Kwanini waliosomea sheria huzivunja sheria?Na kwanini waliosomea sheria hujidai wapo juu ya sheria?

Kwanini waliosomea sheria huzivunja sheria?Na kwanini waliosomea sheria hujidai wapo juu ya sheria?

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
Habarini wakuu,

Karibuni tutete kidogo hapa,

Nina hili swali moja tu wadau wenzangu na swali lenyewe ni hili hapa.

Kwanini waliosomea sheria huzivunja sheria?Na kwanini waliosomea sheria hujidai wapo juu ya sheria?

Hapa nawaombeni tujadili bila maneno ya matusi twendeni kwa hoja.
 
fafanua swali lako, tusije tukawa tunajibu maswali ya waungaji mkono wa meko!
 
Sheria ni suala ambalo halina majibu ya wazi kama hesabu kwamba 1 + 1 =2 katika base ten math.

Sheria inakwenda kwa ubishi na majadiliano.

Kwa hiyo, inawezekana - si mara zote, ila inawezekana- pale wewe mbumbumbu wa sheria unapoona sheria imevunjwa, gwiji wa sheria anaweza kukuonesha kwamba hapa sheria haijavunjwa, ni uelewa wako mdogo tu wa sheria ndio unaokufanya uone kwamba sheria imevunjwa.

Na akajitetea hivyo, mpaka mahakama ikakubaliana naye.

Chukulia mfano, Tundu Lissu anaweza kuitwa kituo cha Polisi akaripoti.

Akasema siendi.

Ukaona kavunja sheria.

Kumbe, kisheria, hakuna sheria ya kumuita mtu kituo cha Polisi. Polisi kama wana ushahidi mtu kavunja sheria wanatakiwa kumkamata, na kama hawana ushahidi mtu kavunja sheria wanatakiwa kumtafuta alipo na kumuhoji.

Sasa, Tundu Lissu akisema siendi kituo cha Polisi, kwa kuijua sheria zaidi yako, wewe unaweza kuona kavunja sheria, kumbe anaijua na kuitekeleza sheria.

NB: Huo ni mfano tu.

Zaidi, mjuzi wa sheria anaweza kuvunja sheria akijua atajitetea vipi, akijua mfumo mzima ulivyo na jinsi ambavyo hatapata madhara yoyote hata baada ya kuvunja sheria (mfano wa Jecha).
 
Siyo kweli, Jiwe hajasomea sheria lakini anavunja sheria sambamba na katiba.
 
Lissu anazijua sheria na ndio maana wanamshindwa na kuishia kusema anavunja sheria kumbe wao ndio wavunjaji wa sheria. Watanzania tafuteni kuunda taifa lenye haki na uhuru la sivyo mtajuta siku moja kwa kuunga mkono watu wasiofuata sheria na haki.
 
Back
Top Bottom