Kwanini wanaonunua Magari kwa Kuyaagiza Moja kwa Moja kutoka 'Majuu' na hawa wanaoyanunua 'Yards za Tanzania' Wanadharauliana sana?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wenyewe wanasema kuna Raha yake Kuliagiza Mwenyewe kutoka Mamtoni ( Majuu ) kuliko Yule ambaye anaenda Kununua Yard tena na Fundi wake kabisa Ili Kubahatisha lililo zuri na salama.

Haya mlio na Magari yenu mliyoyaagizia kutoka Majuu na mliyonunua hapa hapa Yards za Tanzania tafadhali karibuni mtupe Mrejesho na Uzoefu wenu japo nikiri tu kama Mleta ( Mtoa ) hii Mada GENTAMYCINE kuwa sina hata hilo Gari lenyewe, Pikipiki na Baiskeli achilia mbali Guta ila napenda kuona mnavyotambiana / mtakavyotambiana hapa.
 
Mhhh, hii kali. Na kama ni kweli, mtu atajuaje kwamba hii gari imenunuliwa yadi au imeagizwa, kwani kuna namba maalumu za magari ya yadi na yale ya kutoka nje?
 
Gari la kipanya linapatikana kwa shilingi nhapi
 
Wenyewe wanasema kuna Raha yake Kuliagiza Mwenyewe kutoka Mamtoni ( Majuu ) kuliko Yule ambaye anaenda Kununua Yard tena na Fundi wake kabisa Ili Kubahatisha lililo zuri na salama.

Haya mlio na Magari yenu mliyoyaagizia kutoka Majuu na mliyonunua hapa hapa Yards za Tanzania tafadhali karibuni mtupe Mrejesho na Uzoefu wenu japo nikiri tu kama Mleta ( Mtoa ) hii Mada GENTAMYCINE kuwa sina hata hilo Gari lenyewe, Pikipiki na Baiskeli achilia mbali Guta ila napenda kuona mnavyotambiana / mtakavyotambiana hapa.
Gari ya yard inakuwa mkweche. Yaani iko hivi:-
Kuna classes kwenye minada ya magari, class 1 ni bora sana, zimeenda hadi class 7 mikweche iko huko.

Huko mikweche huuzwa bei ndogo sana, na imetembea km nyingi za kutosha hadi kupitiliza.

Wapakistani wanayajumua kwa bei cheee na kuyaleta bongo na kurudisha nyuma kilometres.

Tena magari hayo yana historia mbaya ya ajali, kubadilishwa parts na kadhalika.
 
Ni rahisi tu..Ukiagiza mwenyewe, una uhakika na ubora wa gari lako. Maana litafika bandari, na wewe mwenyewe utalitoa kupitia kwa clearing agent. Sasa hizi za kununua yard, mara nyingi hakuna uhakika kama kila kitu kiko vilevile kama gari lilivyokuja. Kuna wakati kuna "Engineering" huwa zinafanyika kakatika baadhi ya yard - ingawa sio zote. Pia kuna kuna "grades" za magari. Ukienda kwa wauzaji wa magari wakubwa kama "Befoward"; "JapaneseVehicles" utaona hizo grades. Ukienda yard hautaona hizo grade.
 
Nna Carina Ti huu mwaka wa nne Sasa, na nilinunua showroom za hapahapa,

Mi naona hakuna tofauti
 
Gari za grade 4 ndizo Bora zaidi hata kwenye mtandao wa be forward ukiona wameandia hivyo ujue hiyo gari ni Bora zaidi pia kwenye mnada uliofanyika Huko Japan hiyo gari ilikidhi viwango vya ubora
 
Wenyewe wanasema kuna Raha yake Kuliagiza Mwenyewe kutoka Mamtoni ( Majuu ) kuliko Yule ambaye anaenda Kununua Yard tena na Fundi wake kabisa Ili Kubahatisha lililo zuri na salama.

Haya mlio na Magari yenu mliyoyaagizia kutoka Majuu na mliyonunua hapa hapa Yards za Tanzania tafadhali karibuni mtupe Mrejesho na Uzoefu wenu japo nikiri tu kama Mleta ( Mtoa ) hii Mada GENTAMYCINE kuwa sina hata hilo Gari lenyewe, Pikipiki na Baiskeli achilia mbali Guta ila napenda kuona mnavyotambiana / mtakavyotambiana hapa.
Kununua Gari Show room kuna Faida kubwa zaidi ya kuagiza
 
Nna Carina Ti huu mwaka wa nne Sasa, na nilinunua showroom za hapahapa,

Mi naona hakuna tofauti
Miaka minne ni kidogo sana kwa gari....Mimi nina Gari nilinunua 2009 (Zaidi ya Miaka 13 sasa) kutoka Japanese Vehicles - limepiga sana rooutes za Mikoani na Nje ya nchi (hapa kwa majirani zetu) - lakini engine sijawahi kuigusa na iko vilevile kama ilivyokuja. Hiyo ndio heshima ya magari ya kuagiza moja kwa moja na kama ulipata grade nzuri.
 
Back
Top Bottom