usome uislamu vizuri kiufupi wahindu ni wabaguzi kupita kiasi kwenye dini yao wenyewe mtu mweusi amelaaniwa yani ni wabaguzi grade A duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imani nikitu hatari sana nihisia za ndani kabisa kwa mwanadamu kwa hiyo kila mtu anacho amini hapo ndio utata unakuja mwingine kulazimisha kuamini asicho kiamini mwisho mauaji, chuki na kutengana

MUNGU ATUNUSULU KWA TAIFA LETU.
Kwenye uislamu hakuna kulazimishana kwenye dini kama mtu amekataa kusilimu na kuwa muislamu upaswi kumfanyia vitimbi vyovyote unatakiwa kumuacha na vile vile kuitusi dini za wengine ni haramu kwenye uislamu .. Uislamu ni amani na upendo na wala siyo chuki na vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kona ya hii dunia Dini ya kiislamu ni shida. Inapigwa vita na wazungu , wachina na wahindi na shida ni ile ile waislamu wanataka kulazimisha dini yao ifuatwe kwa nguvu kitu ambacho akikubaliki kwa dunia ya saiv ambayo dini ni hiyari ya mtu.
Narudia tena hakuna kulazimishana kwenye uislamu kama mtu amekataa kusilimu aitakiwi kumlazmisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tatizo lingekuwa Waislamu kwani Dubai wengi wao ni wa dini gani na msuguano kama huo umeuona?

Qatar napo kuna Wahindi wengi msuguano kama huo umeuona?

Kuwait kuna Wahindi wengi msuguano wa namna hiyo umeusikia?

Kote huko Wahindi wana nyumba zao za ibada.

Kuna kipindi ilikuwa ni mwezi wa Ramadhani futari iliandaliwa kabla ya kuswali magharibi ili baada ya swala watu wale. Kwa ghafla kundi la nyani likavamia na kula futari. Kumaliza swala nyani wanakula futari.

Viongozi wakasema tusiwafukuze! Wakaenda temple ya karibu kuwaambia kuna suala limetokea kwenye nyumba yetu ya ibada tunaomba mtusaidie kuli tatua. Walipofika wakakuta nyani wanakula futari, walifurahi sana! Wakalipia gharama ya chakula chote kwa ujumla. Sikujua ina maanisha nini! Kuuliza nikaambiwa ile temple nyani ni mungu wao! Tungeliwakimbiza laiti wangelituona ingelikuwa mtafaruku mkubwa! Wahindu wana miungu mingi! Kuwa makini na kila kiumbe ukiwa kwenye jamii yao hususani India.

Kwa Waislam kuna dhehebu linaloitwa Salafi. Salafi nao wamegawanyika; kuna wa moto kiasi na wa moto kabisa. Hawa chao ni sahihi cha kwako si sahihi, ukimfuata upo sahihi usipomfuata umepotea. Hawa ndoa zao wanafungishana wao tu! Wengine wanafika mbali kabisa asie Muislam kwao wanamuona amekuja bahati mbaya duniani. Fahamu pia; mpaka Waislamu dheheb la Sunni kwa upande wa Salafi wanawaona Sunni wamepotea hivyo utapewa majina mabaya kweli.

Sasa Muhidu mwenye dini nyingi na miungu mingi wawe ndani ya jamii moja na Salafi unategemea nini? Chuki itakuwepo baina yao na uhasama mkubwa!
Dubai imejaa wageni sio waarabu na ndio maana makanisa yapo kibao na hata majengo mengi ni wazungu, wahindi na wachina wapo
 
Shida ni Mafundisho ya Dini ya Uislamu, Waislamu wanafundishwa kwamba Mtume Muhammad (SAW) ndiyo wa mwisho kwa maana hiyo hakuna mwingine hivyo basi binadamu wote ni lazima wamkubali na kumfwata, shida inaanzia hapo, tatizo la India ni kwamba Uislamu hauutambui Uhindu na Waislamu wanaamini kwamba watu wote mwishowe ni lazima wawe Waislamu.

