Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Sema tu shida yako ni uwe unachungulia wallet yangu kila saa. Ova
 
dah nimecheka sana
naona umegusa maslahi yetu ndo maana umeshambuliwa sana
umetumia muda mwingi kutetea hoja badala ya kujenga hoja hiyo ina maanaisha hoja zako zina mapungufu
 
aisee bora ufuge ng'ombe kuliko kuwa na wewe
yaani hadi kubeba mimba unaona unaonewa
50/50 bado unasema unamuhudumia mume
hivi unaelewa unachoandika
moja ya madhara ya demokrasia ni haya
unaandika pumba kisha unatetea mashudu
 
Wanaume nyinyi wa karne hii mnataka mtu kama bibi zetu(kitabia na anavyojiweka) na wakati huohuo mnataka mwanamke aliyeelimika,mpenda maendeleo,mchapa kazi n.k ili musaidiane majukumu.
Ngoja nitoke na hii nukta.

Mwanamke aliye elimika ana sifa gani,naomba uwasemee hao wadau.

Hao wanaume wa karne hii wanamuelezea vipi mwanamke mchapa kazi na mpenda maendeleo ?

Ninasema mimi Zurri ya kuwa :
Katika kitu ambacho huwa nawashangaa vijana wenzangu wa kiume ni wao kujilinganisha na watoto wa kike,wanaishi na haya mawazo ya kura veto na makongamano kwamba kusaidiana katika majukumu. Hivi tangu lini mwanamke akafanana sawa kimajukumu na sisi ? Kwanza tu kimaumbile hatufanani.

Mwanamke kiasili ni wakukaa nyumbani na kulea watoto,asubiri aletewe huu ndiyo usawa na wale waote wanao enda kinyume na hii kanuni habari wanayo,wanaugulia maumivu kimya kimya.

Nipo ....
 
aisee bora ufuge ng'ombe kuliko kuwa na wewe
yaani hadi kubeba mimba unaona unaonewa
50/50 bado unasema unamuhudumia mume
hivi unaelewa unachoandika
moja ya madhara ya demokrasia ni haya
unaandika pumba kisha unatetea mashudu
Tangu dunia inaumbwa sijapata kuona wanawake wajinga kama hawa wa kuanzia karne ya 19 mpaka hii 21. Sababu huu upofu wa haki sawa na harakati zao ndipo ulianza. Wanawake wa zama hizi wana sifa ya mshumaa,wenyewe unaungua na kuisha ukiwanufaisha watu kwa kauli mbiu ya haki sawa.

Wanajidhuru wenyewe huku wakifurahika,huwa nawaambia hakuna nazi iliyo shinda jiwe,wanajidhuru wenyewe huku wakichekelea.
 
Mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho.
Mwanamke, utazaa kwa uchungu.

Siku hizi wanawake wanakula kwa jasho na bado wanazaa kwa uchungu wakati wanaume achilia mbali kutokuzaa, hata ile kula kwa jasho inawashinda.
SABABU NI ZIPI KIONGOZI?
 
50/50 kwenye hela dada zangu nyinyi ni wagumu mnoooooo,wanawake wenye moyo wakugawa 50/50 kipato chao ktk kumi hawazidi watatu.Halafu hela yenu ni chungu huambatana na masimango na ndio maana ktk maisha yangu sitokuja kuipigia bajeti hela ya mke wangu.

Ndio maana sometimes mwanaume anaamua kumuachisha kazi mke wake sababu haoni huo msaada wa kazi yake.
 
Wanaume hkuna anaelalamika but mwanaum alyekamilika lzma awe juu ya mwanaum kimaamuz kma c hvyo lzm ugomv uwepo tu bcoz hta muumba alitaka hvo
 
Naona wewe bado ni mgeni sana na ulimwengu wa mahusiano sababu umeandika kwa namna ya mtu ambaye hana experience yoyote juu ya maswala ya ndoa.

Nitakuuliza maswali kadhaa na ukiweza kuyajibu pengine tunaweza kuwa katika mlengo mzuri kujadili hii mada yako uliyoleta!

1. Una umri gani?! Nakuuliza umri ili nijue nazungumza na mtu ambaye amepita umbali gani katika utu uzima.

2. Unayajua mahitaji ya mwanaume anayotaka kutimiziwa na mwanamke?! Usiniambie mambo ambayo umesikia, nipe wewe personally unachojua na kama haujui (for the sake of honesty and goodwill) sema sijui nielimishe ila usije na hoja mitandaoni unazookota huko kuhusu wavulana ukiita ni wanaume.

3. Nani role model wako katika haya maisha kama mtoto wakike?! Tafadhali kama katika list ya role models au role model wako hawapo katika ndoa usihangaike kujibu hili swali sababu hatutakuwa na cha kujadili kama role model wako mwenyewe ni kipofu kama wewe.

