Sheria ni suala ambalo halina majibu ya wazi kama hesabu kwamba 1 + 1 =2 katika base ten math.
Sheria inakwenda kwa ubishi na majadiliano.
Kwa hiyo, inawezekana - si mara zote, ila inawezekana- pale wewe mbumbumbu wa sheria unapoona sheria imevunjwa, gwiji wa sheria anaweza kukuonesha kwamba hapa sheria haijavunjwa, ni uelewa wako mdogo tu wa sheria ndio unaokufanya uone kwamba sheria imevunjwa.
Na akajitetea hivyo, mpaka mahakama ikakubaliana naye.
Chukulia mfano, Tundu Lissu anaweza kuitwa kituo cha Polisi akaripoti.
Akasema siendi.
Ukaona kavunja sheria.
Kumbe, kisheria, hakuna sheria ya kumuita mtu kituo cha Polisi. Polisi kama wana ushahidi mtu kavunja sheria wanatakiwa kumkamata, na kama hawana ushahidi mtu kavunja sheria wanatakiwa kumtafuta alipo na kumuhoji.
Sasa, Tundu Lissu akisema siendi kituo cha Polisi, kwa kuijua sheria zaidi yako, wewe unaweza kuona kavunja sheria, kumbe anaijua na kuitekeleza sheria.
NB: Huo ni mfano tu.
Zaidi, mjuzi wa sheria anaweza kuvunja sheria akijua atajitetea vipi, akijua mfumo mzima ulivyo na jinsi ambavyo hatapata madhara yoyote hata baada ya kuvunja sheria (mfano wa Jecha).