Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Ukiangalia Tanganyika ni nchi ilioathirika sana na utawala wa Uingereza na hasa katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la Sahara.
1.Kenya na Zanzibar kabla ya kukabidhiwa serikali na uingereza, mtawala huyo alihakikisha anaweka mipaka ya nchi hizi kwa kuzinufaisha! Kenya ambayo awali ilikuwa haina bahari iaipatiwa Mombasa tena kwa gharama.
Zanzibar, kwa upande wake, ilithibitishiwa kimaandishi eneo lake lote inalolimiliki na kuinyima Tanganyika hata umiliki wa fukwe na bahari kuanzia Mombasa mpaka Ras Kanzi, kiasi cha kilomita 120 urefu na upana kilomita 40 na hivyo kuifanya Tanganyika kuwa ni nchi kasoro bahari. Sehemu pekee ya Tanganyika kuwa na bahari ni kuanzia Ras Kanzi kwenda kusini
2.Malawi ambayo pia ilitawaliwa na Uingereza, wao walipewa eneo lote la ziwa mpaka kwenye fukwe za eneo lote la Tanganyika. Lakini ilipokuja mpaka wa Msumbiji na Malawi,Ziwa Malawi liligawiwa nusu kwa nusu. Msumbiji ilikuwa inatawaliwa na wareno.
3.Tanganyika sasa inalazimika kuwa na uchu wa kudaka kila kitu mbele ya macho yao iwe kwa hadaa au kujaribu kujenga hoja bila mafanikio.
4. Uingereza pia ilihusika kunyofolewa kwa Ruanda Urundi kutoka Tanganyika wakati awali ikiwa chini ya mtawala mmoja Ujerumani.
Hivi Tanganyika ilkosa nini kwa Uingereza kustahili kufanyiwa yote haya?Kitu pekee Uingereza ilioifanyia Tanganyika na cha kukumbukwa ni "kuigaia" Mlima Kilimnjaro kutoka nchi ya Kenya.