Kwa namna ya kimwili,wakati mwingine mwili unawaka tamaa mbaya na hata akili inafikiri mawazo mabaya na kupelekea kutenda dhambi ya uzinzi.Tofauti na wanyama binadamu Mungu kampa utashi/akili ya kutambua jema na baya pia kampa UWEZO wa kushinda majaribu(tamaa mbaya,mawazo mabaya,dhambi).
1)Kwa kutumia akili Mungu alizokupa
2)kwa kutumia nguvu ya kiroho au kiimani..mfano watawa wa imani za kibudha,au imani fulani au sheria fulani zinazoweka ukanuni zinazokataza uzinzi kwa muumini wa kweli mwenye kuishi imani yake kwa matendo akiwa na hofu kubwa ya kumtenda dhambi Mungu wake au miungu yake mfano hata wanaopewa masharti na waganga wa kienyeji kwamba siku akizini atapata madhara fulani mathalani hasi ,mfano akikiuka masharti atapoteza hali/nafasi cheo/uhai atakufa,ama mtu anaogopa kumtenda dhambi Mungu wake kwa kuogopa kuvunja mahusiano mazuri na MUNGU wake /au imani yake na kuogopa madhara ya kutenda hiyo dhambi kadiri ya imani yake.
Ukiruhusu tamaa za mwili zikuongoze hii desire/kiu ya uzinzi ukiendekeza kiu hii haijawahi kutosheka na haitakaa itosheke.Ni imani ya kiroho au maamuzi magumu ya akili yako kuikataa kwa sababu za kiimani ama msimamo mkali.lakini pia pamoja na imani yako ama msimo wako hautakuwa free from kujaribuiwa na tamaa za mwili zitaendelea kuwaka kukusumbua ila kadiri muda unavyoenda utajikuta unazoea kuishi maisha ya mke mmoja bila kuchepuka na ukiongeza uhisiano wako na imani yako/kukua kiroho mwisho kabisa UTAFAULU /Utashinda fhambi ya uzinzi. Epuka vishawishi,kuwepo maeneo au kushiriki kutazama kusikiliza ama kufikiria vishawishi vya ngono.INAWEZEKANA,na tupo tuliofanikiwa kuacha uzinzi michepuko.Vitu vingine ni kujiendekeza kwa maana kuruhusu akili yako itawaliwe na kuamini imani potofu kuwa haiwezekani,ukiamini haiwezekani kwako itakuwa hivyo ila ukiamini unaweza utaweza.Kwa uzoefu wangu suala la kuacha zinaa linaamuliwa na wewe mwenyewe sio hata la kwa njia ya kuomba inabidi ianzie moyoni mwako na wewe mwwnyewe usumamie maamuzi yako kuamua kujikana kwa akili yako kisha utafute mbinu zitakazosaidia kufanikisha maamuzi yako ya KUIKIMBIA ZINAA mbinu hizo ndio hizo za kuvikwepa vishawishi,na kupalilia imani yako ya kiroho au sababu iliyokufanya uikimbie zinaa.