Kwanini wananchi wengi wanadai Masoko yanayoungua hayaungui kwa bahati mbaya bali yanachomwa?

Mnyonge mnyongeni lakini mpatiani haki,,hivi kwanini wakati wa jiwe hapakuwa kuchoma masoko lakini wakati wa kikwete na sasa wakati wa samia ndo mambo yamepamba moto.
 
Hilo soko halina vizuizi vya kuzuia moto kuteketeza kila kitu... kiufupi sio soko ni mabanda ya hovyo tu mbao na nylons zimejaa
Moto unaanza aje?
 
Masoko yote huwa yanaungua usiku tu.
Tume zote hazijawahi kutoa ripoti pamoja na mbwembwe za viongozi na tena jana kuna mwingine kasahau kuwa Tume ya Kariakoo mpaka leo zile siku 14 hazijafika na yeye katoa siku 14...
Kuna vitu vinatia hasira kuona watu wanapewa majawabu rahisi wakiwa kwenye nyakati ngumu kama hizi...
Mwishowe tutaambiwa litajengwa Soko la kisasa halafu watagawana vizimba wenyewe kwa wenyewe....
 
Jibu wanalo hao 99% ya raia (sijui ni kwa utafiti upi?).

 
Umewahi kuona report yoyote ya chanzo na sababu za moto. Kuanzia Mwanjelwa, Kariakoo na masoko mengine mengi hakunaga maelezo yanayojitosheleza. Wacha wananchi waamini
 
ngoja tuone kamati inakuja na nini, tuliofuatilia vyombo mbali mbali vya habari nadhani tutakuwa na kitu hasa tukikumbuka ushuhuda wa mhanga mmoja ambaye yeye alisema yu tayari kuwa shahidi na aliona tukio zima
 
ngoja tuone kamati inakuja na nini, tuliofuatilia vyombo mbali mbali vya habari nadhani tutakuwa na kitu hasa tukikumbuka ushuhuda wa mhanga mmoja ambaye yeye alisema yu tayari kuwa shahidi na aliona tukio zima
Kuna report ya moto umewahi ona? Itakuwa muujiza tukipewa. Wanajua Watanzania ni wa kusahau.
 
Mnyonge mnyongeni lakini mpatiani haki,,hivi kwanini wakati wa jiwe hapakuwa kuchoma masoko lakini wakati wa kikwete na sasa wakati wa samia ndo mambo yamepamba moto.
Wakati wa jiwe shule ndio zilikua zinateketea kila siku, hususani shule za ndugu zetu wa upande ule.
 
Hii inatokana na ukweli kuwa hii serikali ya wahuni haiwapendi machinga toka mwanzo.
 
~ Moto unaanza usiku wa manane tu kwenye masoko yote yaliyoungua Tz Mwanjerwa, Kariakoo, Karume n.k
Asubuhi wahanga wanajenga vibanda vyao, polisi wanafika na kubomoa nakuwafukuza!
~ Kiongozi mmoja jana katoa maneno yakuonesha kabisa kuwa pale wamachinga wasipahesabie tena! Kwa haya yote kwanini wananchi wasifikiri kama ni hujuma?!
 
Jiulize hili mkuu
Kwa nini Masoko mengi yanayoungua mkuu wa mkoa ni Makalla?
 
Baada ya kusoma hoja nimegundua
1.Masoko mengi yanaungua usiku tu
2.Watu hawaamini kama ni ajali bali ni kitendo kilichokusudiwa
3.Wengine wanaamini kila anapohamia Amos Makalla masoko yanaungua?
 
Kuna report ya moto umewahi ona? Itakuwa muujiza tukipewa. Wanajua Watanzania ni wa kusahau.
mkuu ni hivi wengi tunataka kila kitu kiwekwe kwenye vyombo vya habari na hivyo vyombo vya habari haviwezi kurusomea ama kutuambia kilakitu wao wanatoa vile ambavyo wanaona vitawavuta wengi kwa wakati huo,
Hizo riport ni mpaka uzitake ndo utazipata na hata hii kama ukihitaji utaipata
 
Basi kama hawawezi kuziweka hadharani, hakuna maana ya kutangaza uchunguzi hadharani.
 
Unganisha dots kuhusu maelezo ya yule kitengo kwamba moto ulisababishwa na Mateja , na yule ofisa wa zimamoto kwamba walichelewa kupewa taarifa za moto , baada ya hapo jiongeze mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…