Kwanini walevi wakiambiwa wamelewa wanachukia?

Kwanini walevi wakiambiwa wamelewa wanachukia?

Utaniitaje mlevi wakati ndio mlipa kodi mkubwa nchi hii.Utaniitaje mlevi wakati nina usafiri binafsi,utaniitaji mlevi wakati watoto wangu wanasoma shule sio za kata,utaniitaje mlevi wakati nina nyumba ya kuishi nzuri tu,Utaniitaje mlevi wakati nimekuzidi wewe mnywa kahawa kijiweni,hebu nionyeshe maendeleo yako sababu tu hunywi.
Tuheshimiane braza usiingie anga zetu kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake nyie ndio mkiona mtu kaendelea huku anakunywa mnamuita ni FREE MASON.
WAITER ONGEZA K-VANT NA PELEKA MOJA MOTO MEZA ILE
😂😂😂🙌🙌
 
Akikubali kuwa kalewa huyo hajalewa! Mlevi lazima uwe mbishi kidogo..
Walevi wanabishiaga hadi nyimbo,wengine mpaka taarifa ya habari..😂
🤣😂🤣 Wanajiita walipa kodi
 
Bila shaka wote humu ni wazima.
Na wale wenye changamoto za hapa na pale nizidi tu kuwaombea Kwa Allah awatatulie shida zao.

Moja Kwa moja niingie kwenye lengo la kuuliza swali langu hili ni Kama ifuatavyo.

Iko wazi kuwa Kila mtu anafurahia Kila anapofanya kitu ambacho anaona kiko sawa. Na mara nyingine haiwi aibu kujinadi Kwa watu kuwa yeye ni mtu wa namna gani. Mtu akila chakula kizuri haiwi aibu kwake Kama ataulizwa amekula nini ikawa hawezi kujibu wazi wazi.

Sio jambo la aibu Kwa mtu mswaliji kujibu narudi msikitini endapo ataulizwa ulikuwa wapi hali kadhalika wakristo nao watakujibu kuwa wanarudi kanisani bila aibu na Kwa furaha tele.

Iweje hawa walevi na wanywaji wanapenda kuvunga wanapoulizwa maswali inayoendana na taratibu na mazingira Yao Kwa muonekano wao wa nje?

Kwani ulevi kwao wao sio sehemu ya furaha?
Kwanini hawapendi kuambiwa kuwa wamelewa wakati kilabuni/bar wanaenda Kwa hiyari yao?
Kwani nyie walevi mnatuchukuliaje sisi tusiolewa katika jamii?


Naomba kuwasilisha swali langu Kwa masikitiko makubwa sana.


Ahsanteni...
Umajuaje kama na wewe siyo mlevi?
 
Ukisikia hizi kauli jua kashalewa mtu

Bro mm nishawai kukuvunjia heshima...........[emoji16][emoji16]

Unanijua mm ni nani.........[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Dah bro mm nakukubali sana toka kitambo icho........[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]



Sent from my using JamiiForums mobile app
Hahaha!

Hiyo kauli namba moja ni common zaidi.
 
Wanataka tuwaite walipa kodi
Jina sahihi kabisa. Ukiendesha mkoko wako kwenye lami unatembea juu ya pesa ya huyo unayemwita mlevi.

Ukiona mtu anakunywa, kwanza mpe pole kwa majukumu. Kisha umshukuru kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuletea maendeleo.
 
Back
Top Bottom