Kwanini wanaoruhusiwa kuchinja ni Waislamu peke yao?

Qurani anakiri kuwa Majini ni Malaika walio asi.

AL - JINN - 9 ]
Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia.

1. Na hakika (zamani) tulikuwa tukikaa humo (Mbinguni) na kusikiliza anachosema Mungu.

2. Lakini sasa tumefukuzwa na tukitaka kurudi Mbinguni ili kumsikiliza Mungu tunapigwa na Vimondo.

Maana yake tumefukuzwa
 
Wakristo wameona hakuna haja ya kubishana katika mambo ya kijinga. Ila Mimi sifanyi huo ujinga wa kumuita muislamu kuja kuchinja kuku nyumbani kwangu
 
Wakristo wameona hakuna haja ya kubishana katika mambo ya kijinga. Ila Mimi sifanyi huo ujinga wa kumuita muislamu kuja kuchinja kuku nyumbani kwangu
Kuna muislam ametuma maombi kuja kuchinja kwako???
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Aaah wapi kwangu nachinja mwenyewe
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Kuchinja ni ibada, Wakristo wanashirikishwa ibada wasizo zijua
 
Wengine waliishaachana na ujinga wa kuchinjiwa na wachinjaji wa dini wanachinja wenyewe. Hao wa machinjio ya umma ndio hao wa dini waliowekwa ila haina madhara mwingine akichinja. Ni kasumba tu imewekwa kuamini wa dini fulani wakichinja eti nyama itakuwa ni halali
 
Kitimoto wanayokula nani huwa anawachinjia?
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Tunapopeleka kuchinja kwa waislam ni kwa sababu tunataka rafiki zetu waislam wakija kututembelea wale chakula chetu, wao hawali nyama iliyochinjwa na mpagani (Kaffir). Na kama wewe sio muislam ni mpagani. (Kwa mujibu wa maandiko yao). Sisi ni wakristo wakatoliki, kuchinja ilikuwa lazima tupeleke kwa muislam kwa sababu familia rafiki na yetu walikuwa waislam, tunashinda kucheza kwao na wao wanashinda kucheza kwetu, wazazi wetu nao marafiki. So wakija home wanapiga msosi bila mawazo.
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Hawa kuku tunaokula kwenye mabaa na sherehe unadhani wamepita kibra?
 
Duh yani unatafsiri unavyotaka wewe au sio? hii ndo sababu kwanini Quran inapaswa kusomwa katika lugha husika iliyoteremshwa ili kuepusha tafsiri kama zako.

Quran 72:8 - "(Earlier) we tried to reach heaven ˹for news˺, only to find it filled with stern guards and shooting stars."
Quran 72:9- "We used to take up positions there for eavesdropping, but whoever dares eavesdrop now will find a flare lying in wait for them."

Neno "take up position - kuketi kwa kuibia" na "live - kuishi" yana maana tofauti sana ila katika kiswahili ni rahisi kupotosha maana yake na yote ukasema ni kukaa.
Quran isema wazi kuwa majini sio malaika, strainght forward wala haizunguki in multiple verses, moja ya verse hini hiyo chini
(Quran 18:50) - "And recall when We said to the angels: "Prostrate yourselves before Adam"; all of them fell prostrate, except Iblis. He was of the jinn and so disobeyed the command of his Lord. Will you, then, take him and his progeny as your guardians rather than Me although they are your open enemies?"

(Quran 55:15) "and has created the jinn from the flame of fire."

Ukihitaji darasa zaidi sema kamanda
 
ni sababu ya kuheshimu Imani za dini nyingine, kawaida tukiacha umasikini wetu unapopika chakula mtu yeyote anakaribishwa kula. Kwa sababu waislamu Wana Imani Yao ndio ili waweze kushiriki mlo lazima nyama ichinjwe na mwislam mwenzake.
 
Basi tuache na sisi tuamini majini ni malaika walioasi na nyinyi mbakie kuwa wote ni ndugu regardless ujambazi,uchawi...wenu na mengine yafananayo na hayo.
Wala sina tatizo na hilo, nilichotaka muelewe tu ni kwamba waislamu tunaposema wapo majini waislamu mnapaswa muelewe na muache kukurupuka kudhani tunaongelea hao nyinyi mnaowaita malaika waasi. kwa mafundisho yetu malaika hawezi kuasi, simply hana uwezo huo na hana matamanio hayo.
 
ni sababu ya kuheshimu Imani za dini nyingine, kawaida tukiacha umasikini wetu unapopika chakula mtu yeyote anakaribishwa kula. Kwa sababu waislamu Wana Imani Yao ndio ili waweze kushiriki mlo lazima nyama ichinjwe na mwislam mwenzake.
Karuhusu Waislamu wachinje ni kudumisha ujirani mwema tuliojijengea wenyewe.
Kwa sasa umekuwa kama utamaduni wetu.

Ukiishi mahali penye Waislamu wengi na unataka kuchinja nyama kubwa kama Mbuzi au Ng'ombe tuna watafuta Waislamu ambao ni ndugu zetu watuchinjie ili tujumuike nao katika mlo.

Je Wakristo tungeamriwa tule nyama iliyochinjwa kwa Jina la Yesu tu.
Waislamu mgekubali tuwachinjie Wanyama wenu?

Kwa Jina la Yesu ?
 
Soma hapo
 

Attachments

  • Screenshot_2023-08-04_112054.jpg
    49 KB · Views: 5
Soma
 
hakuna sheria ya nchi Wala ya ukirisro inayosema ili nyama iliwe lazima ichinjwe na mwislam ila u\ila kwa sababu hakuna kizuizi ndio maana kwa nia njema wanaruhusiwa.
Mimi ni mkiristo na baba yangu alisoma seminari pia mkiristo ila Toka utoto tukitaka kuchinja kuku naambiwa mtafute Athumani, Bakari au Selemani aje atuchinjie kuku. Sioni tatizo wakichinja ila tatizo no pale watakapoona ni haki Yao kuchinja-na kuanza kutoza pesa za ajabu kisa lazima wao wachonje. Rejea mgogoro uliotokea Geita kuhusiana na maswala ya kuchinja.
 
Allah alipo sema Malaika wote wasujudu , alasahau iblis sio Malaika ,

Na Kwanini amuadhibu ablis wakate kina Allah walisema Malaika wasujudu ?
 
Mmmmh basi sawa
 
Malaika wana free will mkuu ila wao wanaishi mbinguni na baadhi yao wanapokea command direct kutoka kwa Allah(the almighty ) bila ya kumuona ndiyo maana walimuuliza Allah (the almight) swali ili wapate kufahamishwa kwanini anataka kuwaumba viumbe wengine ilhali watakuja kumuasi yeye .

Kumuuliza pekee inaonesha wanauwezo wa kufanya reasoning na pia wana free will ila sasa wao si kama sisi wao ni ma'asum(hawana dhambi) Allah ( the almighty) amewakinga na kuwaepusha na challenges ambazo sisi na majini tunapitia.

mfano dhaifu labda ni sawa na wanafunzi wawili wanaosoma masomo ya sayansi ila mmoja akawa anasoma theory pekee na mwengine akawa anasoma both theory na kisha anafanya experiments ku prove hizo theory kikawaida yule anayesoma na kufanya experiment huwa ana ufahamu mkubwa sana wa anachokisomea kuliko yule anayesoma theory pekee ukija kupinga hoja ya yule anayefanya experiment na wakati ameshaithibiti anaweza akakushangaa sana tofauti na yule wa theory.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…