Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mpaka sasa wapalestina ni wananchi wa Israel. Palestine (Gaza na West Bank), ni mamlaka tu ya ndani.Katika mgogoro wa Israel na Wapelestina ni wazi mpango wa mataifa mawili kama umeshakufa kimya kimya. Fursa moja kubwa iliyobaki ni uwepo wa taifa moja lenye kujumuisha jamii zote mbili za Wayahudi na Wapalestina kama raia walio sawa katika taifa moja.
Inawezekana Siku moja Wapestina wakakubali haiwezekani tena kuwa na taifa lao tofauti na Israel na wakataka kuwa sehemu ya Israel?
Itakuaje wakitaka kuwa raia kamili wa Israel na watambulike rasmi kama raia wa Israel wenye haki zote za taifa la Israel?
Kabla ya shambulio la October 7, mwakajana, wapalestina wengi, hata ajira zao ilikuwa ni ndani ya Israel, na wapo wapalestina wanaoishi ndani ya Israel, waliogoma kwenda huko kwenye mamlaka ya ndani.
Israel haijawahi kuwakataa wapalestina, hata mwaka 1947, Wayahudi walitaka liwe Taifa moja, bali wapalestina, kwa kushawishiwa na nchi za Kiarabu, ndio waliokataa.
Na kwa kweli kama wapalestina wangeijiwa na hekima, hilo la kuwa nchi moja inayoheshimu na kuwapa jamii zake zote haki sawa, lilikuwa ni chaguo zuri sana, na ingewafanya wapalestina kuwa na maisha bora maradufu ya walivyo sasa, na hata walivyo wananchi wa Iran, Lebanon au Jordan. Wao wangepigania kuwa na haki maalum za kikatiba, ambazo zingeingizwa moja kwa moja kwenye katiba, kama vile lazima nafasi fulani ndani ya Serikali zishikwe na wapalestina, au lazima idadi fulani ya wapalestina wawepo kwenye uongozi wa juu wa nchi. Hiki wanachokipigania sasa, na kwa mazingira ya uhasama uliopo, ni vigumu sana Israel kuridhia. Hawatakubali wawe na adui mlangoni pao.