Imenilazimu nipitie comment zote mpaka mwisho ili niijue dhamira ya dhati ya mwanzisha uzi.
Baada ya kuona ni hoja za kitoto na hata akipewa hoja za msingi anazipiga teke ilimladi anogeshe uzi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nikaamua kutupa kuleeeeeee.
Ila kiukweli nimevuti saana na mdau hapo
DeWitt J ambae ameongea kitakwimu saana...sisi waislamu tunasema MAASHALLAH umeongea vizuri.
Binafsi kuna siku nilikuwa napitia takwimu za wafuasi wa dini (kuna presentation nilikuwa naandaa) baada ya kupekenyua maeneo mbali mbali nikaona wwbsite flan hv ikinionesha waislam tanzania wapo asilimia 29.8%. Nikashtuka na kuamua kufatilia physically na kuwauliza baadhi ya watu wafuatiliaji wa mambo na wenye kupenda sana kudai usawi wa kifursa baina ya dini hizi mbili zinazokaribiana.
Wengi wao waliniambia kuwa waislamu tupo asilimia 65% nilipouliza hii data umeitoa wapi!!? Wengi hawakuweza kunijibu, ila sikukata tamaa nikaendelea kichimba mtandaoni nikagundua takwimu ambazo mashekhe wengi wanazitoa ni zile za sensa ya mwaka 1957.
Nikaona hapa kuna haja kuwaokoa na aibu masheikh wangu ili siku na siku wakiulizwa wawe na takwimu...nikafatilia mtaoni zaidi nikapata tawimu za aina tatu zinazo karibia 29.8% , 30% , 32-35%..nikasema wacha na mie niingie kwenye utafiti.
april 2018 nikaingia kwenye utafiti rasmi. Nikaanda sample zangu 9 mpaka sasa nishamaliza sample 6 kuzipitia mpaka sasa nmeibuka na matokeo kuwa waislamu tanzania tupo 29 - 32% labda sijajua hizo sample 3 zilizobaki zitanipa majibu gani.
Yaani kwa sasa nikiwaambiaga waislamu tupo asilimia hzo wananiona kama nimekengeuka. Na uzuri utafiti huu ipo kiwilaya na kimkoa..kwahyo ukisema mkoa fulani una waislamu asiliamia ngap nakuambia nikiwa na uhakika wa hali ya juu.
Mfano jamaa
DeWitt J Amezungumzia kuhusu kigoma. Kigoma waislami wapo wilaya ya kigoma mjini pekee ambapo ni 56% pekee ila ukienda huko kasulu, kibondo, manyovu ni asilimia 13% , 9.2% , 6% mtawaliwa.
Na nitamdaa jarida na nitawapatia bakwata na taasisi zote kubwa za kiislamu na sababu za kushuka kwa kwa hizo asilimia kutoka 65% mpaka ~32%
Na kuhusu ukweli wa hiyo 65% ya mwaka 1957 nipo katika kufuatilia ila nimepata kuambuwa nawenzangu jamaa yangu (mkristo) kuwa nyuma ya hapo waislamu walikuwa 75% kulingana na takwimu za kanisa katoliki. Nitafatilia.