Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Wasalaam Ndugu wanaJF
Mwaka 1517 Padre machachari wa kanisa katoliki Martin Luther aliamua kujitenga rasmi na kanisa Katoliki, Claim ya Luther ilikuwa kanisa kwenda kinyume na maandiko, pia kanisa kujihusisha na mauzo ya rehema!
Kwa Mujibu huo Luther aliwekwa katika kikundi cha watu wanaoitwa Heretics yaani wanaopotosha na kupinga mafundisho ya Kanisa.. kwa kitendo hicho akatengwa na kanisa yaani "Excomunicated"
Luther alikuja kuanzisha kitu kinaitwa "Uprotestanti" yaani kupinga mafundisho ya kanisa katoliki.. kitu kilichozaa kanisa la Kilutheri!,
Muktadha wa mada yangu ni ushirikiano thabiti uliopo sasa baina ya kanisa katoliki na Lutheran, Je imekuwaje wanashirikiana tena kwa upendo kiasi hiki? Wakatoliki hawawachukulii Lutherans kama Heretics tena?
Mfano leo nilikuwa kwenye Misa ya Pamoja pale Parokia ya chuo kikuu DSM, Monsignori Mbiku na Mchungaji wa KKKT waliendesha ibada kwa Pamoja, na pia hiyo nyumba ya ibada wanaitumia wote na wameandaa litrujia ya pamoja..
Ukiachana na hilo wakatoliki hawambatizi upya Mlutheri, wanachofanya ni kubariki tu ubatizo wake ila wasabato na wengine baadhi wakihamia Katoliki lazima wabatizwe upya..
Je nini chanzo cha kurudi kwa ushirikiano baina ya haya makanisa Mawili?
Divine!