fundi bishoo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2018
- 14,264
- 27,132
Habari za jioni wakuu
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, ni muda mrefu nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa muziki mtamu na wenye ladha tamu kutoka Africa ya Magharibi(hasa Nigeria.
Kiukweli wenzetu wana mafanikio makubwa sana kwenye muziki wao tofauti na sisi wa East Africa au hata South Africa. Na mafanikio yao yanatokana na ubunifu, juhudi na USHIRIKIANO baina ya wasanii, wataarishaji na waongozaji.
Kwenye jambo lolote bila ya ushirikiano na juhudi halitoweza kufanikiwa na jambo hilo(USHIRIKIANO, JUHUDI) wasanii wetu wa bongoflavour hawana kabisa. Wengi wao ni wanafiki japo sio wote na hawapendi kabisa mafanikio ya wengine au hata kujifunza kupitia mafanikio ya wengine.
Wakiona mwenzao kafanikiwa kidogo wanaanza kumuwekea ngumu(kinyongo). Mifano ya wasaníi wanaochukiwa kisa mafanikio yao ipo na mnawajua.
Kwanini wasanii wa bongoflavour hawapeani support hata ya kusupport kazi za wenzao? Hata mkongwe Dully alishasema hilo kipindi ametoa ngoma ya bomberdia alitokwa na povu sana kuhusu wasanii wa bongo kuwekeana ngumu kwenye tasnia.
Nawaomba wasani wa bongo wapeane support kama walivyo wenzetu. Hawa wakina PHYNO, OLAMIDE, WIZKID, DAVIDO, TEKNO, REEKADO BANKS, LIL KESH, REMINSINCE, OREZI, YCEE, TIWA SAVAGE, YEMI ALADE, ARAMIDE, SIMI , OLADIPS NK ni mazao ya waasisi wa burudani huko kwao mfano Fella Kuti(japo sijawah kumsikiliza), Don Jazzy, P Square, Dbanj, J Martins, MI na wengineo.
Pia ni ubunifu wa maproducers wakali kama Legendary Beatz, Tekno, Young John(the wicked producer), Don Jazzy, E Kelly, Pheelz mr producer Maleeky berry, Mastercraft, Shizzy n.k.
Utatufanya tuzidi kuupenda muziki wao miaka nenda rudi kama wasanii wetu hawatakuwa na utayari wa kushirikiana.
NB: Ninapenda miziki ya KINAIGERIA wanajua sanaa
[HASHTAG]#YUNGTEmpeR[/HASHTAG]