Kwanini 'Wajinga' wanatoboa kimaisha haraka kuliko sisi 'Great Thinkers’?

Ujinga ni nini,? Kutokusoma mpaka level ya chuo huyu mtu tumuite mjinga.
Kuna watu wanatengeneza hela ambayo mwenye akili ni ngumu kuingia kichwa kichwa

Nitakupa mfano kuna hawa wanaochezesha mchezo wa vidaftari wanaingiza hela mule kuna wanaoweka

500,000 kwa siku
200,000 kwa siku
100,000 kwa siku
75,000 kwa siku
50,000 kwa siku
25,000 kwa siku
10,000 kwa siku
5,000 kwa siku

Hapo unachagua package yako unayoiweza mwisho wa mwaka unavunja unachukua hela yako

Nb: hii ipo hivi huyu unaempa yeye anaizungusha kwenye issues zake za mjini kutengeneza faida ila mwaka ukiisha anakukunjia hela yako yote uliyoiweka mwaka mzima unapewa

Mfano ana kibanda chake cha Mobile Money, kwa hio ukimpa 100,000 kila siku yeye anaizungusha humo kisha mwisho wa mwaka anafanya hesabu anakukunjia pesa yako yote ndani ya mwaka mzima

Sasa hio risk hapo ya kupoteza hizo pesa mjinga haioni anaweka hela win win situation ikifika mwaka anakunja kibunda kizuri tu, ila mwelevu huanza na maswali mengi sana kwamba hii nampa huyu bila maandishi yoyote je akilala mbele itakuaje? Mjinga hajiulizi mara 2 yeye anapeleka tu kwenda kuweka pesa unakuta kila siku anapeleka 100,000 sasa piga 100,000 × 365 inakuja ngapi?

Mjinga kila siku anaenda kuandika 100,000 kwenye kidaftari mwaka ukiisha ana 36,500,000/- cash anapewa

Hio 100,000 anayoipeleka kila siku inazungushwa kwenye miradi ya huyo anaempelekea ili apate faida ila mwaka ukiisha tu anampa jumla ya pesa zake zote alizoweka
 
Sio kweli mkuu, Mtaa unatuchapa wote tuu Wenye A kwenye vyeti, wenye C, Wenye 0 na wale ambao hawajasoma kabisa wote mtaa unatuchapa tuu.

Kiti kingine, Wasomi walishashtuka kitambo watu wanaanza kupiga harakati tangu wakiwa first year, side haso za kutosha na vitasa vya kutosha, shida ni kwamba mpaka utakapo make it ndo unakua recognized.

Nikitazama wanangu tulio maliza nao 0 level, Wale walio feli na kuingia kitaa moja kwa moja Wana maisha ya kawaida tu hakuna utofauti mkubwa na wale walio enda University, kila mtu anachapika kwa upande wake.

"The street is fair as is unfair to every one"
 

wewe unazani hao walimu wasinge soma wangekua matajiri? Inamaana mtaani hakuna hopekess people ambao hawakwenda shule?

Elimu haimzuii mtu kutafuta hela, Kama umesoma na huna hela, You are just not husler au sio mjasiriamali.
 

mm nikiona sehemu immediate boss wangu anatembea kwa Mguu, Simalizi mwaka lazima nikimbie 😀

Sikai sehemu hakuna harufu ya pesa
 
Hao ni wachuuzi tu kuna mahali utajiri ukifika elimu inapaswa itumike , ndio maana kumi bora ya matajiri Tanzania kuwakuta wamatumbi vilaza ni ngumu sana🤔

Tajiri no.1 Duniani Yuko na Masters.
Tajiri no. 1 Tanzania Yuko na Degree

Elimu haimzuii mtu kufanikiwa, Ni jinsi unavocheza karata zako.
 
Sasa hapo kati ya anayetoboa maisha haraka alafu na wewe Sakala nani mjinga!!?

Mbona kama umeshajijibu tayari.
 
Bado sijakusoma mkuu
 
hmmm
 
Siku ukijua akili ninini ndio utajua huko kichwani umejazwa upuuz mtupu. Wewe unaprogramiwa kuwa mtumwa then unajiita mwenye akili. Asilimia 90 ya bilionea dunian walidrop chuo kuja kukimbiza na ndoto zao. Wewe endelea kujidanganya na vyeti vya A. Mzee ukishafikisha miaka 45 kwenda juu watu hawataki kujua una PHD ngap wanataka kuona matokeo.
 
Hivi mbona kila mfano duni ni mwalimu
 
Elimu ni muhimu sana katika utafutaji pesa hasa elimu ya juu shida muda wa kuitafuta hiyo elimu ili uje uitumie katika haso zako ndio mwingi Sana at least iwe seven years ushapata degree yako unajipambania kivingine
 
Hapo ndipo flaw ya analysis yake ilipo. The focus is on the successful few, ignoring the millions of illiterate folks who continue to languish in abject poverty!
 
Kama "mjinga" unamaanisha mtu asiye na elimu basi huo utafiti wako kaurudie. Watu walioishia darasa la 7 au ambao hawakumaliza hata la 7 wengi wao choka mbaya sana. Ni mmoja kati ya laki 1 ndo unakuta ni tajiri. Hao jamaa ndo wateja wakubwa wa mataputapu na gongo. Kimsingi wengi wamechoka hatari. Hawa wachache ambao ni matajiri ndo wanafanya wasomi wakose kujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…