Kwanini Wakenya siyo wajanja kwenye hili?


Ndiyo nakwambia sasa, ungependa Ukikuyu wako usingeoa Mluhya. Umekasirisha mizimu yako ndiyo maana kila siku kazi yako kubwa humu ni kuchafua hali ya hewa.
 
Ndiyo nakwambia sasa, ungependa Ukikuyu wako usingeoa Mluhya. Umekasirisha mizimu yako ndiyo maana kila siku kazi yako kubwa humu ni kuchafua hali ya hewa.

Nilioa binadamu sio kabila.
 
Ina uhusiano gani na Mada husika? Isitoshe mimi siyo Msukuma, asili yangu ni Rufiji kama ulipenda kujua.
Mi sijakuuliza km wewe kabila gani..
Lkn ukwel utabaki kuwa pale pale, muacha mila ni mtumwa
 
Huyo jamaa ameuliza swali la msingi sana, kwa kujua idadi ya watu katika kila kabila, hiyo data inasaidiaje katika mipango ya serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi?. Hivi mipango ya serikali ya kuendeleza nchi inategemeaje idadi ya watu katika kila kabila?.

Hivi Kenya hadi Leo pamoja na madhara makubwa yanayosababishwa na ukabila, hamjajifunza kutoka Tanzania katika hili?. Tulitegemea kadri miaka inavyokwenda mtajaribu kujifunza kutoka Rwanda ambako sasa hivi hawaruhusu kuuliza kabila la mtu, wote wanajiita " wanyarwanda.

Ninyi wakenya ni wabaguzi sana, na kigezo kikubwa mnachokitumia ni ubaguzi. Tanzania tunayo makabila Mengi zaidi yenu, lakini hatuyatumii kubaguana na kupigana kama ninyi, dunia nzima inasifia Tanzania kwa utulivu na umoja pamoja na kwamba tupo na makabila Mengi, hata ninyi wakenya mnatamani sana namna tunavyoishi.
 
Mwalium Nyerere RIP, alisema "Unataka kujua kabila la mtu ili iweje? Unataka kuandaa matambiko? Kama ni idadi ya wakristu au waislamu basi watajihesabu wenyewe huko makanisani na misikitini".
Mbona ukienda polisi lazima utaje kabila? Kuna watoto bibi ni mnyakyusa, babu mchaga, baba mhaya na mama ni mnyaturu sasa huyu ni kabila gani? Ifike mahali polisi iache kudhalilisha watu na makabila sababu watu hawajui hata makabila yao kwa sasa.
 
Acha kukwepa maswali, nani kakuambia hatuulizi makabila?, unaulizwa katika sensa ambako serikali inauliza hilo swali, lengo ni nini?, jeshi la POLISI linauliza hilo swali kwa ajili ya kuweza kupata utambulisho wa MTU katika mambo ya usalama, ila sio lazima kujata kabila kwasababu kuna watanzania wengi, hasa kutoka Zanzibar ambao hawana makabila, sasa ktk sensa ya nchi, kuuliza kabila la MTU kuna maana gani?
 
Mbona ukienda polisi lazima utaje kabila? Kuna watoto bibi ni mnyakyusa, babu mchaga, baba mhaya na mama ni mnyaturu sasa huyu ni kabila gani? Ifike mahali polisi iache kudhalilisha watu na makabila sababu watu hawajui hata makabila yao kwa sasa.
Nani amekuambia ni lazima, hilo swali hulaximishwi, hata Hospitali huwa wanauliza, lakini sio lazima, unaweza kusema huna kabila wala dini, na hakuna POLISI wala daktari atakayekulazimisha. Kumbuka kwamba wazanzibari hawana makabila. Mimi huwa nikienda sehemu zote hizo sitaji kabila langu, Mara kwa Mara nikienda kituo cha POLISI ninawauliza kwanini bado mnauliza kabila la MTU, huwa hawanijibu, wanacheka tu.
 
afadhali ya Kenya kuliko ukabila wa ccm . ccm wanaangamiza utaifa wetu.
 
