Kwanini 'Wajinga' wanatoboa kimaisha haraka kuliko sisi 'Great Thinkers’?

Kwanini 'Wajinga' wanatoboa kimaisha haraka kuliko sisi 'Great Thinkers’?

Ujinga ni nini,? Kutokusoma mpaka level ya chuo huyu mtu tumuite mjinga.
Kuna watu wanatengeneza hela ambayo mwenye akili ni ngumu kuingia kichwa kichwa

Nitakupa mfano kuna hawa wanaochezesha mchezo wa vidaftari wanaingiza hela mule kuna wanaoweka

500,000 kwa siku
200,000 kwa siku
100,000 kwa siku
75,000 kwa siku
50,000 kwa siku
25,000 kwa siku
10,000 kwa siku
5,000 kwa siku

Hapo unachagua package yako unayoiweza mwisho wa mwaka unavunja unachukua hela yako

Nb: hii ipo hivi huyu unaempa yeye anaizungusha kwenye issues zake za mjini kutengeneza faida ila mwaka ukiisha anakukunjia hela yako yote uliyoiweka mwaka mzima unapewa

Mfano ana kibanda chake cha Mobile Money, kwa hio ukimpa 100,000 kila siku yeye anaizungusha humo kisha mwisho wa mwaka anafanya hesabu anakukunjia pesa yako yote ndani ya mwaka mzima

Sasa hio risk hapo ya kupoteza hizo pesa mjinga haioni anaweka hela win win situation ikifika mwaka anakunja kibunda kizuri tu, ila mwelevu huanza na maswali mengi sana kwamba hii nampa huyu bila maandishi yoyote je akilala mbele itakuaje? Mjinga hajiulizi mara 2 yeye anapeleka tu kwenda kuweka pesa unakuta kila siku anapeleka 100,000 sasa piga 100,000 × 365 inakuja ngapi?

Mjinga kila siku anaenda kuandika 100,000 kwenye kidaftari mwaka ukiisha ana 36,500,000/- cash anapewa

Hio 100,000 anayoipeleka kila siku inazungushwa kwenye miradi ya huyo anaempelekea ili apate faida ila mwaka ukiisha tu anampa jumla ya pesa zake zote alizoweka
 
Sio kweli mkuu, Mtaa unatuchapa wote tuu Wenye A kwenye vyeti, wenye C, Wenye 0 na wale ambao hawajasoma kabisa wote mtaa unatuchapa tuu.

Kiti kingine, Wasomi walishashtuka kitambo watu wanaanza kupiga harakati tangu wakiwa first year, side haso za kutosha na vitasa vya kutosha, shida ni kwamba mpaka utakapo make it ndo unakua recognized.

Nikitazama wanangu tulio maliza nao 0 level, Wale walio feli na kuingia kitaa moja kwa moja Wana maisha ya kawaida tu hakuna utofauti mkubwa na wale walio enda University, kila mtu anachapika kwa upande wake.

"The street is fair as is unfair to every one"
 
Mkuu unatakiwa kujua kuwa mtu akiwa na uwezo wa ku accumulate wealth huyo ndo ana akili kuliko wewe mwenye A's zako. Japo ungeachana na makaratasi ukaingia uraiani uhakika wa ku make ulikuwa mkubwa.

Yaani hizi elimu za darasani usipobahatisha kupata ajira kwenye sekta yenye marupurupu ndiyo ujue basi tena. Angalia kundi la walimu wamesoma kweli ila kiuchumi sasa duh utawahurumia.

wewe unazani hao walimu wasinge soma wangekua matajiri? Inamaana mtaani hakuna hopekess people ambao hawakwenda shule?

Elimu haimzuii mtu kutafuta hela, Kama umesoma na huna hela, You are just not husler au sio mjasiriamali.
 
Hao wanaoitwa wajinga si wajinga, ni watu wenye kujitambua Sana Tu....Ili utoboe lazima uwe "go getter",wasomi wengi waoga. Tena ingetakiwa msomi ndie ajitoe kimasomaso kwenye biashara maana exposure yake itamsaidia lakini waap, biashara nyingi za Kati wamiliki siyo wasomi wa darasani, we fikiria mtu Hadi anakaribia kustaafu hata finishing ya nyumba bado!, Hapa bado Tu wasomi hawaoni funzo lolote?, umeajiriwa mahali hata mkuu wako wa kitengo Tu ana Hali mbaya, we hustuki kama hapo sipo?...

Ni Bora uchelewe kupata lakini future yako Itakua Bora kuliko kuwa na uhakika wa Kila mwezi then future itakuwa ya hovyo.

mm nikiona sehemu immediate boss wangu anatembea kwa Mguu, Simalizi mwaka lazima nikimbie 😀

Sikai sehemu hakuna harufu ya pesa
 
Hao ni wachuuzi tu kuna mahali utajiri ukifika elimu inapaswa itumike , ndio maana kumi bora ya matajiri Tanzania kuwakuta wamatumbi vilaza ni ngumu sana🤔

Tajiri no.1 Duniani Yuko na Masters.
Tajiri no. 1 Tanzania Yuko na Degree

Elimu haimzuii mtu kufanikiwa, Ni jinsi unavocheza karata zako.
 
