Kwanini wanasiasa wengi wa Afrika wanatofautiana kimaono na wanaowaongoza/wananchi?

Wananchi hata tukiwajibika wanatufanyia figisu.!!
wao wameshika mpini, sisi tumeshika makali unadhani kuna kitu kitatokea hapo??
 
Wananchi ndio wanasiasa. Jamii Bora haiwezi kuzaa kiongozi mwizi
Sawa kabisa. Kwa mantiki nani anakosea? Ni kiongozi ama wananchi? - ki msingi ni wananchi wenyewe. Kwa sababu hawatumii mamlaka na nguvu zao kuwawajibisha viongozi wao. Na hii inajenga trend kwa kila kiongozi kwenda Kinyume na matakwa ya wananchi.

Wananchi hawaamini kuwa wao ndio waajiri wa viongozi wao. Japo katiba imeandikwa hivyo, lakini bado hawajiamini.
 
Hapo ndipo kosa la ki ufundi lilipo. Wananchi wengi hawafahamu nguvu na mamlaka walizonazo dhidi ya viongozi wao. Lait wangefahamu na kuzifanyia kazi Afrika ingekuwa bara bora sana Duniani.
Nini kifanyike??
 
Hapo ndipo kosa la ki ufundi lilipo. Wananchi wengi hawafahamu nguvu na mamlaka walizonazo dhidi ya viongozi wao. Lait wangefahamu na kuzifanyia kazi Afrika ingekuwa bara bora sana Duniani.
Jamii lazima
Tupo pamoja kaka sema tunatumia lugha tofauti, unapewaje tishrt Ili ukamchague mbunge Mwenye dhamana ya eneo lako?
 
Kitu kimoja tu: Wananchi wawajibike kwa ajili ya Taifa lao.
Kivipi sasa?
Wakitumia sanduku la kura kuwawajibisha, wanaambiwa hata mpeleke kura upinzani ila serikali itaundwa na chama chao.!!
Wakiandamana kudai katiba wanaletewa polisi na wanajeshi wafanye usafi.!!
 
Sina hakika kama kuna tofauti kati ya wananchi na viongozi.
 
Kivipi sasa?
Wakitumia sanduku la kura kuwawajibisha, wanaambiwa hata mpeleke kura upinzani ila serikali itaundwa na chama chao.!!
Wakiandamana kudai katiba wanaletewa polisi na wanajeshi wafanye usafi.!!
Wananchi wengi wanaangalia eneo la uchaguzi pekee. Ni kama vile hakuna maeneo mengine kabisa.

Unajua ni kwa nini?

Kwa sababu wananchi wengi wanadhani kwa kile kibaya kinachotokea wa kulaumiwa ni viongozi pekee. Yaani ile mentality ya kulaumu ni kubwa sana kwa wananchi walio wengi.

Kwa mfano kuna ubaya gani Jeshi kusaidia kufanya usafi mitaani?

Kuna ubaya gani kwenda mahakamani kupinga matokeo? Mbona mara kibao mahakama imetengua matokeo na kuwapa wapinzani?

Jinsi pekee ya kuwajibika ni kuandamana? Kimsingi maandamano ni njia ya kizamani sana ya kudai haki.

Mfano mwingine:

- Mazingira wanakoishi wananchi wenyewe baadhi ni machafu sana lakini wa kulaumiwa ni viongozi na sio wananchi wanaokaa maeneo hayo. Je, wananchi hawawezi kufanya usafi kwenye maeneo wanakoishi bila kusubiri miongozo ya viongozi?

- Uvunjivu wa maadili mitaani mikubwa kwa nyakati hizi. Je, ina maana wananchi hawawaoni wanaovunja maadili mitaani kwao na kuwachukulia sheria badala ya kukaa kimya na kuwalaumu viongozi?

- Michango ya sherehe vs Michango ya maendeleo ya Taifa. Kila siku kuna michango ya sherehe mbalimbali mitaani lkn hao hao wananchi hawawezi kuchanga kwa ajili ya kujenga daraja lao au kuweka kokoto kwenye barabara wanayotumia kila siku. Wa kulaumiwa ni viongozi.

Kwa kifupi sana, ni kwamba viongozi wanajitahidi pakubwa sana kwa ajili ya Taifa hili wakishirikiana na wale wananchi wanaojitolea kwa dhati kubwa kwa ajili ya Taifa lao.

Sio rahisi kuwaongoza watu wanaolalamika na kutukana matusi badala ya kusaidia. Kulaumu na kutukana ni rahisi sana kuliko kuwajibika kutatua changamoto. Viongozi wapewe maua yao.

Changamoto nyingi za wananchi zipo ndani ya uwezo wao wenyewe kiongozi hapaswi kulaumiwa
 
😹😹😹 Imebidi nicheke.!!
Kwa viongozi gani hawa wanaosema viziwi??
Yani unaongea as if wewe unaishi Mars huielewi siasa ya nchi yetu.!!
 
Mbona ushahidi upo.wazi mtu anajifanya chura kiziwi ,maoni atasikiliza je ? This Africa 😭😭😭shout and be killed
 
Laiti wananchi wenyewe wangekuwa ni wawajibika wazuri wa Taifa lao kusingekuwepo kiongozi yeyote wa kisiasa ambaye angethubutu kulichezea Taifa hili kwa sababu anafahamu wazi nini atakachokipata kwa wananchi wapenda nchi yao.
,πŸ‘πŸ‘
 
Ni kwa sababu Wananchi bado wanaamini katika ile imani iliyokuwepo zamani kwamba Uongozi ni Wito 😳
Lakini kwa bahati mbaya au nzuri kwa upande mwingine mambo yamebadilika kwa sasa uongozi una fursa nyingi za kutajirika!
Kuanzia mishahara minono na marupurupu kede kede na mengineyo mengi !

Sasa kwa kuwa ilisemwa huwezi kutumikia mabwana wawili,
Hivyo ndivyo ilivyo na itabaki kuwa hivyo !πŸ™„πŸ‘πŸ™„
 
Mkuu, umezungumza jambo zito sana. Kwamba zamani uongozi ilikuwa ni WITO ila sasa ni FURSA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…