Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
- Thread starter
- #21
Ahsante kwa mchango lakini Tanganyika haikuwahi kuwa Protectorate hata siku moja kwa vile hakukuwa na uongozi wenye kuheshimika kama vile Zanzibar, Malawi na Uganda. Nchi hizi ndio zilikuwa ni Protectorate. Tanganyika ilikuwa ni Territory (1916-1961)Baada ya Ujerumani kushindwa kwenye vita vya kwanza vya dunia, ilinyang'anywa makoloni yake na League of Nations.
Uingereza walipewa Tanganyika kuilea (Protectorate) na sio koloni. Rwanda na Burundi walipewa Ubelgiji. Kwa hiyo Uingereza walikuwa walezi tu na ndio maana hawakujali kuiendeleza. In fact, Uingereza ilikuwa ikichukua mapato yatokayo Tanganyika (mkonge, chai, kahawa, madini, n.k.) na kuwekeza kwenye koloni lake la Kenya.
Hata hivyo napata shida sana kutafautisha baina ya Colony na Territory na kwangu naona kama ni sawa tu kwa vile msimamizi anakuwa ima mtu au Taifa.
Naweka hapa maana ya maneno haya mawili kwa lugha ya kiingereza kuhofia kupunguza au kuongeza maana.
“a colony is a territory under the immediate political control of a state” while “a territory is a defined area, including land and waters, considered to be a possession of a person, organization or nation state"