Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Baada ya kusoma maoni ya baadhi ya wenzetu humu ilipotangazwa ajali ya gari iliyowahusisha wabunge, nimepigwa butwaa na kuibua maswali.
Mosi, kwanini wabunge wanachukiwa hivi?
Pili, wafanye nini hii chuki iondoke?
Tatu, wamepokeaje, kama wamepokea mwitikio huu?
Nne, chama chao nacho kinasemaje?
Tano, spika ambaye wengi wameonyesha kumuombea yasikuwa mazuri anajitafakarije kwa hali hii?
Sita, jibu ni kuwachukia au kuhakikisha hawarejei uchaguzi ujao?
Saba, tatizo ni wabunge au wapiga kura wanaohongwa udohoudoho?
Nane, tatizo ni tume mbovu ya uchaguzi inayochakachua uchaguzi?
Naomba kuwasilisha