DOKEZO Kwanini Walimu Kilwa tunalazimishwa kubaki CWT? Wengine tunataka kuhamia CHAKUHAWATA?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Poleni sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Wakurugenzi na maofisa utumishi hata makatibu tawala wa mikoa ni wahusika wakuu katika manyanyaso haya kwa walimu . Serikali ya mh Samia na waziri wa tamisemi mnafurahia unyanyasaji huu??

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
CWT ife tu Haina msaada zaidi ya kupunguza Pato la mwalimu. Majizi makubwa !!

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Nisingependa kutambulika Kwa jina langu.

Naomha Serikali iingilie kati suala hili. Kuna michezo inafanyika ngazi za wilaya Walimu wanaotaka kuhama CWT kwenda CHAKUHAWATA wanalazimishwa na Maafisa Elimu ngazi ya wilaya kubaki kwa kupewa vitisho mbalimbali

Kama Sheria inasema kila mtu yuko huru kuanzisha au kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi sasa iweje walazimishwe kubaki CWT?

Je, hii ni sawa na haki wanachofanyiwa Walimu?
 
Cwt kilikuwa na nguvu gani?
 
Kiteto HRO anaitwa John anasema zoezi limesitishwa japo mkurugenzi alishasign barua mtoa makato kamgomea boss wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…