Hata Ukristu ulikuwa hivyo zamani lkn tofauti ni kwamba Ukristu unabadilika na muda wakati Uislamu uko vile vile, hivyo siyo India tu hata hapa Tanzania ni swala la muda tu kabla hakijanuka, kwa sababu ya kuamini hivyo nilivyoandika hapo juu, kwa maana nyingine kwa Muislamu kama wewe siyo Muislamu kwa upande wake ni kwamba ubinadamu wako una mapungufu au kasoro hata kama hatokwambia usoni lkn deep inside anaamini hivyo, …
Dini zililetwa na waarabu na wazungu, na walitukuta tukiabudu na kupata matokeo ya ibada zetu, mtu anakuja anakwambia wewe ni khafiri na ukimuu khafiri mmoja unapata thawabu mbinguni.

Huu ni ujinga mkubwa sana
 
Mimi ni Muislam. Nimeusoma Uislam na bado naendelea kuusoma Uislam.

Ukisema unafuata sharia kwa maana muungozo wako wote wa masuala ya mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla utafuata muongozo wa sharia ambazo ni za Kiislam. Nazo zinatoka kwenye:

-Quran
-Sunna
-Ijtamaa (ya wanawazuoni)
-Qias

Na hapo hakuna mbadala wa kutumia sheria nyengine zaidi ya hizo.

UAE chanzo chao kikubwa cha sheria zimetoka kwenye sheria za Kiislam. Hii sentensi unaielewa Bw. ndugu? Na ndiyo maana kuna option hata kwa masuala ya ndoa ikiwa mtu ni mkazi wa UAE lakini si raia wa pale ana uhuru wa kuchagua sheria za nchini kwake zimuhukumu. Nenda Saudi Arabia pendekeza hilo nafikiri watakupatia majawabu mazuri.

Ama kwa mfano mwengine: Ni kama sisi Tz vyanzo vyetu vya sheria tumetoa kwenye sheria za kiislam za kijadi n.k

Sijui umenielewa?

Nakushauri Bw. ndugu, tembelea hata google kuhusu mfumo wa sharia kwa UAE utaelewa kwa mapana.
Acha kuongopa..sheria za Tanzania zimetokana na common law..na customary laws.

#MaendeleoHayanaChama
 
Chanzo kikuu na uadui wa Waislamu na Wahindu nchini India ni Ukoloni wa Uingereza waliyokuwa wakiwatawala. Hao ndiyo walisababisha sumu ile waliyoipandikiza, iwe kichocheo cha uadui hadi leo hii. Walitumia sera yao ya DIVIDE AND RULE wakawagawanya kwa makundi kwa mujibu wa dini zao na sababu nyingine za kisiasa, waliwafanya wasiwe na umoja ili waendelee kuwatawala vyema.

Chuki kubwa ilizaliwa baada ya kuwagawa hivyo na ndiyo hiyo inayowatafuna hadi leo hii, ila kabla ya ujio wa mkoloni hakukuwa na uhasama baina yao.

=====

Huku Afrika hii sera yao imepelekea ukabila mkubwa sana baina ya watu wa nchi moja, wakoloni waliamua kuvunja umoja wa watu ili wasiweze kuungana dhidi yao kwenye utawala wao. Tanzania yenyewe tungeingia pabaya sana kwenye uhasama huu wa kikabila, kama isingekuwa kupigwa vita mapema.

Huko India walilenga imani zao maana ndiyo zilikuwa kila kitu, na huku wakalenga kabila kwani ndiyo zilibeba nguvu kubwa. Matokeo ya sumu yao ndiyo chuki ipo hadi leo hii
Utamlaumu mzungu lakini chanzo cha yote ni udini na chuki za Islam baada ya kushindwa na kukataliwa kuharibu tamaduni za wahindi..

Leo mzungu kaondoka kutawala huko miaka mingi kwanini wasirudi hali yao ya wali?

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuna uelewa mbaya juu ya kila wanao jilipua kuwa Ni waislamu kwasababu Tu Wana majina ya kiislamu au mavazi ya kiislamu....au inchi wanazo toka.

