Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Tupe sababu za kuwapenda basi.View attachment 3170961
Baada ya kusoma maoni ya baadhi ya wenzetu humu ilipotangazwa ajali ya gari iliyowahusisha wabunge, nimepigwa butwaa na kuibua maswali.
Mosi, kwanini wabunge wanachukiwa hivi?
Pili, wafanye nini hii chuki iondoke?
Tatu, wamepokeaje, kama wamepokea mwitikio huu?
Nne, chama chao nacho kinasemaje?
Tano, spika ambaye wengi wameonyesha kumuombea yasikuwa mazuri anajitafakarije kwa hali hii?
Sita, jibu ni kuwachukia au kuhakikisha hawarejei uchaguzi ujao?
Saba, tatizo ni wabunge au wapiga kura wanaohongwa udohoudoho?
Nane, tatizo ni tume mbovu ya uchaguzi inayochakachua uchaguzi?
Naomba kuwasilisha
Hao ni mzigo kwa jamii. Wapo pale kwa maslahi ya CCM