Kwanini Walokole wanaamini Kila gumu wanalopitia ushirikina umehusika?

Eti mtoto wake au kijana wake MLEVI WA POMBE, MRAIBU WA MADAWA YA KULEVYA KWA AJILI YA KAMPANI YAKE...AU BINT KAANZA UMALAYA...AKIENDA KWA MWAMPOSA NA WENZIE ANAAMBIWA KUNA MTU KATIKA NDUGU ZAKO WA KARIBU AU JIRANI YAKO KAWATUPIA PEPO WANAO...NONSENSE...
 
Walokole ni watu gani hasa? Tuanze hapo.

Kwa uelewa wangu, kila imani ina miongozo yake, kwahiyo labda hawa watu unaowazungumzia wanaongozwa na imani zao kuchukulia kwamba kila baya linaletwa na uchawi...

Sioni kama kuna shida...
 
65 ya matatizo ya watu kwenye nchi za kiafrica ,sio natural cause ethical
Ni mkono wa mtu au ni mizimu
Kutokuoa
Ndoa kuvunjika
Watu kuwa waraibu wa pombe sio vitu vya kusolve kwa kutumia akili zako za kukariri upo ufahamu beyond ulionao binti
Sasa mkuu, husimamii biashara zako ipasavyo, MDA mwingi unautumia makanisani, umewaachia Watu Baki,wanafanya Bora liende

Hivi hapo napo utasema unarogwa?
 
Usemalo Ni kweli kabisa, huyu jirani yangu tangu afeli kurejesha mikopo yake, na biashara zake zikayumba, na akaanza kusali haya makanisa ya kilokole, amekua anajitenga na sisi kabisa
Mimi nilikuwa na jirani yangu...nashangaa naenda dukani unaambiwe yule msipokee pesa yake...chumq ulete yule...unaishia kucheka tu...kwa sababu hujui hata huo uchuma ulete unafanyikaje...ningeenda kuufanyia bank...
 
Ukisoma sn biblia unakuwa muoga na kujitisha mwenyewe
 
Inaonekana wazi wewe Una matatizo sana zaidi ya hao walokole unaowataja!!!!
 
Yaani vitu vya HOVYO kabisa,
Mtu analea watoto WA kiume kimayai
Wakiwa mashoga, anaenda kukemea pepo, anashindwa kukemea tabia za kijana wake kushinda na watoto WA kike na kuact kike kike..
 
Ndivyo wanavyoaminishwa na manabii wao ili wawakamue pesa bila huruma mkuu.
 
Hao ni wajinga sana kwa kweli kuna sehemu nlikuwa nafanya kazi na maza wa kilokole ni biashara yake nilikuwa namuweka kamba tu kuja kushituka mimba mtoto kafanana na mfanyakazi wake kilichofata nilijikuta nipo mkoa mwingine tu na bado ni MOST WANTED
 
Mimi nilikuwa na jirani yangu...nashangaa naenda dukani unaambiwe yule msipokee pesa yake...chumq ulete yule...unaishia kucheka tu...kwa sababu hujui hata huo uchuma ulete unafanyikaje...ningeenda kuufanyia bank...
Ha ha ha....
Niliwai kumuacha wife dukani
Nkikuta short ya laki 2, kaja na story za chuma ulete.

Nkamwambia ntakupasua, pesa zangu, usije niletea huo upumbavu. Akajiliza, nkaamua kumpotezea.

Siku nafanya usafi kwny droo, nazkuta laki 2 Zimejibana kwny faili la risiti za mizigo, zishaota Hadi ukungu.

Hapo keshakemea pepo Hadi Basi😅
 
🤣🤣🤣
 
Hii ni mentality ya Watanzania karibu wote japo Walokole wamezidi.

Fuatilia status za wengi utasikia, "Nawapenda mnaonipenda, maadui zangu mkae mbali, hata mkinisema sipungukiwi kitu, mnanijua sana kupita mama yangu"...
 
Hii ni mentality ya Watanzania karibu wote japo Walokole wamezidi.

Fuatilia status za wengi utasikia, "Nawapenda mnaonipenda, maadui zangu mkae mbali, hata mkinisema sipungukiwi kitu, mnanijua sana kupita mama yangu"...
Kwamba wanarusha Sana vijembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…