Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Wakuu,
Mie sipendi tubishane sana. Wala si kwamba naleta mambo ya ujuaji kiviiile.
Ukiachana na watu wachache wenye kusifia kila jambo, kama unataka kuamini we ulizia watu 10 hapo mtaani kwenu ni kwa kiwango gani wanaridhika na uongozi wa viongozi wao. Kisha waulize wao wangependa viongozi wao wafanye mambo gani haswa? Bila shaka majibu utakayopata yatakushangaza. Yaani ni kama mbigu na ardhi.
Mfano mzuri: Japo wanasiasa wengi wa Africa hukimbilia kusema vijana wanatumiwa na mashirika ya nje kila vijana wanapopaza sauti zao, ila jaribu kujiuliza ni kwanini Ruto aliamua kufutilia mbali ule mswada baada ya maandamano na si yeye mwenyewe kujua kuwa ule mswada haukufaa hata vijana walipopaza sauti zao kabla ya maandamano?
Mfano mwingine tukisalia hapohapo Kenya, vijana wanadai baadhi ya Mawaziri waliorudishwa ( ambao walikuwepo hapo kabla)hawafai na walitaka mawaziri wapungue kwa idadi ila kupunguza matumizi ya anasa, ila Ruto ameshupaza shingo na kuendelea kufanya atakavyo. Japo nampongeza kwa machache aliyofanya.
Huku mitaani kwetu ukitembelea vijiweni utasikia watu wa kawaida wana maono makubwa sana kuhusu nchi yao na vile wangependa ienende, ila uhalisia ni tofauti kabisa na kinachofanyika.
Watu wana malalamiko kuhusu:
Ufisadi
Rushwa
Kujuana (connection)
Uhaba wa ajira uliopitiliza
Matumizi ya anasa ya pesa za umma
Huduma za elimu, afya za kusuasua n.k
We jiulize tu, hivi kwanini sekta binafsi zinahuduma bora kuliko sekta za umma kwenye elimu, afya n.k? Je, ni kweli Serikali haina fedha za kuwezesha huduma bora kama wafanyavyo Private sectors?
Sasa swali langu, hivi ni kwanini viongozi huwa hawana uwezo wa kutenda kama Wananchi wanavyopenda?
,Inamana kiti cha uongozi ukishakikalia unakuwa unaona tofauti kabisa na waonavyo unaowaongoza au inakuwaje Wakuu?
Mie ningekuwa Kiongozi Mkubwa:
1) Ningekuwa nafanya mpango wa kukusanya maoni na hoja za wananchi nao waongoza angalau kila baada ya mwezi mmoja
2) Baada ya kukusanya maoni na matakwa yao, ningekuwa nafanya analysis juu ya mawazo hayo na kuitisha mjadala wa kitaifa ambako tungejadili suala moja baada ya lingine, yaani hoja kwa hoja.
3) Kisha ningekuwa natoa mrejesho juu ya maoni ya wananchi na nini Seerikali itafanya/ inachofanya..
Haha ha haaa. Huenda haya ni mawazo fyatu lakini mwenyewe sina uhakika ya niwazacho.