Lkn pia sio kila wanao jilipua wanapigana Vita ya kidini....kuna wengine wahuni ambao hata Dini hawaijui wanafuata matamanio Yao Tu.

Kwanza Uislamu unasema kuwa anayeua mtu mmoja basi ni Sawa Sawa na kama ameua watu wote na mwenye kuokoa Maisha ya mtu mmoja ni Sawa Sawa nakuokoa Maisha ya watu wote....kuna ambao Wanapaswa Kuuwawa Kwa haki...mfano kama umeua nafsi Kwa makusudi basi nawe itabidi uuwawe...kwani ktk kulipiza kisasi kuna kuwa na Uhai mzuri...Kwa maana watu wataogopa kuuwana ovyo.

Sasa waislamu Kwanza wanaruhusiwa kupigana Tu endapo maadui wameanza chokochoko dhidi ya waislamu...na kwahiyo watapigana kuondoa udhalimu na kusimamisha haki katika jamii na endapo hao madhalimu wakasilimu amri nakuacha basi waislamu nao wanatakiwa waache kupigana.

Vile vile katika hiyo Vita waislamu hawatakiwi kuwapiga makundi maalumu...kama wazee,wanawake na watoto isipokuwa wanaume mashababi ambao ndio hushika silaha....na kama haitoshi haitakiwi kuharibu mazao wala kuwapiga wanyama....sasa hapo ndo utaona tofauti ya wahuni ambao wanajificha nyuma ya Uislamu...wao wanavaa mabomu na kuua watoto,wakina mama nawazee na watu wasio na hatia...hao sio waislamu wanao ijua Dini Bali ni wahuni Tu.

Hiyo ndio Hali halisi linapokuna swala la Dini ya kiislamu
Wapi jamii ya kiislamu ilishawahi kupaza sauti kukemea hao wanaofanya vitendo hivyo..ama hayo makundi ya kigaidi?zaidi ya kukaa kimya kumaanisha wanaunga mkono yote hayo yanayotokea.

Mimi na mfano mdogo tu wa hapa hapa kwetu hata tusiende mbali..kwanini wakristo wa zenji wanakatariwa kumiliki ardhi..na kwanini miaka ya nyuma mapadri waliuliwa zenji na wengine kumwagiwa tindikali...kama kweli uslam ni dini ya upendo na amani kwa watu wote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Amna kitu kama icho Uislamu hauna chuki na dini nyingine yoyote ikiwa na wao wanaishi na nyinyi kwa upendo tuje kwenye kipindi cha uhai wa mtume s.a.w aliishi kwenye mji mmoja na watu wa dini nyingine wasiokuwa waislamu na wala akuwadhuru ..usome uislamu vizuri kiufupi wahindu ni wabaguzi kupita kiasi kwenye dini yao wenyewe mtu mweusi amelaaniwa yani ni wabaguzi grade A duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhusu ubaguzi hata waarabu kupitia dini yao hawachangamani na mweusi ndio mana leo hii ni ngumi sana mwarabu pure kuozesha mtoto wake kwa mweusi hata kama wawe imani moja...

Ubaguzi ni asili ya yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
..usome uislamu vizuri kiufupi wahindu ni wabaguzi kupita kiasi kwenye dini yao wenyewe mtu mweusi amelaaniwa yani ni wabaguzi grade A duniani

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtu mweusi anaiingiaje kwenye Uhindu? Nimesoma Bhagvad Gita hakuna mahali niliona imeongelea mtu mweusi kama ulimaanisha Mwafrika labda kama unachanganya na caste System ya India ambayo ina classes kuanzia Brahmas juu hadi wale wa chini kabisa untouchables, lkn untouchables siyo watu weusi kama sisi ni Wahindi wenzao, hivyo kama ni Ubaguzi ni wa Wahindi kwa Wahindi kutokana na hiyo caste system yao, lkn Uhindu hauna uhusiano wowote na mtu mweusi wa Afrika kama sisi!
 
