kilam
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 2,092
- 2,128
Mada kama hizi za kutaja makabila huwa kama asali kwako, chunga usije kuachia ukabila ukakumaliza.
Mimi najivunia Ukikuyu maana ndio asili yangu, sikuzaliwa Mkikuyu kwa bahati mbaya, ndiko walikozikwa mababu zangu, na kila nikienda kuwasabahi watu wetu kule huwa natiririka Kikikuyu hadi raha.
Lakini pia hata hapa mjini huwa natumia lugha yangu ya asili sehemu stahiki, ukizingatia pia nimejifunza lugha kadhaa za huku kwetu.
Kila mmoja wetu dunia hii ana asili yake, hata ukizamia kwa Wazaramo Dar na kujifanya Mswahili, ukweli ni kwamba hutafuta asili ya ulikotoka, kwa njia moja au nyingine kuna kitu ndani yako kimeunganika na mababu zako. Watanzania mnaishi vibaya sana kwa kukana na kutelekeza asili zenu.
Hata hivyo, Mzungu alikuja akachora chora mipaka na kuwakusanya watu wa asili mbali mbali na kuwasindika kwenye makundi, kila kikundi akakipa taifa, na kuwaamrisha Waafrika waanze kuonana kwa misingi ya hayo makundi, hivyo mababu zangu wakajipata ndani ya kikundi cha Kenya, nimezaliwa na kuikuta hali ikiwa hivyo, nikaikumbatia na kujivunia Ukenya japo bila kusahau asili yangu ya Ukikuyu.
Zaidi ya hapo, nasheherekea Uafrika unaotuleta pamoja kwenye bara hili licha ya kutenganishwa na michoro ya mkoloni, hamna kitu huniuma kama ninapotembelea mojawapo wa haya mataifa halafu uhamiaji wananihoji siku ninazokusudia kukaa humo. Yaani mtaani unapishana na watu mnaofanana katika kila hali, mnaotaniana kama ndugu, ila siku zako zinajihesabu na zikiisha lazima uondoke.
Ndio yale ya Afrika Kusini, Waafrika weusi wanatembezana mapanga kwa misingi ya hiyo michoro iliyowekwa na mzungu.
Ndiyo nakwambia sasa, ungependa Ukikuyu wako usingeoa Mluhya. Umekasirisha mizimu yako ndiyo maana kila siku kazi yako kubwa humu ni kuchafua hali ya hewa.