Kwanini wananchi wengi wanawachukia wabunge hivi?

Kwanini wananchi wengi wanawachukia wabunge hivi?

Hili ni jibu la vyombo kukolea, hakuna sehemu nilipomtaja Trump.
Kama huwezi au hukuweza kuona 'connection' hapo ina maana ' you're narrow minded; or you have a one track mind'.

Ndiyo, pamoja na kuchangamsha a stale posting, hiyo ya Trump ina relevance katika hayo uliyo yazungumzia kwenye hizo 'whipping' zako. Ni mara ngapi Trump kakataliwa na representatives wa Republicans, hata katika ngwe yake ya mwanzo na wakati akigombea. Hiyo ndiyo iliyo kuwa pointi hapo.
Hiyo 'whipping' unayo izungumzia, ndiyo ina sehemu yake; lakini siyo njia ya kuwaburuza wasiotaka yanayo takiwa na wabunge kama inavyo fanyika hapa kwetu. Hilo ndilo nilo lenga kukujibu.'
 
Hao watu unaowaongelea maamuzi yao ni kutokana government decision au poor supervision ya government.

Wanaingia bungeni na wenyewe ni wabunge; Iła nafasi zao ni za kiserikali. Wanawajibika kama sehemu ya serikali lakini si kwa sababu ya ubunge.

Ndio maana hata wanapojiuzulu nafasi za serikali bado wanabaki kuwa wabunge.

Ni kama Ndugai
Sasa unataka kusema nini hapa?
Kwamba serikali ndiyo inayo wa'whip' wabunge katika nchi hizo?
Kwani hizo serikali, si viongozi wao ndio how ma'prime ministers'; ambao na wao wanawajibika kwa chama chao cha siasa?
 
Usipende kuhalalisha Mambo yako kwa hisia zako. Umeenda kwenye mitandao mingine ukakuta hali ni tofauti??

COMMENTS ZA WANANCHI KTK MITANDAO BAADA YA WABUNGE KUPATA AJARI:

1. TBC waliochangia mpaka sasa ni 539, kati yao 506 wamewatakia kifo na 33 wametoa pole
2. AZAM TV waliochangia hadi sasa ni 161, kati yao 157 wamewatakia wabunge kifo na 4 wametoa pole
3. KITENGE, waliochangia hadi sasa ni 77, wote wamewatakia kifo wabunge.
4. EATV, waliochangia 36, 1 ameonyesha huruma na 35 wamewatakia wabunge kifo.
Hii nimeikuta mahali. Je hao nao ni wana JF??
Vizuri
 
Sasa kuwalaumu wabunge kwa maamuzi ya serikali ambayo ni unpopular ni kuwaonea maana mengine wanalazimishwa kuunga mkono (that’s how part politics work) adhabu yao ni kutowachagua kipindi kijcho na chama (thats what democracy is all about) lakini kusherekea ajali zao huko ni kukosa utu.

Learn politics
Tundu Lissu alipo nusurika kwa risasi zaidi ya kumi, nakumbuka ulisha andika humu humu maoni yako juu ya hilo; lakini leo naona una himiza "utu"!

Ndiyo maana mara nyingi nasema humu kwamba akili yako inafanya kazi kiajabu ajabu sana,.. you'have ana ectopic mind'.

Kuwalinganisha hawa wabunge wetu na hao unao wazungumzia huko kwingine, hilo pia linakuweka nje kabisa ya' rationality'.
hawa wabunge wanawajibika kwa wananchi walio wachagua; au wanawajibika kwa chama, na 'specifically' kwa mtu aliye wapeleka Bungeni? Wewe hapo huoni tofauti kubwa na hao wa nje unao wazungumzia kuwa 'whipped'? Utafanya mlinganisho vipi kwa watu ambao ni tofauti kabisa!

Huku kwenye Bunge la Tanzania; kama mbuge wa CCM hakubaliani na hoja zinazo wasilishwa na serikali, anao wabunge wengine wa chama mbadala anao weza kushirikiana nao kukataa jambo hilo linalo sukumwa na serikali? Kama hakuna, unataka mtu huyu afanye nini, kama siyo kujisalimisha tu kama kondoo.
 
View attachment 3170961
Baada ya kusoma maoni ya baadhi ya wenzetu humu ilipotangazwa ajali ya gari iliyowahusisha wabunge, nimepigwa butwaa na kuibua maswali.

Mosi, kwanini wabunge wanachukiwa hivi?

Pili, wafanye nini hii chuki iondoke?

Tatu, wamepokeaje, kama wamepokea mwitikio huu?

Nne, chama chao nacho kinasemaje?

Tano, spika ambaye wengi wameonyesha kumuombea yasikuwa mazuri anajitafakarije kwa hali hii?

Sita, jibu ni kuwachukia au kuhakikisha hawarejei uchaguzi ujao?

Saba, tatizo ni wabunge au wapiga kura wanaohongwa udohoudoho?

Nane, tatizo ni tume mbovu ya uchaguzi inayochakachua uchaguzi?

Naomba kuwasilisha
Haramu haija wahi kuwa halali.
Acha aachukiwe ili wajue watu tuna hasira nao. Ila Mungu sijui kwanini haku ruhusu watu waimbe ule wimbo wa parapanda!!!
 
Sometimes huwaga nakuelewa Mayor, lakini kwa hili umeuma na kupulizia.

Embu tuyakumbuke mabunge yaliyopita kwa majina ya Maspika wake, tuone ulinganifu wa ulichokitetea.

Bunge la Sitta, Bunge la Makinda na Bunge la Ndugai, je yanafanana ingawa saazingine sura za Wabunge wake ni zile zile?

Bunge la Sitta, kipindi cha Bunge watu walishinda kwenye maTv hadi Serikali ikakasirika na kufanya zengwe la kuzima 'live', kwa nini leo hapana, kuna raia anaweza kupoteza muda kusikiliza Bunge live la machawa?

Tunapochambua tuwe wakweli katika uchambuzi wetu.
Hawa wabunge ni bendera fuata upepo wa Rais aliyepo madarakani kutokana na mfumo butu na wa hovyo wa katiba iliyopo, inayompa nguvu Rais kuchomoa mawaziri kutoka katika wabunge anavyotaka yeye.

Ukikuta Rais ni aina ya mtu tuliyenaye leo, kila mbunge anageuka kuwa chawa mwenye manyoya ili aweze kuonekana na 'mweshimiwa'.

Tafsiri ya yote haya ya kuzomewa wabunge na kuombewa mabaya, ni ujumbe kwa Serikali iliyopo madarakani kwamba haifa hata kwa kulumangila.
 
Back
Top Bottom