Kwanini wanaume huwa na michepuko?

Heloo!

Kaka zangu naomba niwaulize hivi kwanini wanaume wengi walio kwenye ndoa, au mahusuano na wenza wanakuwa hawaridhiki na kuwa na vimada nje?

Tatizo ni nini hamtoshelezwi? Tamaa, hulka au ndo asili ya wanaume kuwa na wanawake wengi? Kwa utafiti mdogo tu niliofanya kuanzia baba yangu, wajomba zangu, majirani zangu wenye wenza wao na wafanyakazi wenzangu wengi hao wanaume wana michepuko.

Wengine wake zao wazuri, kisura, kiumbo mpaka tabia ila vinafanya mpaka anatafuta kimada.

Ila ninyi wanaume mkihisi mmegongewa tu ni shida mno na hamna hat a msamaha, ila ninyi mnafanya na mnasamehewa.

Kwanini hamridhiki lakini na wake zenu.?

Mungu anawaona lakini na sasa wadada tunawakubali tu hakuna namna usawa ushakaba huu! Japo ni waume za watu.

Au ndo ule msemo MWANAUME BILA NYUMBA NDOGO NI SAWA NA TAIFA LISILO NA UPINZANI!

Ila taifa lisilo na upinzani lawezekana tu si kama Korea Kaskazini.
 
Sio kila mwanafunzi wa chuo jinsi ya kike inavyosemekana wote makahaba,,, ichukue hivyo hivyo,, wapo wababa wanao jielewa, wanachafuliwa na asilimia ndogo sana,,
 
[emoji23] [emoji23] wanawake wengi sio wa kuchepukachepuka...

nyie ndo mwapendaaa mambo hayo lazima shida iwepo!!

Kwamba wanawake wengi sio wa kuchepuka, hiyo ni dhana potofu tu.

Wanawake wengi tu huchepuka.

Huenda hata wewe ushawahi kuchepukaπŸ˜›πŸ˜€.
 
Kwamba wanawake wengi sio wa kuchepuka, hiyo ni dhana potofu tu.

Wanawake wengi tu huchepuka.

Huenda hata wewe ushawahi kuchepukaπŸ˜›πŸ˜€.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] sawa bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…