Kwanini wanaume wasasa wamekalia malalamiko na kusahau nafasi na majukumu yao kama vichwa vya familia?

Huu ni mjadala kila mtu ana haki ya kutoa mchango wake positively na negatively.Sikuuleta kutegemea watu wote wanisapoti,tunajifunza wote!
sawaaa
vipi out hutaki ?
hupendi milinda nyeusi wewe ?
 
Kwa uelewa wangu mimi mwanamke aliyeelimika ni yule ambaye ana elimu ya juu kumaanisha chuo n.k aidha ana bachelor degree au masterdegree n.k
Kama huu ndiyo uelewa wako,basi una uelewa mbaya sana na wa makosa juu ya kuelimika.

Usahihi wa mambo kuelimika ni kufanya mambo kwa uzuri yaani kuwa na tabia nzuri yenye kusifikia,kitu ambacho hata mtu wa darasa la saba au la nne anakuwa nacho. Kusoma "secular" na kuelimika ni vitu mbali kabisa. Mtu huwezi ukaitwa umeelimika ukawa unafanya vitu vinavyokushushia heshima au vinavyo dhuru afya ya akili yako,au mali yako au heshina yako au nasaba yako.

Kuelimika ni kustaarabika na kuwa na tabia njema,kwahiyo hakuhusiani kabisa na mtu kusoma sana "secular".
 
Ni kweli kielimika pia ni kustaarabika na pia kuongeza knowledge,upeo wako wa kufikiria unabadilika ukielimika.

Kuna watu wameelimika na hawajastaarabika inatokana pia na malezi n.k

Definition inaweza kuwa pana na kila mtu akaiainsha kwa upeo wake wa kufikiri.
 
Huwa unafanya 50/50 na mwenza wako ? Katika asili ambayo wanawake wanaipenda japo wanajidai wanataka haki sawa ni wao kupenda kuhudumiwa.

Lakini kama kuna mwanaume mwenzangu anakubali 50/50 na mwanamke,aisee huyo ana matatizo,huyo atakuwa ana jinsia ya kiume ila hana tabia za kiume. Jambo la mwanamke linasimamiwa na sisi.
 
Kuna wanaume wamechangia kwenye uzi huu huu wamesema wanafanya yote nloyaandika kwahio hao sio wanaume?Yaani wanasaidiana na wake zao na wamefadhaika hata nisiwajumuishe na wao!
Samahani lakini naona unawakosea heshima wanaume wenzako sio haki.Kama kwa uelewa wako mwanaume ni kubeba majukumu 100% hakuna tatizo.Ila wote hawapo kama wewe!
 
Kuna watu wameelimika na hawajastaarabika inatokana pia na malezi n.k
Bibie hakuna aliyeelimika akawa hajastaarabika,shida yako hili tamko linakushinda kulitumia aidha hulijui,wewe unalinasibisha na kusoma hizo shahada zenu,huko tunasema ni kusoma na kuelimika sasa ni kule kuwa na tabia nzuri yaani ustaarabu. Hili tamko "ustaarabu" ni tamko lenye asili ya kiarabu lenye kumaanisha tabia nzuri,kwa maana watu hao walikuwa wanasifika kwa tabia nzuri na kuwaheshimu sana wanawake,ndiyo mwenye tabia hiyo nzuri akaitwa "Mstaarabu".

Ukisoma Fizikia inakufanya vipi uelimike au uwe mstaarabu au Kemia au utabibu ?
Ni kweli kielimika pia ni kustaarabika na pia kuongeza knowledge,upeo wako wa kufikiria unabadilika ukielimika.
Kustaarabika ni matamko mawili yenye kufanana. Sema ukisoma na ukiifanyia kazi eliku uliyo isomea ndiyo unapanuka kifikra. Watu wa zamani walikuwa wanasoma fani za kimasomo na walikuwa wanasoma somo la "Tabia njema" yaani "Adabu" somo hili ndiyo liliwafanya watu waelimike na kustaarabika ila siyo yale masomo ya kifani. Yale yanakupa ujuzi ila somo la "adabu" lina kufunza namna ya kuishi na elimu hiyo katika njia nzuri,ndiyo maana ukikuta mtu au watu fulani wanasema fulani amesoma lakini hajaelimika ujue hapo wana maanisha ana tabia baya,labda hana heshima labda mlevi labda mzinzi labda ana mdomo mchafu mtu wakuropoka ropoka. Sasa tabia tabia njema huipati kwenye masomo ya juu ya kisekula tabia njema unaipata nyumbani kwenye malezi au kwenye maeneo ya mafunzo ya dini.
Definition inaweza kuwa pana na kila mtu akaiainsha kwa upeo wake wa kufikiri.
Hili halipo na mambo hayaendi hivi lazima uhalisia uzingatiwe na asili ya neno kadhalika. Ingekuwa hivyo basi hata maji kila mtu angefasili atakavyo na pasingekuwa na usawa au kukosoa.
 