 
Kinachoudhi ni pale wanapokuwa wanatangaza eti wamemkamata jambazi, the next sentence ni kabila lake. They have to stop. Wananikumbusha wamarekani walivyo bado na culture ya Ethinic eti black, white, hispanic or whatever. I hate that.
 
Kinachoudhi ni pale wanapokuwa wanatangaza eti wamemkamata jambazi, the next sentence ni kabila lake. They have to stop. Wananikumbusha wamarekani walivyo bado na culture ya Ethinic eti black, white, hispanic or whatever. I hate that.
Ni kweli, hilo swali pamoja na kwamba katika taarifa za POLISI linaonekana ni muhimu, kwasababu kama muhalifu jina lake ni " John Patrick " ukitaja kabila lake, linaweza kusaidia kutofautisha kati ya "John Patrick" ambaye ni Mngoni, na Muhehe, kwasababu huwa majina yanafanana, hivyo kabila linaweza kusaidia kuwatofautisha.

Kwa upande wa Tanzania, hata tukitaja kabila la mtu, madhara sio makubwa, kwasababu hatuna tabia ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, lakini kwa Kenya, hili jambo linamadhara makubwa sana, hivyo si busara kwa wakenya, waganda, Burundi au Rwanda, kujilinganisha na Tanzania.
 

Kutokana na hii fomu kuuliza kabila ni sehemu muhimu ili kufanikisha hilo dodoso katika taratibu za uhamiaji. N.B Uhamiaji mfano huwezi kua na jina Mwakipesile kisha ukasema ni mwenyeji wa Tanga lazima kutakua kuna walakini katika maelezo yako. Vilevile ukiangalia hiyo fomu haijaishia kwako tu imefika kwa baba, mama, bibi hadi babu ili kupata taarifa sahihi kuhusu wewe. Lengo si kujua kabila lengo ni kujua uraia wako.
 
Kuhesabu kikabila au kusema kabila lako unapoingia gesti..gani ya kiboya
Tofautisha kati ya nchi kutangaza kila kabila kwa idadi yao na kujaza taarifa binafsi kwenye fomu huko guest House na maeneo mengine ambayo hayana uhusiano na kuhesabu watu

Tanzania haipingi watu kuwa na makabila yao au kujivunia kabila lako ndio maana tunayo tamasha maarufu linaitwa URITHI FESTIVAL linakutanisha makabila yote huku kukiwa na ngoma, vyakula, mavazi, mila na desturi za kila kabila nchini na tamasha hilo linaendesha na serikali,

Tanzania haitaki kuendekeza ukabila mpaka kwenye kuhesabu idadi kwamba kabila a wapo kadhaa kabila b wapo kadhaa (unafanya hivyo ili iweje? Kwani kuna huduma yoyote serikali inatoa kikabila kwamba lazima wajue idadi ya wanufaika?)
 
Bado hukujibu swali la msingi. Kutokana na mantiki ya sensa, nini umuhimu wa kujua idadi ya watu katika kabila?
 

Nitakuuliza kama wanavyouliza wenzako, kabila unataka kujua la nini, ukatambike, mbona usifute kabila kwenye dodoso uhoji mengine.
 
Bado hukujibu swali la msingi. Kutokana na mantiki ya sensa, nini umuhimu wa kujua idadi ya watu katika kabila?

Nimejibu ila sio lazima nijibu kwa kutumia maneno mnayolazimishia, ukiwa na nia utaelewa, fahamu kwamba dodoso la sensa huandaliwa kisayansi, lengo na madhumuni ya kila swali humo huwa kwa ajili ya takwimu zinazosaidia kisayansi. Kuna tasnia mbali mbali ambazo hutumia kanzidata ya sensa kwenye maboresho ya kijamii.
 
hii post mbona umeandika kama umepaniki sana?.
 
Huna jibu la Kisayansi kuhusu hilo na muktadha wa sensa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…