Kwanini wakoloni wameamua kutembelea makoloni yao kwa mpigo

Kwanini wakoloni wameamua kutembelea makoloni yao kwa mpigo

Mkuu kwani waliondoka lini? Nauliza hivyo kwa sababu!

1. Lugha rasmi tunayo tumia kwenye mawasiliano muhimu ya ndani na kimataifa ni Kwao.

2. Mfumo wa uendeshaji serikali, Bunge na mahakama tunaotumia ni wa kwako

3. Tunaabudu kwa kutumia dini na vitabu vyao vya imani.

4. Tunakopa kwao

5. Mfumo wa elimu ni wa kwao.

6. Mfumo wa uchumi tunaotumia ni wa kwao.

5. Fedha tunazotumia kuagiza vitu mbali mbali kimataifa ni ya kwao

7. Mfumo wa siasa wa kidemokrasia ni wa kwao.

8. Teknolojia ya viwanda, usafirishaji, afya na habari ni ya kwao.

9. Silaha, taratibu na mifumo ya usalama na ulinzi ni wataifa ni ya kwao

10. Starehe, sanaa na muziki tunaomba na kuburudisha ni ya kwao.

Mkuu hapo unasemaje wa narudi wakati hawakuondoka?
hapo sawa, waliacha tujitawale wenyewe kwa mifumo yao, ni kweli mifumo ni ya kwao na wanafurahia kuwa walishinda ushindi wa muda mrefu. Nchi zetu bado zipo chini ya wakoloni wake.
 
Wamekuja kuomba tag ya vita vya 3 automatic kama wewe ni muelewa wa mambo ya ndani utanielewa
 
Wameona Waarabu wameweza.
Na wao wanaona wataweza.

Kwanini na wao wasiweze?
 
Juzi kati Mfalme wa Uingereza katua pale Kibera, nchini Kenya. Hatujakaa sawa Rais wa Ujerumani katia nanga hapa Tanzania.

Wote kwanza wakaomba msamaha na radhi juu ya unyama waliotenda Babu zao katika ardhi hizi mbili, kuua na kuwafanya watumwa Majimaji warriors kwa Ujerumani hapa Tanzania na Maumau warriors kwa upande wa uingereza pale Kenya.

Ni kama hawa Wakulungwa walikuwa na mission yao, maana ngozi nyeupe iko mbele ya muda sana kuzidi ngozi nyeusi. Unaweza kudhani ni Presidential visit ya kawaida tu, kumbe ni patrol ya wazee wa kazi.
Mtalaka hatongozwi.. 😂😂
 
Tulipewa Uhuru wa bendera tu huo ndiyo ukweli ukitaka kujua hilo angalia vita isiyo koma drc, angalia kifo cha Gaddafi,angalia kupinduliwa kwa Mugabe,angalia kulundikwa kwa maraisi wa Afrika kwenye daladala UK kwenye mazishi ya malkia wa uingereza,angalia wanaojaribu kupinga ushoga Afrika wanavyo shughulikiwa,angalia Tanzania kipindi cha Magu direction yake ingekuwa kama angekuwa hai wange deal naye mpaka waone wao wanabaki washindi,kwa ufupi hakuna raisi yoyote anaye ongoza Africa.Africa ndiyo bara ambalo ni shamba la bibi la mataifa makubwa kujichotea rasilimali kwa kadri wanavyo taka.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Lini waarabu nao wataomba radhi/msamaha kwa ushiriki wao wa biashara ya kuteka na kuuza binadamu kama bidhaa na ushahidi ungalipo? Mbona ni wabishi hivyo? Wazungu wanaomba radhi kwa udhalimu walioufanya, why waarabu wawe na kiburi wasiombe radhi wakati kina Tip Tip walijihusisha na unyama huo?
 
Waarabu sio watu wakuomba msamaha.... Wazee wa kujilipua kwao msamaha ni kama kuomba hukumu ya kifo
 
Hali ni nguvu ulaya, miaka michache ijayo somo litaeleweka zaidi. msukosuko ulioikumba ufaransa kwenye makoloni yake Afrika ndio unaenda kutokea kwa wakoloni wengine sehemu nyingine. Ziara unazoziona sasa ni za kujaribu kujikosha ili hali iendelee kuwa kama zamani.

Kuna nchi ndani ya bala la ulaya zinapambana kuwa "Superpower" kuchukua nafasi za ujeremani uingeleza na ufaransa, ...siku zijazo utaona viongozi wao wakipishana angani kuwahi ushawishi ndani ya bara wanaloita la giza.... Yajayo yanafikirisha!.
 
Dipiiworld wakae mguu pande..
Hawawezi kukubali mwarabu aingie kwenye koloni zao
Ni swala la muda kutakuwa na 360 U-turn
 
Badala wajadili mambo ya msingi wanaomba kurudishiwa mafuvu na mijusi. Tuna mafuvu na mijusi kibao ufipa wao watume muamala basi.
Bufa ingekuwa ndugu yako amenyongwa na Mjerumani wakakata kichwa na kwenda kukiweka Makumbusho huko Ujerumani ungeelewa kwa nini baadhi yetu wanataka hayo mafuvu yarejeshwe.

Na wengi wanaotaka kurejeshewa hayo mafuvu ni ndugu wa wale watemi ambao wao siyo kazi yao kuomba vya maana toka kwa hao Wajerumani. Serikali ndiyo inapaswa kuomba hivyo vya maana na haijazuiwa kufanya hivyo na hawa wanaotaka mafuvu na viwiliwili vya ndugu zao
 
Badala wajadili mambo ya msingi wanaomba kurudishiwa mafuvu na mijusi. Tuna mafuvu na mijusi kibao ufipa wao watume muamala basi.
Nyie watu weusi mna aina yenu ya ubongo😂😂😂
 
Watanzania mna aina yenu ya ubongo watu wamekazania kudau mafuvu ya wafu, na mamijusi kafiri kama ndio yatawaletea akili na ubunifu.
 
Bufa ingekuwa ndugu yako amenyongwa na Mjerumani wakakata kichwa na kwenda kukiweka Makumbusho huko Ujerumani ungeelewa kwa nini baadhi yetu wanataka hayo mafuvu yarejeshwe.

Na wengi wanaotaka kurejeshewa hayo mafuvu ni ndugu wa wale watemi ambao wao siyo kazi yao kuomba vya maana toka kwa hao Wajerumani. Serikali ndiyo inapaswa kuomba hivyo vya maana na haijazuiwa kufanya hivyo na hawa wanaotaka mafuvu na viwiliwili vya ndugu zao

Una uhakika gani hakuna ndugu yangu?

I can careless about mafuvu ya miaka 100 iliyopita hata angekua ndugu yangu wa karibu hakuna point ya kurudisha mafuvu. Hawa kimsingi wanadhani watapata hela za utalii kwa kurudishiwa hayo mafuvu. I hate to break it to you hakuna mmatumbi bongo ataenda kuangalia mafuvu tena kwa kulipia, hayo ni mambo ya mizungu na hao wazungu hawatakuja bongo kwa wingi kisa mafuvu.

Waulize ndugu zao kati ya mafuvu na muamala wanachagua kipi uone kama kuna mtu atachagua mafuvu.
 
Back
Top Bottom