Kwahio unachojaribu kusema mtu anaenda shule ili ajifunze kuwa mstaarabu?nimeshasema kwenye quote ilopita inatokana na malezi! Na ndio anastaarabika akielimika pia kwasababu anapata uelewa zaidi...

Sawa kama ndo definition yako hio nimejifunza kitu kipya kuelimika ni kuwa na tabia njema!
 
Kuna wanaume wamechangia kwenye uzi huu huu wamesema wanafanya yote nloyaandika kwahio hao sio wanaume?
Hao ni wanaume kijinsia ila si wanaume kitabia. Ndiyo maana huwa tunasema hivi kwenye Wanaume kuna Wanaume.

Bibie hatulingani kimaumbile na hatuwezi kuwa sawa katika majukumu. Mwanaume lazime asimamiwe na mwanaume,ahudumiwe,aongozwe na alindwe,sababu kiasili jambo la kutafuta au kulisha familia si la mwanamke hata kama akiwa na kipato madamu ni mwanamke yeye akae na kipato chake ila kulishwa,kuhudumiwa, kutunzwa ni jukumu langu yeye akae na hela zake,labda itokee dharura na kazima akae nyumbani.
Yaani wanasaidiana na wake zao na wamefadhaika hata nisiwajumuishe na wao!
Hao wana matatizo na kama wangekuwa wakweli wakasema wanayo kutana nayo,wangekiri hadharani.

Kama mnafanya ishu ya ushirika katika hiashara haina shida ila shrlarti msimamizi anakuwa mume yaani wewe mke unakuwa kama unamtume mumeo faida mnagawana,ila wewe unakuwa bado uko nyumbani sababu kazi yako ya kulea wana na kuwafunza ni kubwa mno kuliko hata uwe raisi wa bara zima na huko nyumbani ndipo ilipo heshima yako ya kweli.
Samahani lakini naona unawakosea heshima wanaume wenzako sio haki.Kama kwa uelewa wako mwanaume ni kubeba majukumu 100% hakuna tatizo.Ila wote hawapo kama wewe!
Bibie tunaishi hapa duniani kuyafanya mambo kwa uzuri hakuna mwanaume mwenye akili timamu majukumu yake akagawana na mwanamke,aisee hakuna.

Nikisema asili,unajua maana yake nini ? Yaani asili inataka mwanaume asimamie mambo ya wawanawake,sababu ya kimaumbile na maslahi.

Ukweli wote wanatakiwa kuwa kama mimi sababu mimi ninarejea katika asili na kiangalia maslahi dhidi ya ufisadi.
 
Kwahio unachojaribu kusema mtu anaenda shule ili ajifunze kuwa mstaarabu?
Kwanza shule gani katika hizi ambazo watu wanauenda kusoma ili wajifunze ustaarabu kwanza huo ustaarabu huko mashuleni haupo.

Huko mashuleni waende kujifunza na kuzifanyia kazi elimu hizo.

Uhalisia watu wanaenda mashuleni ili wawe madaktari,wawe wahandisi wawe walimu,wawe wanasiasa mwemisho wa siku wapate hela waishi maisha mazuri,yaani wengine wanasema wapate "gamba".
 

Not even a joke Chief!

Wavulana wasiojielewa wanataka kuchafua sifa ya wanaume wachache waliosalia.
 
" ..... hilo halina discussion..." yaani matumizi yako ya maneno yanaonyesha we ni mwanamke wa namna gani. Jamaa yetu ana kazi sana. Ila una option ya kutafta mwanaume unayetaka wewe awe unavyotaka maana kama ndoa yako unaona haina furaha nikuhakikishie tu kuna ndoa zina furaha saaaana .
 
Mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho.
Mwanamke, utazaa kwa uchungu.

Siku hizi wanawake wanakula kwa jasho na bado wanazaa kwa uchungu wakati wanaume achilia mbali kutokuzaa, hata ile kula kwa jasho inawashinda.
wanaikimbia nature yao
 
hahaahaaa[emoji3][emoji3][emoji3] inasemekana ndoa za mwanamke aliyeajiriwa zina migogoro sana
 
Not even a joke Chief!

Wavulana wasiojielewa wanataka kuchafua sifa ya wanaume wachache waliosalia.
Inabidi tusawazishe habari, if only for the record.

Wengine kuhudumia familia ni utamaduni wenye historia ndefu, tumeurithi na tunarithisha kwa mfano mzuri.

Jadakiss anakwambia.

"My little boy is 7, he's the sequel to the thug
So I told him the money will never equal the love"

"When it comes to my family, it ain't never a problem it's only a phonecall".

 
Sasa tuna Madam President, ndiyo kichwa cha familia ya Tanzania, tafakari swala la kichwa cha familia, kwa sasa hakuna cha kiume au kike...😑😠🀬
 

Absolutely Brother!
 
mkuu haujawi niangusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…