Wanawake kutoolewa naweza nkasema kunasababishwa na vitu vitatu.
1.Kujisikia kwao na kuringa pasipo na sababu za msingi.Unaweza ukamtokea binti kwa nia njema tu lakini akawa analeta nyodo na maringo.Pia wengine wanakuwa na masharti magumu sana zaidi hata ya waganga,mara uwe na gari aina flani,huwe na hela za kutosha n.k. Wanawake wa dizaini hii huwa wanakosaga watu wakuwa nao maisha kwasababu ya masharti yao ya ajabu ajabu na tamaa.
2.Sababu ya pili naweza nkasema kitenda cha sisi wanaume kupiga na kuacha mara kwa mara kinachangia kwa kiasi fulani.Just imagine msichana ambaye ameshaangukia ktk bad relations mara nyingi,hufikia wakati anakosa imani na kila anayekuja,matokeo yake umri unaenda .
3.Hii sababu ya tatu pia inarudi kwetu tena mens.Wengi tunapenda ule msemo wa Mwana FA kuwa bado tupo tupo kwanza.Just imagine kijana anaamua kutooa mpaka ajipange vizuri kimaisha kwanza,let say kwenye 35 ndio anaamua kuoa,unadhan atamuoa yule waliyekuwa wote chuo??(wa umri wake).Ni kitu ambacho ni nadra sana,hapa atatafutwa mwenye 20's ndio atawekwa ndani.Yule wa 35 je?? Kwa style hii wengi huwa wanakuwa na mawazo sana.
But mimi ningewashauri dada zangu kutatua matatizo yaliyo upande wao mfano kuringa,dharau n.k...alafu yaliyo upande wetu sisi Mwenyezi Mungu atawapigania.
#Analyse
Jibu Mubashara Hili Hapa
Mwanamke anapigiwa simu kwa namba ngeni, anauliza namba yangu umeitoa wapi? Usiponiambia aliyekupa usinipigie. _HAPO UMEPISHANA NA MUME_
Mwanamke anaingia ndani ya daladala, amekaa na mwanaume, kwa maringo, anachukua earphone na kuweka masikioni na kuwasha mziki ili asiongeleshwe. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke anasalimiwa njiani, anaitikia, akiongeleshwa tena anachuna. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unatumiwa meseji inbox, hujibu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unapigiwa simu na mwanaume, unaona kabisa anakupigia ila hutaki kupokea tu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unakwenda gheto kwa mwanaume, una mkoba wako, ukifika muda wa kuondoka unaomba nauli. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unakwenda kwa mwanaume, badala ya kusonga ugali, cha kwanza unataka chipsi kuku. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unaanza uhusiano na mwanaume, siku ya pili tu unamwambia bebi sina hela ya vocha. _HAPO UMEPISHANA NA MWANAUME._
Mwanamke upo na mwanaume, anakwambia agiza chochote, bila kujishtukia unaagiza bia. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unachati na mwanaume, chatting zako ni K, P, Pw. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unaweka picha mapaja wazi, kifua umebust. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
Mwanamke unamwambia mwanaume akutumie video za ngono kwenye simu. _HAPO UMEPISHANA NA MUME._
_Usilalamike kwamba kwa nini mpaka sasa hivi hujaolewa. Taambie sasa wewe she ni mara ngapi umepishana na mume!_
Sent using
Jamii Forums mobile app