Sasa nyie majini mnasema yapo mema na mabaya wakristo hatuna kupepesa macho juu ya majini(malaika waasi) kama mtu anayo akija nayo kanisani yanatimka.Mnadhani tuna kauli mbiu kama yenu ya waislamu wote ni ndugu hata kama ni jambazi,,mchawi,panya road...?
Unalohitaji wewe ni darasa. Tatizo kubwa mlilonalo nyinyi kujaribu kuelewa dini nyengine kwa mafundisho ya dini yenu, acha nikuelezee kidogo huenda ukaelewa waislamu tunaamini nini.
Kwanza kabisa kwetu sisi majini sio malaika walioasi. Miongoni mwa viumbe wengi walioumbwa na Allah (Kuna tunavyovijua na tusivyovijua kwasababu hatuna share katika ujuzi wake isipokuwa kile alichotaka tukijue), kuna viumbe aina tatu ambavyo ni Malaika, majini na watu. Hivi viumbe vitatu vinatoufautiana kimaumbile na kisifa baina ya kimoja na kingine.
1) Malaika - Hawa wameumbwa kwa kutumia nuru, kimaumbile hawajaumbwa wakiwa na maamuzi zaidi ya kutii amri wanayopewa (they dont't have free will), pia hawa hawana jinsia ila wanaweza kujibadilisha katika maumbile tofauti mfano wa wanaadamu (refrence nyingi katika Quran na bible waliwatokea mitume katika umbo la kibinadamu). Pia hawa hawana sifa ya kula wala kunywa.
2) Majini - Hawa wameumbwa kwa moto, wao pamoja na wanaadamu wamepewa uwezo wa kuamua katika matendo yao (They have free will and choice), pia wana jinsia ya kike na kiume hivyo huzaliana kama wanadamu na pia wamepewa uwezo wa kijbadilisha kimaumbile ila hawaonekani katika umbo lao halisia katika macho ya mwanadamu, ila kama wanadamu na wao wanakula na kunywa.
3) Binaadamu - Ndo sisi sasa, asili ya maubile yetu ni udongo. Tofauti zetu na ushabihiano wetu na hao viumbe wengine zimetajwa hapo juu.
Ukizingatia hapo juu utagundua similarity kubwa kati ya majini na watu ni
Free will katika matendo yetu, hili pia ndo sababu tukaletewa muongozo wa jinsi gani ya kuishi hapa duniani, sidhani kama uliwahi kusikia kuna mtume alitumwa kwenda kuwaongoza malaika because hakuna haja hiyo as they do only what they have been comanded by God. With free will siku zote watakuwepo watiifu na wakosaji, kama katika wanadamu kuna watenda mema na pia watenda maovu mf. majambazi, washirikina n.k. pia kwenye majini wapo hivo hivo na moja katika sifa kubwa ya majini waovu ni hii kuwaingia watu, kuwatesa na kuwakufurisha. hakuna jini mwema anayemuingia mtu,
majini wote walio wema wanaishi kwenye jamii zao bila ya maingiliano na wanadamu. Katika lugha nyepesi wote hao wanaosumbua watu ni majini waovu!!!
Jini sio sifa bali ni maumbile, kama ilivyo binadamu na malaika,
bali ushetani ndio sifa ya majini waovu, ila pia binadamu anaweza kuwa na sifa kishetani anapokuwa muovu mfano wa uovu wa majini.