Kinyume cha ushenzi ni ustaarabu na kinyume cha unyama ni ubinadamu, hivyo kadiri miaka inavyozidi kwenda watu wanaojitambua wanachagua kuishi kiustaarabu na kibinadamu zaidi tofauti na walivyoishi kinyama na kishenzi zamani.
Kumpiga mwanamke bado ni kosa, ni uhalifu na ni aina fulani ya ukatili, unyama na ushenzi fulani hivi, haijalishi kama ni zamani au sasa, haijalishi kama walivumilia au hawakuvumilia. Miaka za zamani mfumo dume ulikuwa na nguvu zaidi, elimu na uchumi wa kipato ulishikiliwa na wanaume zaidi, hivyo kuwafanya wanawake wengi kuwa wanyonge, duni, wasio na elimu na walishindwa kutambua haki zao, hivyo walipopigwa hawakuwa na ufumbuzi mbadala na wala hawakuwa na pa kukimbilia.
Hivi sasa wanawake wengi wana elimu ya kutosha kutambua haki zao, wana uwezo wa kuhoji, wana nguvu ya kiuchumi sawa au zaidi hata kuliko wanaume wengi, wanajitambua na wanaweza kutafuta ufumbuzi kwa njia mbali mbali na pia kuna misaada mingi ya kisheria n,k
Ni mjinga pekee anayeweza hata kufikiria kumpiga mwanamke, jambo bora analoweza kufanya mwanaume kwa miaka ya sasa ni kutafuta fedha kwa nguvu zote kwa ajili ya kumlisha mwanamke wake na familia yake na atumie miaka yote ya maisha yake ajifunze kuhusu kiumbe mwanamke.