Sasa hapo kati ya anayetoboa maisha haraka alafu na wewe Sakala nani mjinga!!?

Mbona kama umeshajijibu tayari.
 
Kuna watu wanatengeneza hela ambayo mwenye akili ni ngumu kuingia kichwa kichwa

Nitakupa mfano kuna hawa wanaochezesha mchezo wa vidaftari wanaingiza hela mule kuna wanaoweka

500,000 kwa siku
200,000 kwa siku
100,000 kwa siku
75,000 kwa siku
50,000 kwa siku
25,000 kwa siku
10,000 kwa siku
5,000 kwa siku

Hapo unachagua package yako unayoiweza mwisho wa mwaka unavunja unachukua hela yako

Nb: hii ipo hivi huyu unaempa yeye anaizungusha kwenye issues zake za mjini kutengeneza faida ila mwaka ukiisha anakukunjia hela yako yote uliyoiweka mwaka mzima unapewa

Mfano ana kibanda chake cha Mobile Money, kwa hio ukimpa 100,000 kila siku yeye anaizungusha humo kisha mwisho wa mwaka anafanya hesabu anakukunjia pesa yako yote ndani ya mwaka mzima

Sasa hio risk hapo ya kupoteza hizo pesa mjinga haioni anaweka hela win win situation ikifika mwaka anakunja kibunda kizuri tu, ila mwelevu huanza na maswali mengi sana kwamba hii nampa huyu bila maandishi yoyote je akilala mbele itakuaje? Mjinga hajiulizi mara 2 yeye anapeleka tu kwenda kuweka pesa unakuta kila siku anapeleka 100,000 sasa piga 100,000 × 365 inakuja ngapi?

Mjinga kila siku anaenda kuandika 100,000 kwenye kidaftari mwaka ukiisha ana 36,500,000/- cash anapewa

Hio 100,000 anayoipeleka kila siku inazungushwa kwenye miradi ya huyo anaempelekea ili apate faida ila mwaka ukiisha tu anampa jumla ya pesa zake zote alizoweka
Bado sijakusoma mkuu
 
Mpaka akaweza kutengeneza hela huyo sio mjinga. Kuna maarifa na taarifa ameweza kuzielewa kwa ufasaha.

Labda kama wajinga uliomaanisha wewe ni wale ambao hawajasoma, walifeli darasani au wameamua kutafuta hela kwa njia ya kujizima data(mfano huyo mwijaku na baba levo). Hao wote sio wajinga.

Vilevile ukichukua wastani wa kipato cha hao ambao hawajasoma au walifeli shule(ambao wewe umemaanisha ni wajinga) ukikinganisha na kipato cha ambao wamesoma(kibongo bongo tuseme kuanzia ngazi ya diploma). Population ya ambao wamesoma ndio kuna kundi kubwa zaidi la watu wenye unafuu wa maisha.

Suala la kusema ambao hawajasoma ndio wanatoboa ni stereotype tu iliosababishwa na hawa ambao hawajasoma kuwa na show offs pamoja na kupendelea kuwaponda ambao wamesoma kila wanapopata nafasi. Musukuma ambae hajasoma utamwona anawaponda wasomi lakini hata siku moja hauwezi kumwona Benjamini fernandez anawaponda ambao hawajasoma
hmmm
 
Leo naomba tuweke vyeti vyetu vya chuo na zile "A" zetu za sekondari pembeni, tuzungumze ukweli unaouma. Nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi na kugundua jambo moja la kushangaza sana mitaani:

Asilimia kubwa ya watu tunaowachukulia kama 'watu wa kawaida' au wasio na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, wanapiga hatua kubwa sana za kifedha kuliko sisi ambao vichwa vyetu vimejaa "critical thinking".

Hapa nimejaribu kuchambua kwanini hawa jamaa wanatuacha kwenye mataa, huku sisi tukiendelea kubishana kuhusu sera za uchumi na siasa za kimataifa:

