Kwanini wanaoruhusiwa kuchinja ni Waislamu peke yao?

Kwanini wanaoruhusiwa kuchinja ni Waislamu peke yao?

sasa mkristo gani mwenye akili akae vibandani anasubiri kuchinja mnyama ili apewe kichwa miguu na utumbo...
sikuzote ukiona mjinga anang'ang'ania jambo na analifanya liwe kubwa la kidini muache maana ndio kaburi lake la maisha... Watu na akili zao hawawez ng'ang'ania kuchinja
😎
 
Na sio kila Muisilamu anachinja,lazima uwe na hiyo Elimu.Mimi mwenyewe nilikuwa mkristo na nilikuwa nachinja kabla,lakini kulikuwa na makosa makubwa ya uchinjaji
OK. Mkuu ulijisahihishaje? na bado unachinja?
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Haiko hivyo,
Waislam hula vile vilivyochinjwa na Waislam tu.
vs
Wakristo hula vile vilivyochinjwa na yoyote yule.

So wakristo wakitaka waislam nao wale basi ki uungwana (sio lazima) huita Waislam wachinje. Lakini hata wakiamua kuchinja wao wenyewe hawatokatazwa, ila ndo Waislam hawatokula.
 
wakristo tunaruhusiwa kuchinja , sema tunawapa waislam wachinje ili kwa imani yenu msione haramu wakati tunawakaribisha mezani. Tunahofia tukichinja wenyewe mtashindwa kula tukiwakaribisha.
 
OK. Mkuu ulijisahihishaje? na bado unachinja?
Ndiyo ndugu yangu,zamani nilikuwa nashika kuku na kuchinja,lakini baada ya kupata Elimu,sasa hivi nachinja kwa ruksa ya aliyekiumba kiumbe chake.Kwanza lazima nielekee kibra,pila lazima nimuombe Mwenyezi Mungu
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Lakini Waislam wananiangusha bana.

Hawachinji kitimoto.
 
Sasa nguruwe mpaka umpige azimie hayo mambo ya kuchinja watayajua wapi.
 
Kwanini niguse damu wakati wa kuchinja wakati vijana wako jirani? Tena wanafurahia kuja kuchinja kwani hua wanaindoka na kichwa na makongoro.
 
Kukiwa na ulazima wakristo sio wabishi huwapa waislamu wachinje lakini nao wanaweza kuchinja kawaida tu.

Ilo suala la kusema wanamkabishi Mungu gani ndipo wakristo wameona itatokea competition ya kipumbavu isiyo maana, ndio maana wao wamekubali.
waheshimuni pia maana wamevuka viwango vya ustaarabu.
Hahahaha! Eti wamevuka viwango vya ustaarabu
 
Utakuta watu wa Dini zingine mfano Wakristo wakiwa na vitoweo vyao wanapoitaji kuvichinja walio wengi lazima wawapeleke Waisilamu wawachinjie, ina mana wao hawaruhusiwi kuchinja?
Ni kujenga ujirani mwema.Wewe pia ukitaka chinja.
 
Back
Top Bottom