... kuna mentality za kijinga mingoni mwa wanaume wengi wa kitanzania waliofikia levels za bachelors, phd's, etc. Kwanza kuoa mwanamke aliyesoma (graduate, etc.) ni kujitafutia matatizo - dharau, viburi, n.k. Mwanamke aliyesoma akipata kazi (+ elimu aliyonayo) ni jeuri sana; hakuna heshima ndani ya ndoa!
Pili, kuoa mbumbumbu totally wakati wewe angalau umegraduate nayo ni changamoto nyingine - watanionaje? Mke hawezi hata kuchomekea vijimaneno vya Buckingham kwenye sms au maongezi mbele ya wageni? So, uki-balance hayo mawili ndipo hapo walimu wa msingi + manesi (certificates na diplomas) wanapojipatia "bahati" ya kuolewa maana wana-fit mentality za wanaume graduates wa kibongo!
By the way, hao walimu na manesi huwa hawajilengeshi kwa mbumbumbu; mara nyingi kigezo kikuu ni elimu au utajiri. Ikitokea vinginevyo ni nadra sana.