  • Ugonjwa wa 'Analysis Paralysis': Msomi akitaka kufungua genge la nyanya, atafanya SWOT Analysis, atachora Business Plan ya kurasa 40, ataangalia Market Volatility, na kusoma vitabu vya Robert Kiyosaki. Mwisho wa siku, anaona mradi una hatari (Risk) asilimia 60%, anaacha. Yule 'mjinga' asiyejua SWOT analysis, anaamka asubuhi, ananunua nyanya, anapanga kwenye fungu, anauza. Baada ya miaka miwili, msomi bado anasoma Rich Dad Poor Dad, yule jamaa anamiliki maduka matatu.
  • Utumwa wa 'Brand' na Hadhi: Sisi watu wenye akili tuna shida moja—tunaogopa kuonekana wa kawaida. Mtu mwenye digrii yake anaona aibu kuuza mitumba kariakoo kwa sababu "haishabihiani na hadhi yake". Yuko tayari kukaa ofisini na kiyoyozi, akilipwa laki tano kwa mwezi na bosi ambaye aliishia kidato cha pili, lakini bosi huyo ndiye anayemiliki ghorofa anayopanga huyo msomi. Sisi tunalinda Brand isiyolipa, wao wanasaka pesa.
  • Kizungu Kingi, Salio Dogo: Kwenye mitandao na majukwaa kama haya, tunajua sana kupanga hoja. Tukianza kuchambua Macro-economics au makosa ya serikali, unaweza kudhani sisi ni washauri wa Benki ya Dunia. Lakini ukiingia kwenye Mobile Banking zetu, salio linasoma elfu kumi na mbili. Wakati sisi tunabishana kwa Kiingereza kinyoofu, kuna 'machinga' yupo busy anapokea oda za maelfu ya dola kutoka China kwa kutumia "Google Translate". Pesa haitambui Grammar, inatambua mzunguko.
  • Hatari ya 'Perfectionism' (Kutaka Kukamilika Kila Kitu): Sisi "Great Thinkers" tunataka kila kitu kikae kwenye mstari kabla ya kuanza. Tunataka mtaji kamili, ofisi nzuri, na mazingira rafiki. Watu wa mtaani wana falsafa ya kikatili: "Tuanze, tutarekebisha mbele ya safari." Na mara nyingi, mitaani ndiyo shule halisi. Wanakosea, wanajifunza, wanapata hela. Sisi tunasubiri wakati sahihi ambao haufiki kamwe.
Hitimisho:Sijasema tusome au tusiwe watu wa kufikiri. Lakini huu uzito wetu wa kiakili (Critical Thinking) mara nyingi unageuka kuwa gereza letu la hofu. Tunajua sana hatari za kushindwa kiasi kwamba tunaogopa hata kujaribu.

Je, wakuu mnakubaliana na hili? Au ni mimi tu nimeamka na mawazo ya kifukara leo? Tiririkeni.

View attachment 3562994
Siku ukijua akili ninini ndio utajua huko kichwani umejazwa upuuz mtupu. Wewe unaprogramiwa kuwa mtumwa then unajiita mwenye akili. Asilimia 90 ya bilionea dunian walidrop chuo kuja kukimbiza na ndoto zao. Wewe endelea kujidanganya na vyeti vya A. Mzee ukishafikisha miaka 45 kwenda juu watu hawataki kujua una PHD ngap wanataka kuona matokeo.
 
Mkuu unatakiwa kujua kuwa mtu akiwa na uwezo wa ku accumulate wealth huyo ndo ana akili kuliko wewe mwenye A's zako. Japo ungeachana na makaratasi ukaingia uraiani uhakika wa ku make ulikuwa mkubwa.

Yaani hizi elimu za darasani usipobahatisha kupata ajira kwenye sekta yenye marupurupu ndiyo ujue basi tena. Angalia kundi la walimu wamesoma kweli ila kiuchumi sasa duh utawahurumia.
Hivi mbona kila mfano duni ni mwalimu
 
Elimu ni muhimu sana katika utafutaji pesa hasa elimu ya juu shida muda wa kuitafuta hiyo elimu ili uje uitumie katika haso zako ndio mwingi Sana at least iwe seven years ushapata degree yako unajipambania kivingine
 
huezi kua mjinga ukafanikiwa, In reference ya baba levo na mwijaku, hawa ni watu wa SHOW BIZ, ndo sector yao, however kuna kitu cha ndan sana unatakiwa kukielewa, People who nenver went to school ama walio wajinga(as yuo claim) story zao zinafurahisha kuskia, ila katika 2 waliofanikiwa basi kuna million wengine hawakufanikiwa, the only difference is they dont make it to the main stream because nothing will sell on that story than hao waliokua wajinga alafu wakatoka, chance za wewe kutoka without formal education ni ndogo sana, almost zero! However chances za kutoka ukiwa na education is much higher, thats why kuna watu wengi wameajiriwa
Hapo ndipo flaw ya analysis yake ilipo. The focus is on the successful few, ignoring the millions of illiterate folks who continue to languish in abject poverty!
 
Kama "mjinga" unamaanisha mtu asiye na elimu basi huo utafiti wako kaurudie. Watu walioishia darasa la 7 au ambao hawakumaliza hata la 7 wengi wao choka mbaya sana. Ni mmoja kati ya laki 1 ndo unakuta ni tajiri. Hao jamaa ndo wateja wakubwa wa mataputapu na gongo. Kimsingi wengi wamechoka hatari. Hawa wachache ambao ni matajiri ndo wanafanya wasomi wakose kujiamini.
 
Back
Top Bottom