Kwanini wanamuziki wa Tanzania hawapendani na kushirikiana kama wa Nigeria?

fundi bishoo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2018
Posts
14,264
Reaction score
27,132
Habari za jioni wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, ni muda mrefu nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa muziki mtamu na wenye ladha tamu kutoka Africa ya Magharibi(hasa Nigeria.

Kiukweli wenzetu wana mafanikio makubwa sana kwenye muziki wao tofauti na sisi wa East Africa au hata South Africa. Na mafanikio yao yanatokana na ubunifu, juhudi na USHIRIKIANO baina ya wasanii, wataarishaji na waongozaji.

Kwenye jambo lolote bila ya ushirikiano na juhudi halitoweza kufanikiwa na jambo hilo(USHIRIKIANO, JUHUDI) wasanii wetu wa bongoflavour hawana kabisa. Wengi wao ni wanafiki japo sio wote na hawapendi kabisa mafanikio ya wengine au hata kujifunza kupitia mafanikio ya wengine.

Wakiona mwenzao kafanikiwa kidogo wanaanza kumuwekea ngumu(kinyongo). Mifano ya wasaníi wanaochukiwa kisa mafanikio yao ipo na mnawajua.

Kwanini wasanii wa bongoflavour hawapeani support hata ya kusupport kazi za wenzao? Hata mkongwe Dully alishasema hilo kipindi ametoa ngoma ya bomberdia alitokwa na povu sana kuhusu wasanii wa bongo kuwekeana ngumu kwenye tasnia.

Nawaomba wasani wa bongo wapeane support kama walivyo wenzetu. Hawa wakina PHYNO, OLAMIDE, WIZKID, DAVIDO, TEKNO, REEKADO BANKS, LIL KESH, REMINSINCE, OREZI, YCEE, TIWA SAVAGE, YEMI ALADE, ARAMIDE, SIMI , OLADIPS NK ni mazao ya waasisi wa burudani huko kwao mfano Fella Kuti(japo sijawah kumsikiliza), Don Jazzy, P Square, Dbanj, J Martins, MI na wengineo.

Pia ni ubunifu wa maproducers wakali kama Legendary Beatz, Tekno, Young John(the wicked producer), Don Jazzy, E Kelly, Pheelz mr producer Maleeky berry, Mastercraft, Shizzy n.k.

Utatufanya tuzidi kuupenda muziki wao miaka nenda rudi kama wasanii wetu hawatakuwa na utayari wa kushirikiana.

NB: Ninapenda miziki ya KINAIGERIA wanajua sanaa

[HASHTAG]#YUNGTEmpeR[/HASHTAG]
 
Acha Uongo, Nigerian Hawapendani We Hujui Tu.
 
umoja ni nguvu na utengano ni ____
 
wanashirikiana kivipi mkuu tupe hata ka mfano mi nnavyojua wasanii wa Nigeria hususani wa muziki na filamu wanaongoza kwa kuchukiana kwani kuna mabifu ya hatari hatari yanayosababishwa na wivu wa maendeleo,mapenzi,kushikana uchawi na kadhalika na mifano ipo ila ngoja nilog out nalala
 

wanashirikiana katika kupush mziki wao mfano ata kwenye collaboration hata msanii hajulikani lakin anaweza akapiga collabo na msanii mkubwa tofauti na bongo huwezi ukapiga collabo na mondy au kiba kirahisi utazungushwa mpka miguu iote matende japo sikatai hilo swala la uchawi lipo uko nigeria na beef kwenye mziki ni lazm mziki bila bifu sio mziki labda kwaya au kaswida
 
Sijui ni kwa nini, Ila burudani huwa naipata kwa hapa Celine Dion, Boyzone, Backstreet Boyz, BoyzIImen, Nsync, Westlife, Laura Pausini, L.Armstrong,Parton,N.K
 
Elimu Elimu Elimu.

Tanzania inawajinga wengi waliozalishwa na huu mfumo mbovu wa Elimu yetu.

Mtu anaamini ili awepo nandy lazima ruby ashushwe au ili awepo mboso lazima aslay ashuswe au ili awepo kiba au chibu inabidi mmojawapo asiwepo kabisa.

Wasanii hawaheshimu profession yao ndiyo maana wanacatch feelings za kilimbukeni ndiyomaana hawapendani.
 


fAcT √√√√√√√√Π
 
 
ni kwel kk wanigeria wanajua sana pia producetz wao ni creative sana biti kali sana wanamake mf ngoma ya IF ya Davido kaandika Tekno na Kutengeneza fresh na kamuuzia davido ngoma ikawa kali mno je apa bongo kuna msanii anaweza kukubal kaandikiwa na flan na kuproduce kwake?? Selebobo anaproduce na anaimba na wenzake wananua
 
amini hvo bongo kutwa mtandaoni kupost majungu tu
 
Reactions: Gef
Wasanii wa Nigeria hawana mafanikio kisa ushirikiano.

Ngoja niiweke vizuri.

Hakuna sehemu yoyote duniani wanamuziki wana mafanikio kisa ushirikiano.

Davido bifu na Wizkid.

Don Jazzy bifu na D'Banj.

Skales bifu na Lebo.

Wizkid bifu na Lebo.

Kiss Daniel bifu na Lebo.

Runtown bifu na Lebo.

Huko nje.

East Coast bifu na West Coast.

Watu hadi wakafa.

Nigeria msanii ana mafanikio kwa sababu kinachopatikana yeye anakula 40% mfano Wizkid na Meneja anakula 60% lakini hii 60% inamaanisha meneja atatoa yeye hela ya tour, promotion na gharama zingine ndogo ndogo.

Ukija kwetu.

Fella & Co wakala kila kilichozalishwa na Ya Moto.

Clouds & co ikala kila kitu cha Saida.

Fella & Co ikala kila kitu cha Spark, Niki na Leo Tundaman.

Kwetu sisi maguru wa entertainment ni Fella na Clouds, wakikubania hutoboi, wanakunyonya kila kitu mafanikio utayaona wapi?

Ni maguru ndiyo lakini wametarget soko la watu ambao wakiimbiwa
'Mimi zezeta, zezeta..' Au 'Ooh mimi sikomi' wameridhika na ndo ujinga huo.

Kwahiyo braza ushirikiano hauna huo mchango unaotaka kutuaminisha hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…