Kaka, nchi yetu sasa ina umri wa miaka zaidi ya 50 tangu tupate uhuru, hivi unataka kusema tumekua tukitumia nini kuwasiliana. Leo hii tunaongoza ukanda huu wote kiuchumi, kielimu na kila kitu.
Ifahamike kwamba sisi tunajivunia uwezo wa kuongea lugha nyingi, kwanza tunaenzi lugha zetu za asili, halafu Kiswahili ambacho kilibuniwa kwenye Pwani zetu kwa ushirikiano wa Mwarabu na Waafrika, tunaongea Kingereza na kuna baadhi yetu wanatumia lugha zingine za kigeni.
Nyie hapo mumekomaa na lugha moja ya Kiswahili, halafu uandishi wenu wa Kiswahili hutia kichefuchefu, hebu pitia alichoandika mleta mada ambaye amejikita kwenye kukosoa Wakenya, ameandika sentensi chache lakini zimejaa majanga kwenye uandishi. Tatizo mnafikiria Kiswahili mnachoongea kitaa ndio fasaha, na mara nyingi ndio mnaandika huku JF, watu wa buku jeru.
Tatizo ujamaa uliwafundisha nyie kuishi maisha ya kufungiwa kwenye mfumo mmoja bila kuthubutu mapya, kawaida yenu hutiririka kwenye kitu kimoja bila yeyote kujitolea na kuthubutu chochote kipya. Mumekomaa kwenye lugha moja (ambayo uandishi wenu wa ovyo), halafu stakabadhi zenu muhimu zote zimeandikwa kwa Kingereza, na ndio maana huwa mnaibiwa kwenye hilo shamba la bibi, mna kila kitu, madini, ardhi kubwa yenye rotuba, vivutio bora vya utalii n.k. lakini leo hii bado mnatajwa kwenye nchi maskini wa kutupwa Afrika.
Naskia leo hii ndio mnashtuka eti mumekua mkiibiwa kwenye mchanga wa dhahabu....hehehehe!!