4. Ni nani aliyekuambia wanaume wanataka mwanamke mjinga au anaepelekwa kama bendera?! So kwa assumption yako ni kuwa tunawatafutia watoto wetu mama ndezi?! (una mengi ya kujifunza kuhusu tofauti ya mke bora na mwanamke wa kawaida wa kisasa)

5. Kama assumption yako ni kuwa wanaume wanalalamika (of which sina uhakika kama huwa unaelewa kinachokemewa au kupigwa kelele na hao unaoita wanaume), je umeshawahi jitathimini wewe kama binti mdogo unaeuingia utu uzima mzito kwa kasi, umejitafakari juu ya uwezo wako na mapungufu yako kwa marejeo ya uhalisia wa namna mwanamke anatakiwa kuwa, yaani kwa mfano wakisema mke bora anatakiwa kuwa na vigezo 50, wewe una vingapi na je unaweza viainisha hapa tuone namna ulivyobora?!

6. Hebu tukiacha tu mijadala na mabishano ya mtandaoni baina ya wavulana na wasichana. Wewe umejipanga vipi kuingia taasisi ndoa kwa muktadha wa mchango gani utatoa kwa mumeo mtarajiwa?! Je huyu mume atapata offer gani ya thamani kutoka kwako tukiacha kumpa mwili wako kwaajiri ya kugegedana, una kipi kipya ambacho upo taayari kutoa bila manung'uniko ya kisichana.

7. Je, ndoa kwako ni jambo takatifu na muhimu?! Kama ni ndio hebu tuambie umejiandaaje kuheshimu hilo agano na maandalizi yako kuliingia, na kama hapana, hebu tueleze ni kwann tena unajihusisha na majadiliano ya mahusiano ile hali ndoa kwako si jambo muhimu.

Jibu hayo kwanza then nikuhoji zaidi.
 
Kama wote tunaingiza kipato na kujiimarisha pamoja kuna tatizo ikiwa 50/50?
50/50 katika muktadha gani, maana sijaelewa point ya kuwa nusu kwa nusu. Kama mtu ana kipato kizuri why ahangaike na pesa ya mkewe.

Na kama mwanamke amepata kazi nzuri na kipato kikubwa kumshinda mume wake, why aanze kutaka kuomba kwa mumewe ampatie si asimamie tu gharama na kuendelea kuwa mke kwa mumewe?!

Mbona sisi wanaume tunalipa bili zote na hatuachi kuwa mume kwa wakd zetu?!

Nadhani mabinti wa kisasa mpo busy kuprove kuwa mnaweza kuwa kama wanaume kiasi kwamba mnajisahau kujifunza uanamke. Matokeo mnafika umri mkubwa na kujua hamuwezi kuwa wanaume sababu mliumbwa wanawake na pia hamuyawezi majukumu yenu ya kike sababu kutokea umri mdogo hadi mnakomaa jamii imewajaza ujinga kuwa ninyi na wanaume ni sawa, something which is biologically, scientifically, economically and politically impossible and not true.
 
Hebu nikuulize tu swali?!

Unaweza kutuelimisha huu umati mambo yafuatayo;

1. Nini maana ya neno haki?!
2. Mwanamke ana haki zipi?! Tuandikie zote tafadhali tujifunze.
3. Ni haki zipi kati ya hizo ulizosema ambazo wanawake wananyimwa hapa Tanzania au duniani na ni mazingira yapi huwa wananyimwa.
 
Naomba unipe ufafanuzi hapa.

Je, mwanaume anaheshimiwa sababu ya jinsia yake ya kiume, kama mwanadamu, kama mpenzi au kama nani hebu tupe ufafanuzi kulingana na upeo wako.
 
Ha ha ha ha ha ha bora umempa mwangaza nadhani mabinti wengi wanaongea out of insinuation na sio experience. Matatizo ya kusoma fikra taka za akina Joyce kiria mitandaoni na pia kukaa na mama zao ambao wengi wanachangamoto za maisha yao ya usichana na hawakuwahi pata psycho therapy popote kutibu trauma walizoishi katika experience zao na matokeo wanawatemea watoto wao wakike sumu za namna hii.

Study case Moshi, Mara, Arusha, Machame, etc.
 

Katika kongamano la nne la dunia la wanawake lililo fanyika septemba 15 1995 mlilofanya kule Beijing moja hasa ya lengo lake ni ku

empowering women and girls in economic growth and development.maana yake hapo wote hap tuwe na equal rights ktk job opportunities, properties, etc na aspects mbalimbali za maisha

Kwa hyo unataka 50/50 kwa jinsia zote mbili huku ukishangazwa na baadhi ya wanaume ambao mengi ya majukumu yao yanafanywa na wanawake zao sio wao ?


Wanawake bhana


Anyway hio 50/50 mnayoitaka itakua kinywani tu hapa mwendo ni mfumo dume ndo heshima itakuwepo tu sisi ndio watafutaji sisi ndio ma provider sisi ndio viongozi ndio maana kwenye jamii mwanaume kutosimamia haya majukumu utaonekana wa ajabu especially na wanawake na ni kweli unakuwa ni waa ajabu sana


So ukishangazwa na kwa nini baadhi yenu mnafanya majukumu makubwa hapo tayari tuseme usha support mfumo wa siku zote wa zamani " mfumo dume" sema upo kwenye "denial"
 
"Siku utakayo muelewa mwanamke anataka nini, inaweza ikawa ndo siku yako ya mwisho"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…