Kwanini wanaume waliooa huacha kuwashirikisha wenza wao kwenye vyanzo vyao vya mapato?

Hahah, hili la kuchangia nadhani litakupa ugumu zaidi kwenye suala la wewe kuwa KICHWA,

Vipi ni mbinu unayoitumia au unatarajia kuja kutumia?
Mkuu mimi na hustle mzee ila kwenye developments za familia lazma mwanamke nae mchango wake uonekane! One of my Qualities za mwanamke sitaki mwanamke mchoyo wala tegemezi!

Mimi sitaoa matako wala sura nzuri focus ni brain na attitude ya mwanamke mwenyewe na ambitions! Nyie mnaooa wanawake wa kufuga ili muwapelekeshe oeni tu! Ishu ni mwanamke mwenye uchungu na family na kuhakikisha tunashirikiana kujenga familia bora!
 
Mnautani nyie, nyie si ndo mnalalamika mitetewa na wana harakati kudai haki ya 50/50?

Hamkujua kua hiyo 50/50 inampa immunity mwanaume kua asionekane yeye ndio tegemezi?
Mimi pia ni mwanaume na nimeoa mkuu, umeni quote vibaya au?
 
Nilijua tayar upo ndoani unaitumia hii mbinu, nilitaka utupe experience kwenye kipengele cha wewe kusimama kama KICHWA.
 
Hamchelewi kudai 50/50.
Wakati nipo dukani Kuna mzee alikuja na mkewe kununua vitu.
Yule mzee aliingia dukani akamuacha mkewe nje.
Akaanza kutoa hela kwenye bukta yake ya ndani.akaniambia.
"Mwanamke usimuoneshe hela"
hii kanuni naitumia mpaka leo.

[emoji28]
 
Aiseee wanawake ni ma pretenders sana atakuactia bonge la picha ukahisi huyu mwenyewe ngoja aingie ndoani sasa rangi zote za rainbow zinakuwa kwako.

Hao wanawake wenye akili za maisha ni wachache sana.
Mwanamke lazma ukae nae kabla hujamuoa na wala asijue intentions zako kama ni kumuoa! Tafteni wanawake sio wasichana...Hii namaanisha wanawake ambao wako aged >=25!

This helps alot kukabiliana na vizazi vya kileo ambavyo malezi sio ya maadili yani! Mnaokotana na kupelekana lunch na dinner siku mbili 3 kisha mnatafunana na mnapanga mipango ya ndoa! Lazma mwanamke akuigizie tu😅
 
Nilijua tayar upo ndoani unaitumia hii mbinu, nilitaka utupe experience kwenye kipengele cha wewe kusimama kama KICHWA.
Mkuu mie sijaenda madhabauni tu ila practice ya ndoa nilishafanya na nina experience na hilo so nikioa nahalalisha na najua nini naenda kufanya! Siendi kujifunza kuishi na mwanamke😅
 
Wanaume wasiojielewa ndio huficha mambo Matokeo Yao hufa ghafla na kuacha familia ikiteseka, Sasa unaishije na mtu usiye mwamini na hamshirikishani mambo yenu, wanaume oeni wanawake mnaoendana nao vision
Wakuda wanawaza sisi tukifa tuuu....kufeni nyie kwanza
 
Mkuu mie sijaenda madhabauni tu ila practice ya ndoa nilishafanya na nina experience na hilo so nikioa nahalalisha na najua nini naenda kufanya! Siendi kujifunza kuishi na mwanamke[emoji28]
Sawa sawa mkuu, itakubidi upate muda haswaa kumpata wa aina hiyo
 
Sio supportive kivipi? Yani mwanaume ambaye umekuwa nae mpaka mkaoana anakuwaje sio supportive au unakuwa hujui kuwa sio supportive?
 
[emoji1][emoji1] Kuna wakati wanaume tusisubiri Hadi Mambo yatuharibikie kabisa ndio tuanze kulia Lia ....kuwa na mwanamke sio lazima , ukisha jiona kiuchumi Kuna Mambo yanatakiwa yapunguzwe ili uweze kuwa stable Basi inatakiwa ufanye hivyo.

Kuna kipindi Mimi binafsi nilikosa tenda Kama miezi nane mfululizo hivyo na kubakisha baadhi ya vitega uchumi ndio visaport kulipa bills zote . Ikatokea tv kuharibika na Kama ujuavyo hizi tv za kisasa marekebisho yake lazima mfuko ukutoboke ukweli. Pamoja na hayo yote hela ya kutengenezea au kununua nyingine ilikuwepo ila niliishi kwa hesabu Kali Sana na kujiambia hakuna mtu Alie wahi kufa kwa kuto tazama tv ila kwa kukosa chakula ......

Pamoja na yote hayo mke ndio alikua kiongozi wa kunilaumu kuwa baba Nina roho mbaya na sipendi familia yangu kwa kuto weka tv watoto waangalie makatuni binafsi sikusikiliza la mtu zaidi ya kuwaamjia Kama wanaona hapa nyumbani hapawafai kisa hakuna tv waende wanako kujua wao wataishi maisha wanayo yataka na nilikua serious hata mke angeondoka na watoto potelea mbali kwanza watakua wamenisaidia kubakiwa na bili chache ili nijijenge haraka .

So iliwalazimu kuishi miezi Kama sita hivi bila tv na wakazoea .

Hivyo Kama wewe mwanaume umenusa hali ya hatari mbele yako Anza mapema kujizatiti kukabiliana nayo , Kama ni magari yapaki uwani panda bajaji na bodaboda Hadi utakapo kuwa vizuri zaidi , usisubiri Hadi hali iwe mbaya zaidi uanze kuingia kwenye mikopo na kuuza baadhi ya Mali ndio ujijue upo kwenye Hali mbaya .

Huyo rafiki yako mwambie apaki gari atumie bajaji na hizo 2m za kila mwezi zinaweza msaidia kuongeza kwenye biashara zake na kuweza kujirudi haraka , Kama Kuna mtu anataka kutumia hizo gari akajaze mafuta kwa gharama zake ila yeye anauwezo wa kumpa mtu nauli ya bajaji ....asisubiri Hadi Mambo yawe mabaya zaidi ndio ajijue yupo kwenye wakati mgumu ...ajifunze kusoma Alana za nyakati
 
Sio wote mimi kwa mke wangu anajua kila kitu.hadi nikikosa anajua mana ntakuwa nimenuna siku nzima sina raha.ukiwa na mke anaejua maisha bora kumshirikisha kuliko kujifanya mbinafsi...rejea jamaa alieokota nyumba bunju.!!! Mume anagemshirikisha mkewe nyumba isingepotea baada ya kufa.kawanyima watoto haki yao.

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Wanaume wasiojielewa ndio huficha mambo Matokeo Yao hufa ghafla na kuacha familia ikiteseka, Sasa unaishije na mtu usiye mwamini na hamshirikishani mambo yenu, wanaume oeni wanawake mnaoendana nao vision

Kwanini familia iteseke nikiondoka? Si mama amebaki, aendeleze familia…. au sio jukumu lake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…