Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,503
- 13,463
Kisa cha kwanza.
May 20, 1948 UN ilimteua Count Folke Bernadotte kuwa mpatanishi mkuu katika mgogoro wa Israel na Palestina.Mapendekezo ya Count Folke Bernadotte
1. Kurejesha wakimbizi wa Kipalestina: wakimbizi wa Kipalestina waruhusiwe kurejea kwenye makazi yao au kulipwa fidia kwa mali zao zilizopotea.
2. Kurekebisha mipaka.
3. Kuiweka Yerusalemu chini ya udhibiti wa kimataifa.
Bernadotte aliuawa Sept 17, 1948 mjini Jerusalem na kundi la kiyahudi la Lehi ambalo lilikuwa linapinga mapendekezo yake.
Kundi la wanamgambo la Lehi lilikuwa linaongozwa na Yitzhak Shamir na Yitzhak Shamir alikuwa moja ya viongozi watatu waliopanga mauji ya Bernadotte.
Kisa cha Pili
Oslo Accords 1993Aliyekuwa PM wa Israel Yitzhak Rabin na kiongozi wa Palestina na chama cha PLO Yasser Arafat walianzisha mazungumzo ya siri nchini Norway juu ya amani ya mataifa yao. na hatimae 1993 Oslo 1 ilisainiwa nchini Martekani na hatimae Oslo II ikasainiwa 1995 Taba - Egypt.
Oslo ilikuwa na mapendekezo kadhaa lakini haya matatu hayawakuwafulahisha Waisrael.
1. Kurejesha maeneo yaliyokaliwa:- Vikosi vya Israel kutoka ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharbi.
2. Kutambua PLO: Hii iliwakasirisha baadhi ya Waisraeli ambao waliona PLO kama kundi la kigaidi.
3. Haki ya kurejea kwa wakimbizi wa Kipalestina.
Oct 1994 Tuzo ya Nobel ya amani inatolewa kwa viongozi watatu.
Nov 4, 1995 mjini Tel- Aviv Waziri Mkuu wa Israel Yitzhak Rabin anauawa kwa kupigwa risasi na kijana Yigal Amir myahudi na mfuasi wa mrengo wa kulia aliepinga makubaliano ya Oslo.
Baada ya kuawa kwa Rabin na kijana wa kiyahudi, aliyekuwa Waziri wa mamo ya nje Shimon Peres ambaye pia alikuwa mmoja wa washindi wa tuzo ya Nobel anachaguliwa na chama cha Labour kumalizia mda wa Rabin mpaka uchaguzi mkuu wa 1996 ambapo Benjamon Netanyahu anakuja kuchukua Uwaziri Mkuu.
Benjamin Netanyahu ni mwanasiasa wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali na ni Waziri Mkuu wa Israel kwasasa kupitia chama cha Likud.
Chama cha Likud: Ni chama cha kisiasa cha mrengo wa kulia nchini Israel kilichoanzishwa mwaka 1973. Likud kinaunga mkono sera za soko huria, usalama wa taifa, na mara nyingi kimekuwa na msimamo mkali kuhusu masuala ya ardhi na makubaliano ya amani na Wapalestina.Chama hiki kimeongozwa na viongozi maarufu kama Menachem Begin, Yitzhak Shamir, Ariel Sharon, na Benjamin Netanyahu.
Chama cha Labour ni chama cha siasa za mrengo wa kushoto nchini Israel, Kimekuwa kikijulikana kwa sera zake za kijamii na kiuchumi zinazolenga usawa na haki za kijamii. Labour kimekuwa kikihimiza mazungumzo ya amani na Wapalestina kama Oslo Accords I na II.
Chama hiki kimeongozwa na viongozi maarufu kama David Ben-Gurion, Golda Meir, Yitzhak Rabin, na Shimon Peres. Labour kimekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Israel, ingawa umaarufu wake umepungua kwasasa.
Unamuona nani kikwazo cha amani Mashariki ya Kati?