Kwanza kabisa unatakiwa ujitambue......na hatua kubwa kwenye kujitambua ni kujitoa kwenye utumwa wa matamanio.......
Sio kila kitu ambacho nafsi inakutuma kukifanya basi ni kizuri la hasha......
Pili unatakiwa ujitoe katika ulimwengu wa fikra na uje katika ulimwengu halisi ili utambue....ubaya wa jambo ambalo umeshalifanya na unataka kulifanya......
Ni jambo ambalo linakutoa katika ubinaadamu.....na pia linakutoa katika mikono ya neema za Mungu......ni jambo ambalo kwa macho ni la kawaida....ni jambo nzito sana mbele za Mungu.....,
Mwanadamu hawezi kuishi salama kwa kutimiza matakwa ya nafsi yake bali yale yampendazayo Mungu.....na hilo ni jambo lenye kumchukiza Mungu.......
Kama unaamini kuwa kuna siku ya mwisho na kila mtu atalipwa kutokana na matendo yake....achana na ufirauni huo.......,
Mshinde shetani.....achana na uchafu huo.....tubu yale yaliyopita anza mwanzo mpya........
Madhara yake ni muda mrefu na yanatesa........
NB; MCHUMA JANGA HULA NA WA KWAO.....