Kulazilishwa siyo lazima kukatwa shingo tu hata Uislamu haukuenezwa kila mahali kwa kukatwa shingo labda nikuulize kwa nini Watanzania wana majina ya Kizungu kama George, Elisabeth au sijui Anna? Ilikuwaje ? Nini kilitokea kwani kabla ya Wazungu kuja hakukuwa na Anna wala Christopher sasa nini kilitokea?
Kule garrisa Kenya Yale magaid ya alshabab yalipovamia kile chuo na kuua wakristo na kuacha wavaa kobaaz wenzao walikua na maana gani? Kule Nigeria wale bokoharam wanaolazimisha uislam uko kwao Yani wanataka jamhuri yaa kiislam ..kwanini magaidi wengi wanautumia uislam na siyo ukristo kueneza arakati zao ..kwanini wengi Ni wavaa kobaaz na siyo watu wa kawaida. Kama munadai uislam Ni dini ya amani kwanini magaidi wanatafuta amani ama Sheria zao za kikumbavu kufuatwa. ..
 
Sasa Muhidu mwenye dini nyingi na miungu mingi wawe ndani ya jamii moja na Salafi unategemea nini? Chuki itakuwepo baina yao na uhasama mkubwa!
Upo sahihi kabisa, tena huko India kuna jamii za kihindu zenye misimamo mikali na mara nyingi hujaribu kuwalazimisha waislamu wawe wahindu kimabavu na makundi hayo huungwa mkono na baadhi ya wanasiasa ili wavune kura na wafuasi nyakati za uchaguzi.
 
Lkn ukiangalia tabia za waislam karibu dunia nzima zinafanana hapo uingereza anasingiziwa kwasababu ya mapungufu ya dini nyengine
Uwe unaongea unachokijua na uwe unaijua nature ya Uislamu ipo vipi. Vinginevyo kaa kimya na uache kuendeleza chuki zako kwenye udini, waislamu toka enzi wanaishi na wasiyo waislamu na hawajawahi kuwalazimisha kubadili dini au kuwaingilia imani zao. Hata Mtume Muhammad(S.A.W) mwenyewe kaishi na wayahudi na aliwaheshimu imani zao. Na yeye ndiye kila mwislamu anafuata mafunzo yake na taratibu zake alizoishi na wengine.

India kabla ya ujio wa Ukoloni hawakuwa na uhasama kati ya wahindu na waislamu, waliishi vizuri tu kwa amani. Mambo yamekuja kusababishwa na mkoloni, aliona umoja wao ungekuwa hatari kwake. Akawagawa ili atawale vizuri
 
Utamlaumu mzungu lakini chanzo cha yote ni udini na chuki za Islam baada ya kushindwa na kukataliwa kuharibu tamaduni za wahindi..

Leo mzungu kaondoka kutawala huko miaka mingi kwanini wasirudi hali yao ya wali?

#MaendeleoHayanaChama
Kabla ya ujio wa Mzungu hawakuwa na chuki wala udini, waliishi pamoja. Sera ya DIVIDE AND RULE ndiyo imeleta yote haya. Hii hata huku Afrika imeacha ukabila mwingi maana watu walitambuana kwa kabila, tofauti na huko walipojali dini.

Pia kule India ni watu ambao wanarithishana chuki kutoka kizazi hadi kizazi, suala hili ni gumu sana jambo kama hili kuisha. Kila mtoto akizaliwa alikuwa akipewa sumu dhidi ya adui wanayemchukia. Jambo hili limefanya hadi baadhi ya koo kule kwao kuishi hivyo hadi leo, hivyo usitegemee hilo suala la uhasama likaisha wakati linasambazwa kizazi kimoja hadi kingine

Pre-colonial period India haikuwa na uhasama wa kidini kati ya waislamu na wahindu, na hata watafiti wengi wamethibisha hilo
 
Hawa wahindi wa india ambao ni waamini wa dini ya kihindu wanawachukia sana waislam wanakwambia wangeweza wangewateketeza kwa bomu kama lile la USA kwenda Japan

