Kwanini wanajeshi wanapenda sana kukopa vitu ovyo?

Kwanini wanajeshi wanapenda sana kukopa vitu ovyo?

Hizo posho zinakuja pamoja na mshahara. Nina uhakika na hili jambo. Hakuna pesa inaiingia katikati ya mwezi.
Mkuu humu jukwaani kuna uzushi hadi unajiuliza huyu mtu ni wa aina gani?

Utasikia mwingine anakwambia mshahara wa wanajeshi ni tarehe 18 yaani ni uzushi mtupu.

Mishahara nchi nzima inatoka siku moja kwa watumishi wa umma bila kujali kada. Hizo posho zipo ndani ya mishahara.
 
Ukishakua na mshahara mdogo alaf ukaweka starehe mbele lazima uwe kero kwenye jamii na madeni ya kutosha.

Mshahara mdogo ni lazima uwe na nidham katika matumizi, ukikosa nidham basi na mshahara pia utakudhalilisha
 
Mkuu unaanzia wapi ili umwone huyo oficer? Maana ukifika getini kwao ukiwaona wale MPs jasho linakutoka kabla hujaeleza shida yako!
Wewe ni mpumbavu kiasi hiki?

Yaani kumuona tu MP jasho likutoke kwasababu gani?

Mbona mimi naingia kambini kwa shida mbalimbali ikiwemo matatizo yanayotokea mtaani tunapoishi na hakuna shida yoyote getini.
 
Ukitaka usipate tabu hata usiwakopeshe hao watu na kama wanakuja sana kwenye biashara yako wakataze au zuia huduma sio lazima ufanye nao biashara
 
Hii imekuwa kero sana baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakikopa madukani na hawarudishi vitu na pengine hutumia ubabe wao kutokulipa hata unakuta ukimpeleka polisi ana achiwa tu maana hutumia kazi yao kujiona wakubwa kwa wenzao yaani wanapewa pesa kubwa kila mwezi lakini huishia kwenye pombe na kukopa hovyo sana wanajeshi badilikeni
Askari ni chakula cha risasi wakati wowote unaweza ukaeksipaya kabla ya kulipa deni, hivyo ni mtindo wa kucheza patapotea.
 
Hii imekuwa kero sana baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakikopa madukani na hawarudishi vitu na pengine hutumia ubabe wao kutokulipa hata unakuta ukimpeleka polisi ana achiwa tu maana hutumia kazi yao kujiona wakubwa kwa wenzao yaani wanapewa pesa kubwa kila mwezi lakini huishia kwenye pombe na kukopa hovyo sana wanajeshi badilikeni
Elimu na nidhamu ya fedha ni muhimu,so yawezekana weeng hili swala hawalizingatii
 
Back
Top Bottom