Kwanini wananchi wengi wanadai Masoko yanayoungua hayaungui kwa bahati mbaya bali yanachomwa?

Kwanini wananchi wengi wanadai Masoko yanayoungua hayaungui kwa bahati mbaya bali yanachomwa?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Dhana hii ndiyo inayozungumzwa na Watu wengi mno, kutokana na mazingira yalivyo inaaminika kwamba masoko haya yanapigwa kiberiti, japo haijatajwa hasa ni yupi anayefanya unyama huo.

Lengo langu si kufanya uchochezi, nilichozingatia ni ile methali isemayo MFICHA UCHI HAZAI au MFICHA MARADHI MAUTI HUMUUMBUA, hii ni kwa vile 99% ya raia hawaamini kama moto huu ni ajali, sasa tukiacha hali hii bila kujadili hapa JF na kutafuta ufumbuzi inaweza kuleta mkanganyiko mkubwa sana.

Jambo hili ni lazima lijadiliwe ili kupata Ukweli. Je, ni kweli masoko haya yanachomwa moto au ni ajali tu za kawaida?

Naomba kuwasilisha
 
Nchi hii masoko yote yanaunguaga usiku
Ni muda gani soko litakua halina watu wa kuzuia moto kusambaa? Aah yeah ni asubuhi na mchana ila usiku wanajaa watu wengi sana ni maajabu wanashindwa kuuzuia moto.
 
Hizi chuki tunazozijenga kwa watanzania kuna siku zitatugharimu. Mimi nimejaribu kuvaa uhusika wa wahanga nikajiuliza hivi km mm tu ambaye sijaunguliwa na nahasira kiasi hiki je hao waliounguliwa hali ikoje.Km serikali inaunda tume.

Tume ije na majibu yakurizisha ..sio kesho tusikie panajengwa soko la ghorofa na kwa kauli za kiongozi mmoja jana mm nahisi pale wamachinga waanze tu kutafuta maisha mengine
 
inabidi ifike mahala tukubaliane na kila hali tu sidhani wanaotufanyia ni kwa faida yetu au wao, ila kama ni njia zinazotumika kumfukuza mtu akufukuzae akuambii toka, upo kwa watu siku ya kwqnza unawekewa chakula mboga inachumvi nyiingii,siku ya pili ivyo ivyo yatatu utasepa tu *****
 
Unakuta soko limeungua lakini waliokuwepo wanaanza kuzuiwa kurudi na danadana nyingi. Hili linachangia kuwaaminisha watu kuwa kuna njama.
 
Hilo soko halina vizuizi vya kuzuia moto kuteketeza kila kitu... kiufupi sio soko ni mabanda ya hovyo tu mbao na nylons zimejaa
 
Kinachofikirisha ni masoko kuungua usiku tu...

Lakini uzembe ni matumizi ya kuni/mbao (fuel) kujenga structures zinazohifadhi mali yenye thamani zaidi ya structure husika...

Pia huwa kuna majiko bubu humo ndani ya masoko, waya za umeme zimeungwa ungwa tu, mabanda yameezekwa na materials zinazonasa moto haraka...
 
Dhana hii ndiyo inayozungumzwa na Watu wengi mno, kutokana na mazingira yalivyo inaaminika kwamba masoko haya yanapigwa kiberiti, japo haijatajwa hasa ni yupi anayefanya unyama huo...
Msikilize Hayati hapo
JamiiForums-180840764.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi kamati/tume za uchunguzi ni miradi ya upigaji tu.
 
Back
Top Bottom