Kwanini wanawake hamna huruma?

Kwanini wanawake hamna huruma?

Na wewe usimpangie mwenzako,umenunulia simu na bando kwani?pambana na hali yako

Kama unapiga nyeto ni wewe huko,acha alalamike
Mkuu mbona unalia lia sana?

Una tatizo siyo bure
 
The best lesson to teach a person to hv descipline over resources is NOT TO HAVE IT, vinginevyo mtaishia kugombana
 
Kwahiyo kuku wakipewa chakula unateseka? Ulitaka wakule nini, acha wivu na kulialia kizembe tafuta pesa.
We jamaa bhana sijui hujasoma? jamaa kaandika fact tupu..Kwan we familia uliyo toka wazaz wako walichezea chakula ?? Dah...mnaendekeza tabia za Kishamba Sana akat wabongo wengi maisha yetu karibia Yana fanana
 
Hela za matumizi ya chakula humkabidhi zote isipokuwa kuna wakati ananiomba nimletee baadhi ya vitu
Hii tabia tunaipenda tunategea wakati mnarudi lazima tuombe mje na kitu tuu hahaaa. Any way pole mkuu endelea kusisitiza ataacha
 
Umshazaliwa, ukanyonya ukatunzwa km maskini sasa leo umekua na ndevu unaona wanawake hawana Huruma??hana huruma kwakuwa tu haendani na mawazo yako siyo?

nikisema ulikuwa unastahili kunyofolewa hiyo mimba nitakosea? yaani ulikuja bahati mbaya tu humu Duniani!
 
Umshazaliwa, ukanyonya ukatunzwa km maskini sasa leo umekua na ndevu unaona wanawake hawana Huruma??hana huruma kwakuwa tu haendani na mawazo yako siyo?

nikisema ulikuwa unastahili kunyofolewa hiyo mimba nitakosea? yaani ulikuja bahati mbaya tu humu Duniani!
Mna huruma kwa watoto wenu tu, hamna huruma ya moja kwa moja na yeyote!
 
No shade, but mkeo aliwahi kuwa housegirl? Maana hao ndo wana mentality ya vitaletwa tu...
Au anagawa mtaani, au anauza pia... 10ltr ya mafuta per month mhh
Uko sahihi.
Mimi huyu wa kwangu japo nae nimekaa nae mwaka wa 3 huu.
Mwanzoni aliniletea hizo pigo za kupika chakula kingi na kumwaga.
Aiseee nilimuambia nakupa likizo ya wiki moja ukakae kwenu.
Maana kwao hali ya uchumi ni mbaya sana.
Nikamnunulia na vikontena vya buku buku viporo vikibaki anahifadhi, si lazima kesho yake viliwe mara nyingi viporo vinaliwa jumapili mchana na jumatatu mchana.
Alhamdullilah amerekebika na anaelewa.
Mara nyingi kiporo cha wali huwa anaywea chai.
Ugali unapikwa wa kuliwa muda huo.
Akimaliza kusonga kila mtu anawekewa kwenye sahani yake.
Umwagaji chakula ni tabia mbaya sana yaani ovu mno huu ni ujangili wa aina nyingine.
Ninachukia vibaya sana.
Nimekulia kwenye familia iliokuwa inapika mama ntilie, niliona nikiwa mdogo sana watu wanavyokuja kuomba mabaki ya vyakula ya wateja walau wapate kula.
Yaani nilifundishwa mteja akimaliza kula kabakiza chakula nakichukua nakihifadhi vizuri kuna watu walikuwa wanakuja kula na wanashukuru.
 
Maharage watu wanachemsha kwenye gesi wakati mkaa upo. Mtu anaona uvivu kuanza kuwasha mkaa
Maharage yanachemshwa kwenye mkaa au electric pressure cooker.
Tena yanachemshwa ya kupikwa awamu tatu na kuendelea.
Yanapakiwa kwenye vikontena.
Yanawekwa kwenye frizi.
Siku ya kupika anayadefrost tu anaunga 😋
Hii inasave bajeti na muda.
 
Kuna wanawake ni kichefuchefu hasa kwenye bajeti ya menu hasa Hawa wanawake mabonge nahisi hata mkeo atakuwa binge nyanya! Kutupa Chakula. Ni dhambi mbaya sana kwanza unajikosesha ridhiki kabisa IPO siku hutakuwa na kitu ndo utajua kile ulichokitupa kina thamani gani? Mwanamke asiye ana uchungu na Mali atakurudisha nyuma kimaendeleo huwezi kusonga mbele ! Sasa badili mfumo wa manunuzi acha kununua vitu vya jumla mletee kila siku kilo moja ya unga na mchele na mafuta ya kupima Ili ashike adabu
 
Ukweli ni kwamba mtu yoyote ambae hatafuti hela kwa jasho, hua hajui kupanga matumizi.

Wasichana wa kazi na hawa wadogo zetu tunaoishi nao jamani sijui hua wanadhani sisi ni matajiri sana? Mtu atabandika MAJI YA KUOGA (na joto lote) kwenye jiko la GESI! Halafu anayasahau hapo yeye yuko chumbani na simu. Maji yatachemka wee mpaka yanakaukia we unapita unakuta maji yamebaki nusu, yeye hana habari, akikurupuka anajazia sufuria anaendelea kuchemsha! Au mwingine anachemsha maji, yakichemka anazima jiko anaenda kufanya shughuli nyingine. Akija anawasha tena jiko anayachemsha upya ndio akaoge!
TV ni masaa 24 ipo on, kuwe kuna mtu anaangalia au laa. Taa zote ni on hakuna anaezima.

