Kwanini wali unaotokana na mpunga unaolimwa katika maeneo ya nchi yetu hivi sasa siyo hauna ladha na siyo mtamu?

Kwanini wali unaotokana na mpunga unaolimwa katika maeneo ya nchi yetu hivi sasa siyo hauna ladha na siyo mtamu?

Na ule mchele wa kitumbo ndio ulitoka Thailand. Au wa Thailand ulikuwa mwingine, kipindi mdogo tulitazama movies za Tony Jaa tukaijua Thailand hasa Bangkok (Mukandara Lufufu aliita Bankoko). Nikasikia na mchele unatoka Thailand nikaitambua nchi kirahisi.
Nashukuru kwa masahihisho mkuu. Ni Thailand kweli sio Taiwan. Asante.
 
Ninaomba Wizara ya Kilimo ufanye utafiti ni kwa nini wali unaotokana na mpunga unaozalishwa katika maeneo yanchi yetu ladha yake siyo tamu? Nimenunua mchele ambao ni mzuri kabisa lakini ulipopikwa kwa kweli hauna ladha na siyo mtamu.
Sio wali tu vyakula vingi mfano ndizi za kuiva, matikiti maji, maembe nk.
 
Mchele mtamu Tz nzima ni waziwa rukwa bei sasa 1500 kipindi hiki cha mavuno kwani unapandwa matopeni, wakyela mbaya sana.
 
Kwa maisha yalivyo hiyo ladha utaipataje??
 
Wali umezoeleka sana ndo mnaona hauna ladha, enzi hizo wale siku moja au mbili kwa wiki lazima uwe mtamu.

Sio wali tu hata papuchi hazina ladha.
 
Hebu waliokula wale wenye virutubisho mtupe mrejesho.
 
Ninaomba Wizara ya Kilimo ufanye utafiti ni kwa nini wali unaotokana na mpunga unaozalishwa katika maeneo yanchi yetu ladha yake siyo tamu? Nimenunua mchele ambao ni mzuri kabisa lakini ulipopikwa kwa kweli hauna ladha na siyo mtamu.

Hata kunukia hakuna.

Na viazi Ulaya ni hivyo hivyo.

Havina unga, havinukii kama zamani .

Vimejaa majimaji tu
 
Back
Top Bottom