Hii chuki inatokana na nini? Tukumbuke hawa wote ni wahindi jamii moja

Zamani kutokana na hii chuki kulipelekea waislam kujitenga na kuunda nchi yao ya Pakstan
Ila kuna waislam walibaki kwenye nchi yao ya asili ya India na kupelekea mgogoro hadi leo

Hawa wahindu wanaupendo wa dhati kwa wakristo na wabudha ila hawataki kuwasikia wahindi ambao ni waislam

Na ukichunguza kwa kina wahindi wengi waislam walikimbilia Africa na nchi nyingine kutokana na hizi chuki

Nchini India jamii za kiislam zinaishi kwa wasiwasi sana na ukibainika muislam anaona binti wa kihindi anaweza kufa kifo cha kutatanisha

Cha ajabu kule Pakstan jamii ya kihindi inachuki na ukristo kuliko wahindu

Sijawahi kushuhudia huu uhasama wa kidini nchi yeyote zaidi ya India
Kuna makala niliiona BBC wanasema chanzo cha chuki ni Mkoloni wao ambaye Mwingereza.

Mwingereza wakati anaitawala India, Wahindi wa kihindu walikuwa wanapewa upendelea mkubwa sana kwenye elimu na utawala na Wahindi waislam walikuwa wanachukuliwa kama daraja la china kabisa na watu wanaodharauliwa.

Na hii ilikuwa mbinu ya Mwingereza kuwatawala, kwa hiyo Ile kubaguana kumeendelea mpaka Leo na kesho.

Sawa na ilivyo hapo Rwanda.
 
Hawa watu wengi wao ni wastaarabu kwenye maandishi tu ila mioyo yao imejaa chuki huo ndio ukweli
Kule garrisa Kenya Yale magaid ya alshabab yalipovamia kile chuo na kuua wakristo na kuacha wavaa kobaaz wenzao walikua na maana gani? Kule Nigeria wale bokoharam wanaolazimisha uislam uko kwao Yani wanataka jamhuri yaa kiislam ..kwanini magaidi wengi wanautumia uislam na siyo ukristo kueneza arakati zao ..kwanini wengi Ni wavaa kobaaz na siyo watu wa kawaida. Kama munadai uislam Ni dini ya amani kwanini magaidi wanatafuta amani ama Sheria zao za kikumbavu kufuatwa. ..
 
Kila kona ya hii dunia Dini ya kiislamu ni shida. Inapigwa vita na wazungu , wachina na wahindi na shida ni ile ile waislamu wanataka kulazimisha dini yao ifuatwe kwa nguvu kitu ambacho akikubaliki kwa dunia ya saiv ambayo dini ni hiyari ya mtu.
uislamu haupo hivyo,dini zilibadilika baada ya kuingizwa biashara na siasa ndani yake...tafuta katika Quran suratul baqra aya ya 62 na nadhani suratul maida Aya ya 63 Mungu anaweka wazi yeye NI wadini zote sio uislamu TU....hapo itakufungua macho na kuona Quran inataka Nini na si waumini wa kiislamu wanataka nini
 
Lkn kiongozi wa dini ya kiislam huko iran aliagiza huyo mwandishi auwawe maiti ipelekwe iran
Watu walimfuata Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake juu ya kadhia fulani nayo ni: Wakamuuliza "mwanamke fulani anafunga kwa ajili ya Mungu, anakamilisha swala zote tano na anatumia sehemu yake ya usiku kufanya ibada. Lakini maisha yake ni mwenye kuwaudhi majirani zake". Mtume akajibu huyo ni mtu wa motoni!

Akaja kushitakiwa tena na watu ya kuwa mtu fulani anamtesa paka; Mtume akawajibu huyo ni mtu wa motoni.

Akamwambia kijana mmoja ambaye alikuwa anajiona yeye ni bora kuliko mwengine kuwa "dini yetu ni ya Mungu kuwa na heshima na viumbe vyake".

Maandiko kutoka kwenye hizo nukuu tatu unayaelewaje? Na unayafafanuaje?
 
Back
Top Bottom