Yaani kuna vitu vinakera sana mtu unaongea mpaka unachoka
Halafu ukiongea unaonekana una nongwa!..mimi nkiongea mtu akajinunisha huwa namwambia "siku ukipata majukumu utanielewa"
 
🥲I feel you ..Saivi ndo nakumbuka enzi tukiwa wadogo mama akiwaekea chakula mkashindwa kumaliza mnapanga mstari mnafungua mdomo mnalishwa kilazima [emoji28]nilikua nachukia ila nimekua sasa namuelewa na naishi na hio mentality.
Apo unakuta unalishwa msosi adi unasinzia na unaamshwa na pande la Kofi .
 
Ulu
Ulishawahi kutoka na mwanamke wa mjini sister du fulani out? Akiletewa menu anaagiza nusu kuku na chips alafu anakula kiupaja kimoja na vichips kadhaa anajifuta na tishu kwa mikogo vingereza vingi alafu anakwambia ameshiba! 🤔

Wanaume tumeumbwa mateso hadi kwenye ndoa yanatukuta haya. Leo naongelea wanawake walioolewa au wanaoshi na wanaume kama familia, kwanini wengi wao wana tabia hii? KUTUPA CHAKULA!!! 😭

Nikijitolea mfano mimi binafsi nimetoka familia masikini, Mungu kanijaalia nna kipato cha kubadilisha mboga kwa sasa. Kwakuwa chanzo kikuu cha mapato ni mshahara basi huamua kununua vyakula vya jumla kila mwisho wa mwezi mf. mchele,unga, mboga kama maharage, dagaa, samaki, nyama ya ng'ombe, kuku n.k yani kiufupi mwisho wa mwezi friji inakuwa top kwa mazagazaga na huwa tunapanga kabisa na mke wangu anunue vitu kiasi gani lakini matumizi ya vitu hivi yanakuwa ya hovyo sana hadi kupelekea kitu fulani kuisha mapema kabla ya muda mliojiwekea. Na hata ukimuuliza kuhusu pesa ya matumizi uliyompa tofauti na ya manunuzi ya vitu hivyo utaambulia patupu.

Kuna jambo wanawake hawawezi kubajeti kabisa hasa kipimo cha chakula. Unakuta mchana wanapika ugali mkubwa hadi jioni unatoka kazini unakuta hotpot limejaa ugali na mboga kibao zimebaki wote wameshakula na mimi huwa sili nyumbani mchana siku za kazi. Usiku pia wanapika wali kibao unabaki, asubuhi hauliwi wote sababu kuna mkate au mwanamke kajisikia kupika tambi au chapati, mchana unakuta sufuria limelowekwa na mpunga kibao mwisho wa siku wanapewa kuku wale....

Nimeongea kwa ujumla wanawake maana hiki ni kilio cha wanaume wengi tunaofatilia mambo ya jikoni. Siwafichi mimi huwa nafatilia mambo ya jikoni.

Nna rafiki zangu wengi, ndugu zangu na jamaa wanaoishi maisha ya shida sana, mfano jana nilipigiwa simu na rafiki yangu ananiambia hadi muda huo (saa 2 usiku) hajajua watoto watakula nini akaniomba nimsaidie kumtumia buku mbili tu japo anunue mkate. Si kwamba napesa nyingi lakini najua uhalisia wa anachoniambia sababu haya maisha nimeyaishi nilipambana nikamtumia hela ya kula siku hiyo.

Nikirudi kwa mke wangu mimi hajali kabisa unaweza kushangaa baada ya siku 15 tu anakwambia mchele karibia unaisha, namuuliza mmetumia mchele kilo 30 kwa siku 15?! Jibu lake rahisi anajibu 'unadhani mimi naumwaga, si watoto wako wanakula!' Mwanamke mwenyewe katoka familia hizi hizi kama zetu sijui kwanini hana uchungu!

Lakini si wote kuna wanawake wanajua kubajet aiseee... Kama shemeji yangu mama Alice nakumbuka wakati huo tunaishi nae nyumba moja na mume wake(rafiki yangu). Huyu mwanamke hatumii kwasababu vipo tu, nisiseme mengi.

Kama kusema nilishasema sana sasa hivi naumia tu maana ukizidi kuongea hawachelewi, utasikia "We mwanaume una gubu kweli, mambo ya jikoni yana kuhusu nini?"

Ah! Basi bana, namwachia Mungu Uluo
Ukiona mwanaume kafanikiwa basi ni akili yakewe
 
Umshazaliwa, ukanyonya ukatunzwa km maskini sasa leo umekua na ndevu unaona wanawake hawana Huruma??hana huruma kwakuwa tu haendani na mawazo yako siyo?

nikisema ulikuwa unastahili kunyofolewa hiyo mimba nitakosea? yaani ulikuja bahati mbaya tu humu Duniani!
Sijui umesoma nilichoandika ama umeishia kusoma kichwa cha habari tu? Kama hukuelewa, sikuwa na maana ya wanawake wote hawana huruma bali wale wenye tabia hizo nilizozitaja.
 
Back
Top Bottom