Sasa wewe hapo Pwani unalima nini... Labda ukavue kambale mtoni, udongo wenyewe hauna rutuba
Pwani ipi yenye udongo usio na rutuba?
Pwani ni jina tu yenye maana ya coastal zone.....wilaya za mkoa wa Pwani ni Mafia, Rufiji, Kibiti, Mkuranga, Kisarawe, Bagamoyo, Kibaha na Chalinze. Tukuulize, ni wapi kuna njaa katika maeneo hayo kisa watu hawalimi?
Maeneo yote hayo yana stawi mihogo, mpunga, mahindi, minazi, migomba, viazi vitamu na viazi vikuu, mikorosho, matunda kama mafenesi, maembe, machungwa, ndimu, mananasi n.k wao wanajilimia as a subsistence economy as food tu chakula cha kawaida, miaka inaenda.
Na Pwani haina mito ya kutosha kuvua kambale. Mtu wa pwani hasaaa humlishi kambale.....ni kama chura.
Ipo bahari inayo mazao muruwa kabisa changu, kolekole, ngisi, pweza, pono, kibua, mkizi, jodari....watakani?
Unavyosikia Pwani unadhani ni pale ferry?
Fungua ubongo huo or die a bogus.